Uchunguzi wangu binafsi kuhusu madai ya Tuntemeke & Co

Kikubwa unachofanya kwenye huu uchunguzi wako ni kumsafisha Josephine, ili la walinzi Slaa mwenye pamoja na Josephine, hawakukanusha kwenye majibu yao.

Sasa wewe unakuja kukanusha uoni huko ni kujipendekeza na uchunguzi wako utaoneka porojo?

Katika huo uchunguzi wako Josephine ana kosa lolote?

Ndio uchunguzi lazima umshafishe mtu au upande fulani...bomba inaonekana rahisi kuelewa mkuu
 
Mkuu wangu narudia tena kusema mtu yeyote hawezi kuifanya kazi ya accounting ikiwa hakufundishwa accounting na kuhitimu. Unachodai wewe sio kweli na nakuhakikishia kwa sababu ni profession yangu na nimeifanya kazi hiyo..Mtu anayetumiwa kuingiza data entry za accounting iwe excel au powerpoint hawezi kujua kutumia accounting software bila kuwa na elimu ya uhasibu.

Mkuu sijakuelewa vizuri.
  1. Ambacho sio kweli ni kipi?
  2. Data enrty kwenye power point?
  3. Mtu hawezi kutumia accounting software bila kuwa na elimu ya uhasibu? Elimu gani ya uhasibu mkuu? Najua kuna data entry staff ambao hawana elimu ya uhasibu
 
Hata mimi nashangaa badala ya kujadili issues tunajadili mtu na ndoa yake kaoa, hajaoa, mchumba nafikiri si sehemu yake hapa. Hili la Slaa ana mchumba tulishaliongelea sana, kinachotakiwa kwenye thread hii tujadili hizi tuhuma ni za kweli au za uongo.
Lakini mkuu kama Josephine sio mke wa Dr slaa na anahudumiwa kama mke wa Dr slaa kwa fedha za chama, hapa si ni lazima tuone huo uhalali wa malipo yenyewe?
 
Naona Mkuu Feedback naye amerudi. Karibuni sisi wengine tunajionea tu mambo yanavyoenda humo ndani. Naona watu wameparurana ndani ya chungu.
Tabia yangu huwa sijadili majungu ndiyo maana nilipoona zile thread za Tuntemeke zinaenda too personal nikajitoa, thread inafika page 70 kama hujaelewewa nia ya mleta mada basi wewe hazimo, inafikia watu wanarudia maneno yale yale si afadhali kusoma mada zingine.
 
Kuna mambo kadhaa ambayo nimeyafuatilia katika mada hii utakuta yanaingilia maisha binafsi ya mtu badala ya kujadili mambo yanayohusu chama. Dr Slaa kuwa na mchumba muda mrefu bila kufunga ndoa ni jambo la binafsi na pengine linahusiana na dhamiri ya mtu inavyomtuma kwa vile ana daraja takatifu ambayo alishakula kiapo, holy See ilichofanya ni kumruhusu kuacha shughuli na huduma ya Sakrament ya daraja Takatifu lakini hiyo Sakrament inabaki hadi kifo chake, hivyo kwa yeye mwanasheria anajua hilo na tusishangae kwa nini hafungi ndoa, ni jambo binafsi kadiri ya uelewa wangu mdogo wa Canon Law na maisha binafsi ya mhusika na dhamiri yake. Hata hivyo hilo halimpi pingamizi ya kufunga ndoa kwa vile ni dhamiri binafsi ingawa Holy See imeshampa green light.

Mimi ni mmojawapo niliyelalamika mara kadhaa kuhusu kitengo cha propaganda chamani kuwa hakuna hata dalili kama kuna mtu, leo ndio nagundua kama kulikuwa na mtu. Kwa vyo vyote Chama kimefanya vyema kumpumzisha na kumweka mwingine ili afanye kile ambacho watu tunatazamia. Hata msukumo wa kuwa na vyombo vya habari vinavyojitegemea kwa ajili ya Chadema mhusika katika idara hiyo alitakiwa kufanyia kazi. Kama ameshindwa sasa nini kifanyike kama si kupumzishwa ili kumpisha atakayeweza?

Kuhusu suala nyeti la uhasibu tukumbuke chama bado kilikuwa kichanga, na sasa kimekua kufikia hadhi ya kuwa chama kikuu cha upinzani. Hapo awali watu walifanya kazi kwa kujitolea, na kumwajiri certified accountant ni gharama, wengi walikuwa wanafanya kwa kujitolea. Kama Mwigamba amekuwa na kazi nyingi mno na sidhani kama anajisikia kama amenyang'anywa kazi wakati anayo kubwa zaidi ya kuwa Mwenyekiti wa Mkoa.

Pendekezo langu: Kutenganisha kazi za kiofisi na siasa katika Chama cha siasa ni muhimu, na siasa tu ila pia katika vitengo vingine katika serikali na vyama vingine vya siasa. Naleta mfano wa Jeshi la polisi nchini Marekani. Ofisi za jeshi la polisi wameajiriwa watu wa kawaida ambao hata mguu pande mguu sawa hawajui. Wameajiriwa kadiri ya taaluma yao ya kufanya kazi za kiofisi katika nyanja zote. Polisi hufanya kazi zake za kipolisi tu na hapo unaona mpangilio na mafanikio ya kazi zao zilivyo.

Vyama vya siasa viache kupeana majukumu na kazi kwa misingi ya takrima, bali ifuate uwezo na taaluma ili kujengwa utendaji bora. Ni aibu chama Chadema wakati ule wa kashfa za mishahara baada ya kulipuliwa na Nape ni kwa sababu ya kutokuwa na certified accountant vinginevyo wangekuwa naye angehakikisha anafuata taratibu za sheria za malipo .

Kilichofanyika kuondoa viongozi na watendaji ambao walizorotesha ama kwa kutokuwa na uwezo wa utendaji na wengine kwa kuzidiwa na majukumu mengi kama Mwigamba ni sahihi, na wenye mapenzi mema wataelewa hilo.
 
Mkuu unataka kuleta mambo ya Sioi wewe ha haaa........
Ili mwanamke aweze kuwa mkeo kwa kukaa nae kwa kuishi naye huo muda ulio usema kunahitaji awe na sifa fulani mkuu, si kila mwanamke...
Vipi akiwa mawanafunzi wa miaka 25
vipi akiwa ni binti wa miaka 17
Vipi akiwa hana akili timamu
Vipi ikiwa umemlazimisha bla ya ridhaa yake
Ongeza sasa na vipi akiwa tayari ni mke wa mtu mwenye ndoa halali ambayo haijafunjwa? nk nk nk
Nadhani jibu utakuwa nalo tayari

Mkuu Paulss,
Labda tumpe mfano moja Kimbunga, amchukuwe mke wake akae nae miezi 8 huyo mke anakuwa wa Kimbunga?
 
Mkuu nadhani kwako wewe Tunte,Tii na Paa ni watu watau tofauti. Kama kweli unaamini hivyo utakuwa umekosea sana

nilimaanisha connection ya mwigamba na tumbo na huyu tunte/tii/paa/mwanahalis. Huwezi kumuhukumu mwigamba na tumbo wakati hakuna supporting evidence ya uhusika wao zaidi ya kuwa na hisia. Kama mpo serious mtafuteni tunte/tii/paa/mwanahalis watoe maelezo sahihi on face to face conversation hakuna linaloshindikana ktk ulimwengu huu wa technology

huwezi kumuhukumu known person kwa kushirikiana na mtu mwingine asiyejulikana na tena anayetumia fake IDs. Sasa hapa kama Tunte si mwanachadema hamuoni kwamba mission yake imefanikiwa kuwavuruga cdm? na mbaya zaidi mnazidi kuibomoa cdm kwa kuanika vyupi vyenu barabarani that is mnazidi kuanika maeneo yenu ambayo adui yenu alikuwa hayajui (tumieni akili cdm). Ni mtaji tosha sana kwa adui on where to start

what if ikaja kugundulika kuwa mwigamba na tumbo hawahusiki na lolote? mtaficha sura zenu wapi? muwatendee haki wengine wasio na meno
 
Mkuu wangu kufanya installation ya Accounting software kwenye mifumo ya uhasibu wa chama kikubwa kama CDM unaona ni issue ndogo?

Halafu mkuu nikiweka kwenye pc yangu private au gari langu private likiharibika unaweza kulinganisha na Taasisi?

Yaani leo Mbowe ampe mkewe tenda ya kusafisha ofisi, kesho mnyika ampe tenda mdogo wake ya kutengeneza magari ya ofisi, Saidi Arfi ampe mkewe ya kuleta stationaries, Tundulisu ampe mkewe tenda ya......... the list goes on
Taasisi haiendeshwi hivyo mkuu

Software is one of the most expensive activities kuliko unavyodhania na nakuhakikishia Josephine hajatengeneza software ametengeneza data base pengine kutumia excel or whatever......

Vyovyote utakavyo chukulia gari la shirika likihharibika anatafutwa fundi ambaye anakubalika na viongozi sio lazima tender ila una shop around mwenyewe..Na wala usifikirie kuitafuta software na kuiweka ni jambo kubwa saana kama mnavyolikuza kinachotazamwa ni uzuri wa software yenyewe na matumizi yake - tosha kabisa mimi nimetumia ACCPAC na Quick Book zote nime install mimi mwenyewe kwa shirika kunipa wajibu wa kutafuta software hizo maadam nilikuwa na baraka za viongozi wangu how much they can spend.. hakuna kitu tender wakati ni kitu cha mara moja na kinafanyiwa ukarabati kama unavyotumia Microsoft Window 7 au XP.. huhitaji kuweka tender isipokuwa unataka kutumia software gani unakwenda dukani na kununua. Hivi kweli kama system ya kazini (computer)ina break kwa virusi kwa sababu haina Anti virus, utaweka tender wapi?..
 
Mkuu Nas Das, kwamba hoja zipo open mimi sikatai. Ni kweli zipo Open lakini za Uongo usiomithilika.
Huyo Dr. Slaa mnaemsema ameiba hela za Chama ili ajenge nyumba yake ndiye huyu aliyehamia kwenye nyumba yake bila hata ya kuwa na umeme? Ndiye huyu aliyehamia kwenye nyumba yake hata kabla haijaisha? Ndiye huyu anayehaha hivi sasa kutafuta fedha za kumalizia nyumba yake?
Na kama ni suala la kutoa ushahidi, si mtoa kashfa anatakiwa kutoa ushahidi wa madai yake? Iweje leo tumsumbue Dk.Slaa kuleta nyaraka? Hivi leo nikisema Mwenyekiti wa CCM ni malaya ana watoto kila kona, na mwenyekiti akaita media kukanusha wa kuleta ushahidi ni mwenyekiti wa CCM au mimi niliyetoa tuhuma ndiye wa kuleta ushahidi kama ni birth certificates au picha za hao watoto?. Just be fair to Dr.Slaa

Mkuu Rev., labda suala hili tuliweke hivi:
Ni kweli, mtoa tuhuma ndie anayetakiwa kutoa ushahidi ya tuhuma anazozitoa! Lakini katika hili, ni kinyume chake...tusikariri!! Hii ni vita kati ya Jeshi la Linaloonekana na lile lisiloonmekana! Na ndio maana hapa tumeishia kumtaja TUNTEMEKE ndie huyo huyo TII, MWANAHALIS, Paa n.k! Wengine wakaenda mbali na kusema hao ni akina sijui Komu, mara Mwigamba, mara Tumbo na mambo kadha wa kadhaa! Kilichopo ni clue....no one is sure na hata kama mtu ana uhakika bado hawezi kuthibitisha unless Mods wavunje maadili ya kazi yao kwa ku-disclose identity ya wahusika! Na hata hao Mods wakiamua ku-dislose identity bado hapana uhakika wa 100% coz' sio lazima member aandike jina lake la kweli...!

Lakini, pamoja na contradiction hiyo, bado hakuna shaka yoyote kwamba anayetuhumiwa ni Dr Slaa na Mwandani wake!! Hivyo basi, vyovyote iwavyo ni Dr Slaa ndie aliye kwenye disadvantaged angle na wala msidhanie kwamba madai ya kuwataka akina TUNTEMEKE (Sanga, au?) ndio wathibitishe ni hoja ya kumtolea tuhuma Dr Slaa! Tuseme leo hii Dr Slaa anaenda mahakamani kushitaki kuchafuliwa image yake! Ni nani atakayeenda kumshitaki? TUNTEMEKE? Who's dat? TII? and wht's TII?

Sina hakika kama nimesomeka!

Kama nimesomeka, ndio maana nasisitiza kwamba ni Dr Slaa ndie anayetakiwa kutoa ushahidi ili kujisafisha! Hiyo mifano mnayoitoa ya kuonesha kwamba ni mtoa tuhuma ndie anaetakiwa kutoa ushahidi ni irrelevant and can never work kwenye hii issue!! Msisahau, madai yenu ni kwamba waleta hoja wana lengo la kumchafua Dr Slaa! Kama hivyo ndivyo, ni Dr Slaa ndie anayetakiwa kujisafisha.....!! Think about it!!
 
Tabia yangu huwa sijadili majungu ndiyo maana nilipoona zile thread za Tuntemeke zinaenda too personal nikajitoa, thread inafika page 70 kama hujaelewewa nia ya mleta mada basi wewe hazimo, inafikia watu wanarudia maneno yale yale si afadhali kusoma mada zingine.

Mkuu lakini jamaa wamewatoa mbio watu wengi!
 
Tabia yangu huwa sijadili majungu ndiyo maana nilipoona zile thread za Tuntemeke zinaenda too personal nikajitoa, thread inafika page 70 kama hujaelewewa nia ya mleta mada basi wewe hazimo, inafikia watu wanarudia maneno yale yale si afadhali kusoma mada zingine.

Mkuu taratibu basi, na yale maneno uliyokuwa unamjadili Sioyi mara umuite Mungiki, unajadili sikio lake Sioyi, wewe sema ile thread ya TUNTEMEKE ilikuwa mkuki.
 
Vyovyote utakavyo chukulia gari la shirika likihharibika anatafutwa fundi ambaye anakubalika na viongozi sio lazima tender ila una shop around mwenyewe..Na wala usifikirie kuitafuta software na kuiweka ni jambo kubwa saana kama mnavyolikuza kinachotazamwa ni uzuri wa software yenyewe na matumizi yake - tosha kabisa mimi nimetumia ACCPAC na Quick Book zote nime install mimi mwenyewe kwa shirika kunipa wajibu wa kutafuta software hizo maadam nilikuwa na baraka za viongozi wangu how much they can spend.. hakuna kitu tender wakati ni kitu cha mara moja na kinafanyiwa ukarabati kama unavyotumia Microsoft Window 7 au XP.. huhitaji kuweka tender isipokuwa unataka kutumia software gani unakwenda dukani na kununua.

Hukutumia pesa za walipa kodi wewe. Fanya hivyo kwa pesa za walipakodi uone!
 
nilimaanisha connection ya mwigamba na tumbo na huyu tunte/tii/paa/mwanahalis. Huwezi kumuhukumu mwigamba na tumbo wakati hakuna supporting evidence ya uhusika wao zaidi ya kuwa na hisia. Kama mpo serious mtafuteni tunte/tii/paa/mwanahalis watoe maelezo sahihi on face to face conversation hakuna linaloshindikana ktk ulimwengu huu wa technology

huwezi kumuhukumu known person kwa kushirikiana na mtu mwingine asiyejulikana na tena anayetumia fake IDs. Sasa hapa kama Tunte si mwanachadema hamuoni kwamba mission yake imefanikiwa kuwavuruga cdm? na mbaya zaidi mnazidi kuibomoa cdm kwa kuanika vyupi vyenu barabarani that is mnazidi kuanika maeneo yenu ambayo adui yenu alikuwa hayajui (tumieni akili cdm). Ni mtaji tosha sana kwa adui on where to start

what if ikaja kugundulika kuwa mwigamba na tumbo hawahusiki na lolote? mtaficha sura zenu wapi? muwatendee haki wengine wasio na meno
Mkuu unalazimisha sana eti what if ikijulikana sio Mwigamba na Tumbo! Waje hapa wakanushe waone nitakavyowaumbua. Huyo Tumbo kwa wiki nzima amekaa na mafile ya payment vouchers na anakagua Vocha za Slaa tu yeye kama nani? Aje hapa abishe kuwa hayuko nyuma ya hii move
 
Mkuu karibu manake naona vijana walikukimbiza humu hadi ukaamua kumwachia Mungu na kufunga! Naona Rev. amekupa faraja. Sijui kama yameisha haya manake muda sijawaona akina Tuntemeke, PAA, TII na Mwanahalis. Hawa jamaa kama ni vitani basi wanashambulia makazi ya Raia na target yao huwa very perfect. Nakumbuka kuna siku alikuja Dr. Mkumbo akajibu hapa lakini akapewa stahili yake hajarudu hadi leo. Akaja Makene akajitutumua naye akapata stahili yake toka kwa vijana naye akapotea hadi leo. Ukabaki wewe siku ile ukajitutumua lakini akaja Tuntemeke kijukuu cha Mwakipande akaupa haki yako hujarudi hadi leo ndio nakuona(labda uko busy na uchaguzi). Juzi tumekuwa na Dr. Slaa na Josephine nao wakajibujibu hapa lakini wakapewa haki zao nao wametokomea! Angalia wasije wakarudi kwa kasi mpya wakakupa stahili yako wewe pamoja na Rev. Mkombozi wako.

Naona Mkuu Feedback naye amerudi. Karibuni sisi wengine tunajionea tu mambo yanavyoenda humo ndani. Naona watu wameparurana ndani ya chungu.

Mkuu wangu Kimbunga.Mimi huwa napenda sana challenges za ukweli, huwa siogopi nikiambiwa ukweli.Lakini haipendezi watu wazima kuamua kushadadia uongo wa mchana kweupe eti kumchafua mtu kisa tu umeondolewa kwenye nafasi yako.Hii ni laana mbaya sana na nakuapia itawatafuna mpaka iwamalize Tuntemeke & Co.
 
Vyovyote utakavyo chukulia gari la shirika likihharibika anatafutwa fundi ambaye anakubalika na viongozi sio lazima tender ila una shop around mwenyewe..Na wala usifikirie kuitafuta software na kuiweka ni jambo kubwa saana kama mnavyolikuza kinachotazamwa ni uzuri wa software yenyewe na matumizi yake - tosha kabisa mimi nimetumia ACCPAC na Quick Book zote nime install mimi mwenyewe kwa shirika kunipa wajibu wa kutafuta software hizo maadam nilikuwa na baraka za viongozi wangu how much they can spend.. hakuna kitu tender wakati ni kitu cha mara moja na kinafanyiwa ukarabati kama unavyotumia Microsoft Window 7 au XP.. huhitaji kuweka tender isipokuwa unataka kutumia software gani unakwenda dukani na kununua. Hivi kweli kama system ya kazini (computer)ina break kwa virusi kwa sababu haina Anti virus, utaweka tender wapi?..

Mkuu ulinunua kama Mhasibu na ku install ama ulinunua kama IT specialist na ku install?
 
Mkuu unalazimisha sana eti what if ikijulikana sio Mwigamba na Tumbo! Waje hapa wakanushe waone nitakavyowaumbua. Huyo Tumbo kwa wiki nzima amekaa na mafile ya payment vouchers na anakagua Vocha za Slaa tu yeye kama nani? Aje hapa abishe kuwa hayuko nyuma ya hii move

Mkuu wangu nitamlilia Mungu wangu akupe maisha marefu
 
Lakini mkuu kama Josephine sio mke wa Dr slaa na anahudumiwa kama mke wa Dr slaa kwa fedha za chama, hapa si ni lazima tuone huo uhalali wa malipo yenyewe?
Mzee hili la mke si mke si umeliongelea sana kwenye ile thread ya Tuntemeke. Hapa ongelea uhalali wa malipo ya package na kama alistahili kulipwa na si ndoa yao, kama ni suala la ndoa ya mke wa Slaa (firstlady) fungua thread yake tuanze kufunguka maana kuna wengine huwa wanatumia ndege ya rais kwenda kwenye birthday party lakini hayo yote hapa si sehemu yake.
 
Back
Top Bottom