UDA: Hatujafilisika na hatuna dalili za kufilisika

TJM255

Member
Aug 20, 2015
7
2
TAARIFA KWA UMMA


Kumekuwepo na taarifa za uwongo kwenye vyombo vya habari, hasa kijarida cha Dira ya Mtanzania, na mitandao ya kijamii kuhusu uongo kuwa kufilisika kwa Shirika la Usafiri Dar Es Salaam (UDA) Limited.

Menejimenti ya Shirika la Usafiri Dar Es Salaam inakanusha uwongo huo kuwa UDA haijafilisika na haina dalili zozote za kufilisika isipokuwa ni Shirika la namba moja nchini na Afrika Mashariki na Kati linalokuwa kwa kasi ya ajabu kimaendeleo na kibiashara.

Zifuatazo ni takwimu zinazodhihirisha ukweli huu:

  1. UDA imeongeza idadi ya mabasi kutoka mabasi 7 makukuu na mabovu Mwaka 2012 na kufikia takribani mabasi 400 mwaka 2015 yakiwemo mabasi 255 ya kawaida na mabasi makubwa - Hercalus, mapya na ya kisasa kabisa duniani (ya BRT) 140.
  2. Ndani ya miaka 3, kampuni ya UDA imekuwa kwa zaidi ya asilimia 5,000
  3. Kampuni hii imeweza kufanya maandalizi yote ya kuwezesha kuendesha mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART Project) kwa ufanisi mkubwa. Mbali na kununua mabasi, kampuni imeweze kununua mtambo bora na wa kisasa kabisa duniani wa kukusanya nauli na kuongezea mabasi (Intelligent Transportation System – ITS) wenye thamani kubwa kutoka Ubelgiji na Ujerumani. Vile vile kampuni imeweza kusaili na kufundisha madereva wa Kitanzania zaidi ya 300 na kuwaajiri kwa ajiri ya kuendesha mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART Project)
  4. Kampuni imejenga karakana bora na imara na kununua vitendea kazi vya kisasa kwa ajiri ya mabasi yake ya kawaida na mwendo haraka.
  5. Kampuni imepeleka watendaji wake kwenye miradi mbalimbali ya BRT duniani ili kupata uzoefu wa kuwawezesha kuendesha mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART Project) kwa ufanisi. Vile vile Kampuni imeweza kuajiri wataalam kutoka nje (expatriates) kwa ajiri kuongezea nguvu wataalam wake wa ndani.
Kwa takwimu chache hizo hapo juu, Kampuni ya UDA ni namba moja Afrika kwenye sekta ya usafirishaji wa abiria barabarani kwa idadi ya watu inaosafirisha, idadi ya mabasi na ubora wa menejimenti.

Mafanikio haya ya Kampuni ya UDA yanatokana na umahiri wa uendeshaji kutoka Simon Group chini Uongozi thabiti wa Mwenyekiti wake Ndugu Robert Simon Kisena na si vinginevyo, kama washindani wetu wavyojaribu kutuchafua kwamba kuna wanasiasa nyuma yake.

Tunawataka washindani wetu waache tabia ya fisi ya kumfuata mtu anayetembea kwa haraka wakidhani atandondosha mkono wapate kitoweo vinginevyo watakufa njaa.

Imetolewa na Uongozi wa SHIRIKA LA USAFIRI DAR ES SALAAM (UDA) LIMITED
 

Attachments

  • TAARIFA KWA UMMA.pdf
    359.5 KB · Views: 99
Liabilities zikizidi assets zako.....unafilisika tu, haijalishi thamani ya hizo assets zilizopo. Kama madeni ni trilioni 1 na assets ni bilioni 500....unaweza kuwa mufilisi tu!

Walioshindwa kulipa kodi za TRA ili ku clear mabasi bandarini ni hawa UDA au wengine? Kushindwa kulipa madeni ni dalili ya kuelekea kufilisika.
 
Hawa UDA wamekaa kimipasho flan ivi, ngoja nao waje watumbuliwe maana ni jipu uchungu lililoiva kabisa hili.
 
Taarifa haina thamani ya mtaji wa kampuni kabla na baada,madeni wala gharama za manunuzi za mitambo,tunaaminishwa tu kwa kutajiwa imekuwa kwa 5,000%.Ni kama mipasho fulani hivi..

Mkuu..
Nakuunga mkono hawa matapeli Watakuwa wamevimbiwa walipokua wanaandaa hii Taharifa..
Thamani ya mtaji wa kampuni kabla na baada,madeni bila kusahau gharama za manunuzi za Dhamani..
Tuwape muda watakuja na ngonjera nyingine mpya..
 
Kwani yule aliyesema asubuhi alisema chanzo?
kisena na uda yake ni jipu lililoiva. tutakuja juta kwa kwenda dart na uda ya kisena. ukitumbua uda ya kisena utakuta ni mali ya umma imeporwa. uda ya kisena ni hewa tupu (its a bubble). ni madeni umma unategeshewa kubeba. hakuna uwekezaji hapo ila uporaji wa umma.
 
Liabilities zikizidi assets zako.....unafilisika tu, haijalishi thamani ya hizo assets zilizopo. Kama madeni ni trilioni 1 na assets ni bilioni 500....unaweza kuwa mufilisi tu!

Walioshindwa kulipa kodi za TRA ili ku clear mabasi bandarini ni hawa UDA au wengine? Kushindwa kulipa madeni ni dalili ya kuelekea kufilisika.
Hii ni professional ya watu ndugu. Liability zikizidi assets si kufilisika. Halafu kuna equities na pia kwenye financial institutions hiyo ni kawaida.
 
Taarifa haina thamani ya mtaji wa kampuni kabla na baada,madeni wala gharama za manunuzi za mitambo,tunaaminishwa tu kwa kutajiwa imekuwa kwa 5,000%.Ni kama mipasho fulani hivi..

Nami sijaona mtiririko wa ulipaji wa kodi from 2012 to 2015 kama walivyo ahinisha
 
Mkuu..
Nakuunga mkono hawa matapeli Watakuwa wamevimbiwa walipokua wanaandaa hii Taharifa..
Thamani ya mtaji wa kampuni kabla na baada,madeni bila kusahau gharama za manunuzi za Dhamani..
Tuwape muda watakuja na ngonjera nyingine mpya..

Mi naamini hawa hmaa wame baha na kupagawishwa na Pombe JM
 
Wasituchanganye huko na sie tupo serikalini eti tunajua yanayoendelea kimsingi kampuni haikuwi kwa hizo asilimia 5000 huu ni uwongo
 
Back
Top Bottom