Uchunguzi wangu kuhusu kifo

Uchunguzi wangu kuhusu kifo

Nani hufanya uumbaji kama si wazazi?
Anayefanya uumbaji ni muumbaji ila si wazazi, maana hakuna cha kufanya nione kwamba wazazi ndio waumbaji hasa ukizingatia kwa akili ya kawaida ni kwamba lazima binaadamu alitangulia kuumbwa na ndipo kukaanza uzazi na wazazi. Na ndio maana nikasema huu ni muendelezo tu wa uumbaji wa binaadamu.
 
Muumbaji nani?
 
Nimekuwa nikiwaza kwa mda mwingi je inakuaje mtu unakufa, mbona huyu amekufa mapema, mbona huyu kachelewa kufa.

Sometimes unaweza kuona ni kama unakufuru au ninakufuru kumhusu Mungu ila kiukweli najikuta nikiwaza na kumsii Mungu kama nakosea aniepushe na fikra hizi. Ila kuwaza mambo haya sio kukufuru maana nitakuwa na ushahidi fulani hapa.

Mungu ameonyesha kiwango fulani ccja mwanadamu kuishi katika Dunia na alibadili kwa kila baada ya muda.
Kwa sasa tumepewa miaka 70 tu katika maisha ya kawaida, je Mungu ni muongo maana Kuna watu wanazidi hiyo sabini na wengine wanapungua katika hiyo. Sasa angalia nini kinachosababisha kutokana na uchunguzi wangu.

1. Uchunguzi wa kikawaida(normal investigation)
2. Uchunguzi wa kidini(Religion investigations)

Hapa ntatumia uchunguzi wa kawaida hauhusiani na Imani

Kwanza kifo ni Hali ya roho na mwili kutengana, hivyo roho inaondoka au inatoka na kuacha mwili.
Mwili hauwezi kufanya kitu pasipo roho labda kuwe na seli hai zilizobakia kwa mda mchache baada ya roho kutoka(ntaelezea mkitaka).

Sasa twende kwenye Mada kwa nin tunakufa kwa kutofautiana umri.

A. Muda wa kuanza tendo la ndoa baada ya kubalehe au kuvunja ungo
B. Ufanyaji wa mapenzi
C. Shughuli tunazofanya
D. Ulaji
E. Uzembe wa kujilinda
Mkuu umeandaa swali ukijua ni gumu kumbe ndio jepesi saaaana, Sasa sujui huo utafiti wa kidini umefanya ktk dini gani, okay any way kama ungefanya ktk uislamu ungepata majibu mapema tu, ukweli ni hivi binaadamu hutofautiana umri wa kuishi kulingana na ummat (zama), watu walishii miaka 800,600 nk rejea ktk quraan, tukija kwenye swali lako why not now?, jibu zama hizi ni za ummat Muhammad (s.w) hivo yeye ni kiigizo chetu, amefariki akiwa na 63 around , hivo ummat Muhammad umepewa miaka 60s ya kuishi duniani, na ikiwa mtu Kafika zaidi ya 60, yaani 70 , 80, 90, au 100 nk hiyo ni ziada tu yampasa mtu kumshukuru Allah (s.w).
Note: hizo ummat zilipewa umri wa kuishi mrefu wakiongozwa na manabii zao, pili walipewa habari kuhusu ummat utakao ishi umri mfupi (ummat Muhammad) wakashangaa sna na kuliza maswali na wakajibiwa kwa ufasaha . Pia usisahu ummat Muhammad ndio ummat Bora kuliko zote
 
Hapa ntatumia uchunguzi wa kawaida hauhusiani na Imani

Kwanza kifo ni Hali ya roho na mwili kutengana, hivyo roho inaondoka au inatoka na kuacha mwili.
Mwili hauwezi kufanya kitu pasipo roho labda kuwe na seli hai zilizobakia kwa mda mchache baada ya roho kutoka(ntaelezea mkitaka).
Kuanzia hapa tayari si uchunguzi usio wa kiimani sababu bila Imani hakuna kitu kinaitwa roho kama unathibitisha in norma way tuambie kifo ni nini si definition ya roho ukisha kuja hapo tayari umetimia imani

Kiranga
 
Swali la roho ni nini bado halijapata jibu.
 
Kwa nini hamjaweza kujua?

Na kama hamjaweza kujua roho ni nini, mnajuaje kuwa ipo?
Roho inahusishwa na uhai kwa binaadamu kwa maana pasina roho binaadamu hawezi kuwa hai, kwahiyo tendo la uhai na kifo kwa binaadamu inatufanya tujue uwepo wa hiyo roho.
 
Roho inahusishwa na uhai kwa binaadamu kwa maana pasina roho binaadamu hawezi kuwa hai, kwahiyo tendo la uhai na kifo kwa binaadamu inatufanya tujue uwepo wa hiyo roho.
Sijauliza roho inahusishwa na nini, nimeuliza roho ni nini.

Kama ni habari ya kuhusishwa tu, Willy Gamba anahusishwa na majasusi wa Tanzania, katika riwaya za Aristablus Elvis Musiba, lakini hilo halimaanishi Willy Gamba ni jasusi wa Tanzania aliyepo kiuhalisia nje ya hizo riwaya.

Sasa na wewe unahakikishaje roho ipo kweli na si sehemu ya hadithi tu kama Willy Gamba?
 
Back
Top Bottom