UDA: Hatujafilisika na hatuna dalili za kufilisika

UDA: Hatujafilisika na hatuna dalili za kufilisika

Asilimia 5000 yamamazenu mnakuwakama amjasoma asilimi mwishongapi
 
Jamani Kisena hata wewe unafikiri utawadanyanya Watanzania milele? hizo hadithi mwambie Masaburi, Riziwani na JK Msoga band wezi wenzako, Masaburi alliitwa kwenye mdahalo akasema yuko ikulu anafuturu, jasho la wananchi wa Dar Es Salaam wengine leo marehemu mmelipoka wewe na familia yako kwa faida ya aliyekuwa Rais, Kampuni iliyokua inaenda vizuri mkaipapura maana uongozi wa biashara hauujui ni wizi tu, mkaenda mkapewa na godown iliyokuwa na mabasi ya Scandinavia mkaigeuza ofisi ya wanyantuzu watano mamia ya watu wakapoteza kazi, mabasi yamechoka mkapewa njia za upendeleo za daladala wengine wakafukuzwa, bado hamjashiba na huyo mpumbavu aliyewaingiza kwenye mwendo kasi akae chonjo, time has come uongo wa asiyesoma na ukweli wa wasomi hauwezi kukaa chungu kimoja, unajifanya mbabe kwa kuwa wakati wa JK ulimzaba vibao mkuu wa kituo huko kwenu, tulikuangalia sasa wakati wako umefika, andaa pamba na taulo la kufuta usaha, hivi tutaendeleje kuwa na nchi ya amani kama watu kama nyie mnaendelea kutupora mali zetu? kama wewe mfanyabiashra kwa nini huendi kuanzisha chako, JPM tunataka huyu mtu atolewa na kuwekwa mbali kabisa na mradi wa BRT ili tuvuke hapa salama
Mkuu umeandika kwa uchungu na uzalendo wa hali ya juu sana...hongera sana mkuu....tupo wachache sana wenye kuumiza na haya yanayoendelea hapa nchini...
 
Tunawataka washindani wetu waache tabia ya fisi ya kumfuata mtu anayetembea kwa haraka wakidhani atandondosha mkono wapate kitoweo vinginevyo watakufa njaa.
Hawa washindani wao ndio akina nani ....WAZAWA CITY BUS LIMITED!????
 
Wasituchanganye huko na sie tupo serikalini eti tunajua yanayoendelea kimsingi kampuni haikuwi kwa hizo asilimia 5000 huu ni uwongo
Duuuuh sikia hii. "NDANI YA MIAKA MITATU KAMPUNI YETU IMEKUA ZAIDI YA ASLIMIA 5,000".
Hatari
Ukuaji wa kampuni kwa asilimia 5,000 kwa kipindi kifupi cha miaka 3?

Hii haijawahi kutokea popote duniani, na kama itakuwa kweli UDA itakuwa imekua kwa kiasi kikubwa kwa kiasi hicho, basi itakuwa imejiwekea rekodi mpya ya dunia!
 
Tushachoka na kelele,Uda uda uda,we need to move on,
kama Uda ingekuwa deal chafu kama mnavyoongelea humu jpm si angeshachukua hatua?
We need to work peoples,hizi kelele miaka nenda rudi is un productive
 
hawa majamaa

kapuya
idi simba
masaburi

hawaaa binafsi bila uda ni majipu
ukitia na uda ndo kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
m uda chin ya kisena siwapendi, kunawakati huwa natamani nisipande magari yao, na simply reson, ni kuwa wameongeza gharama za maisha ya usafr jijin dar, yaa wamekuwa kama miungu watu, nlitamani shirika liendeshwe na jj la dar..

kufirisika na ufisadi huenda vipo m sina uhakika ila jf ina data za watu wote hli jambo huenda likawa la kweli,
 
either wamefilisika ama la, bado na sisitiza Investigation Audit lazima ifanyike tuone namna gani walivyonunua hili Shirika la umma, na pia je kodi zote wanalipa...
Ukaaji kimya wa serikali unanikera kwa hili....
 
HA HA HAAAAAAA huku kukua kwa Kampuni hii ni hatari aiseee, wanajamii forum ngoja niwarahisishie alivyopata growth rate ya 5000% amefanya simple calculation ifuatayo:

alikuta mabasi 7 na sasa yako 400 so kwake yeye asilimia za ukuaji ni kama ifuatavyo:

=400/7*100=5714% lakini jambo la kujiuliza cashflow yake iko wapi ili tujue kipato chake na wanaomdai kama vinaendana bila kuathiri ukuaji wa kampuni yake.


Hizo ngoja zitakwisha akituletea Balance sheet yake na Cash Flow statement ili ifanyiwe interpretations na kuona ratios kama ziko standard ama la.


TAARIFA KWA UMMA

Mafanikio haya ya Kampuni ya UDA yanatokana na umahiri wa uendeshaji kutoka Simon Group chini Uongozi thabiti wa Mwenyekiti wake Ndugu Robert Simon Kisena na si vinginevyo, kama washindani wetu wavyojaribu kutuchafua kwamba kuna wanasiasa nyuma yake.

Tunawataka washindani wetu waache tabia ya fisi ya kumfuata mtu anayetembea kwa haraka wakidhani atandondosha mkono wapate kitoweo vinginevyo watakufa njaa.

Imetolewa na Uongozi wa SHIRIKA LA USAFIRI DAR ES SALAAM (UDA) LIMITED
 
Tushachoka na kelele,Uda uda uda,we need to move on,
kama Uda ingekuwa deal chafu kama mnavyoongelea humu jpm si angeshachukua hatua?
We need to work peoples,hizi kelele miaka nenda rudi is un productive

Umemaliza?
 
TAARIFA KWA UMMA


Kumekuwepo na taarifa za uwongo kwenye vyombo vya habari, hasa kijarida cha Dira ya Mtanzania, na mitandao ya kijamii kuhusu uongo kuwa kufilisika kwa Shirika la Usafiri Dar Es Salaam (UDA) Limited.

Menejimenti ya Shirika la Usafiri Dar Es Salaam inakanusha uwongo huo kuwa UDA haijafilisika na haina dalili zozote za kufilisika isipokuwa ni Shirika la namba moja nchini na Afrika Mashariki na Kati linalokuwa kwa kasi ya ajabu kimaendeleo na kibiashara.

Zifuatazo ni takwimu zinazodhihirisha ukweli huu:

  1. UDA imeongeza idadi ya mabasi kutoka mabasi 7 makukuu na mabovu Mwaka 2012 na kufikia takribani mabasi 400 mwaka 2015 yakiwemo mabasi 255 ya kawaida na mabasi makubwa - Hercalus, mapya na ya kisasa kabisa duniani (ya BRT) 140.
  2. Ndani ya miaka 3, kampuni ya UDA imekuwa kwa zaidi ya asilimia 5,000
  3. Kampuni hii imeweza kufanya maandalizi yote ya kuwezesha kuendesha mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART Project) kwa ufanisi mkubwa. Mbali na kununua mabasi, kampuni imeweze kununua mtambo bora na wa kisasa kabisa duniani wa kukusanya nauli na kuongezea mabasi (Intelligent Transportation System – ITS) wenye thamani kubwa kutoka Ubelgiji na Ujerumani. Vile vile kampuni imeweza kusaili na kufundisha madereva wa Kitanzania zaidi ya 300 na kuwaajiri kwa ajiri ya kuendesha mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART Project)
  4. Kampuni imejenga karakana bora na imara na kununua vitendea kazi vya kisasa kwa ajiri ya mabasi yake ya kawaida na mwendo haraka.
  5. Kampuni imepeleka watendaji wake kwenye miradi mbalimbali ya BRT duniani ili kupata uzoefu wa kuwawezesha kuendesha mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART Project) kwa ufanisi. Vile vile Kampuni imeweza kuajiri wataalam kutoka nje (expatriates) kwa ajiri kuongezea nguvu wataalam wake wa ndani.
Kwa takwimu chache hizo hapo juu, Kampuni ya UDA ni namba moja Afrika kwenye sekta ya usafirishaji wa abiria barabarani kwa idadi ya watu inaosafirisha, idadi ya mabasi na ubora wa menejimenti.

Mafanikio haya ya Kampuni ya UDA yanatokana na umahiri wa uendeshaji kutoka Simon Group chini Uongozi thabiti wa Mwenyekiti wake Ndugu Robert Simon Kisena na si vinginevyo, kama washindani wetu wavyojaribu kutuchafua kwamba kuna wanasiasa nyuma yake.

Tunawataka washindani wetu waache tabia ya fisi ya kumfuata mtu anayetembea kwa haraka wakidhani atandondosha mkono wapate kitoweo vinginevyo watakufa njaa.

Imetolewa na Uongozi wa SHIRIKA LA USAFIRI DAR ES SALAAM (UDA) LIMITED
Hii taarifa inaonesha kweli shirika linafilisika. Haijagusia chochote kukanusha kilichoandikwa na gazeti. Hoja ni kwamba UDA imefilisika kutokana na madeni yatokanayo na kukopa fedha, Deni la TRA (PAYE) na deni la NSSF (michango ya watumishi). Nyie mnajitete kwa kutaja idadi ya mabasi tena ya mkopo. Bye UDA
Hivi Bw. Iddi Simba ana nafasi gani ya uongozi ktk kampuni hii? na je Ushauri uliotolewa na kampuni ya EY kuhusu hatma ya mradi huu na uendeshaji wake, taarifa yake inaweza kuwekwa HADHARANI? UDA kuwezi wakweli
 
Time will tell... wacha waruke ruke tu ila wajue Uncle Magu anawaangalia tu!
Hawajui siku wala saa.. Tanzania ya yule msanii sio hii ya Uncle Magu.
 
Ajabu ni kwamba hakuna mwizi duniani ambaye hakuwahi kujulikana. Wezi wanafikiri hawajulikani, wako kama kenge anayekimbilia majini akikimbia matone ya mvua. Wizi ni uongo, it is a negative energy. It has limits. Huyu aliyesema za mwizi ni arobaini alimaanisha kuwa mwizi hawezi kusurvive milele. Hapa UDA ndio arobaini yenu imekaribia.
 
Eti cashflow,sijui financial statement na mambo ya kulipa kodi,hivi mnadhani wanaweza kuleta ripoti zao jf?,
kama serikali inahitaji takwimu hizo inaweza kuzipata ndani ya dakika kumi tu
 
Wamesahau kuorodhesha Barabara za mwendo kasi. .....!
 
Back
Top Bottom