Uchunguzi wangu binafsi kuhusu madai ya Tuntemeke & Co

Mzito K,
Yaani miaka yote hii chama kilichosheheni wasomi hakina Accounting package inayoeleweka? Kuhusu huyo Tumbo, siku zote nimekuwa natahadharisha juu ya hawa wapima upepo wanaokimbilia kwenye vyama baada ya kushamiri kwa vyama hivyo, na sio wao wenyewe kushiriki kuvijenga vyama hivyo. CDM wapo wengi sana. Anton Komu, Joseph Selasini, Msafiri Mtemelwa nk. Watu aina hii ni hatari sana, nashangaa wanapokkuja na nyie kukimbilia kuwatunuku mavyeo. Hivi huyu aliyepumzishwa uhasibu, kama amesomea mbona nafasi ni nyingi tu, aliambiwa uhasibu wake lazima aufanyie CDM?

Umeandika waraka mrefu ambao kwa sehemu kubwa bado haujajibu tuhuma zilizoletwa. Sehemu kubwa ya waraka wako umejaribu kuwapambanua wale walioleta tuhuma hizo ni kina nani. Nadhani si muhimu kwetu kujua mleta tuhuma ni nani! Ili iweje, thibitisha hapa kuwa, tuhuma hizo si za kweli ili upingane na Dr Slaa mwenyewe ambaye ki msingi amekubali. Nilitegemea jambo moja kubwa baada ya Tuntemenke kushusha scud zile, nilitegemea wana CDM makini kuanza uchunguzi wa kutafuta ukweli kuhusu tuhuma hizo ili wasafishe chama, badala yake nao wanawashutumu waliosaidia kufukua maovu. Nikuulize swali dogo. Ikitokea tuhuma hizo zikathibitishwa kuwa ni za kweli, mtaweka wapi sura zenu?
 
Mkuu Maranya, baada ya kusoma uzi nimegundua kwamba kwa upande wa Mwigamba kuna elements za kuonewa. Hivi unaleta accounting package ambayo naamini imekuwa developed na siyo kuchukuliwa kutoka dukani (on the shelf) halafu unasema ameshindwa kuitumia; je alikuwa trained, alishirikishwa katika mchakato wa kui develop? Hii package inaonekana kama imekuwa imposed kwa akina Mwigamba bila kufuata utaratibu wa System Development Life Cycle. Siku zote system ambazo hazikufuata utaratibu huwa zina failkwa kuwa hukosa User Acceptance. Pia mkuu umeseme Mwigamba ni fundi mchundo; imekuwa tena aingilie mambo ya IFRS 9 au ni Mhasibu pia kwa maana ya Certified Public Accountant? Kama si mhasibu na mkampa uhasibu basi mlimuonea tangia mwanzo na hapa ni maendelezo tu ya kumuonea.

Kimbunga,
Kwa taarifa nilizonazo ni kwamba Samsoni Mwigamba ni multi professional. Baada ya FTC alisoma B. Com University of Dar es salaam!
 
Naanza kuunganisha moja na moja na kupata mbili: teh teh teh.

Imeandikwa humu kwamba Komu ndiye mmiliki wa Gazeti Pendwa la Mwanahalisi, ikasemwa pia kwamba huenda Gazeti la Mwanahalisi likaanza kuanika maovu ya Dr. Slaaa kabla sijatafakari akaja mtu mwenye ID ya Mwanahalis akatoa vipande tosha dhidi ya Dr. Slaa. Nikasoma baadaye kwamba Komu naye kafutwa kazi ya kushika fuko la hela huko CDM!! Basi nasubiri kumsindikiza Dr. Golgota. Nasubiri sasa Gazeti la Mwanahalisi ili likemeee ufisadi ndani ya CDM kama lilivyokemea ufisadi ndani ya Serikali ya CCM.

Kuanzia juzi usiku hadi leo tu, tayari imeniwezesha kuifahamu CHADEMA tofauti na nilivyokuwa nimeifahamu kwa miaka kadhaa iliyopita!
 

paulss, plz nd plz; usije na wewe ukaishia kusema kwamba Mkandara na Josephine ndie huyo huyo (one and the same) ila tu anatumia multiple ID!
Ha haaaa........ mkuu au ndio unani alert nini
Ngoja nifanye kauchunguzi lol,
But i dont think so

 
Nakubaliana na wewe kwamba CHADEMA will be better off kwa kumuweka kando Josephine. Aliyokwishafanyia chama ashukuriwe then watu wosenge mbele. Uwepo wake sasa unaanza kuwa source of un-neccessary debate. Ni ushauri tu CHADEMA.

Lakini hapo kwenye red: Mbele ya sheria Dr Slaa sio single. Ukishakaa na mwanamke kwa zaidi ya miezi sita basi anahesabika kama mke. Hivyo kama 'mama mdogo' yuko kwakO tangia mwezi August 2011 basi ndugu una mke! Tarumbeta na ubwabwa ni juu yako lakini mke tayari unaye ndani!


Mkuu lakini huko makazini waajiri huhitaji cheti cha ndoa aidha cha kanisa/msikiti ama cha serikali. Kwenye stahili kazini hawara ama mtu unayeishi naye kinyumba huwa hatambuliki! Ndoa za kimila pia huwa hazitambuliki makazini Mkuu japokuwa kwa sheria ya ndoa ya mwaka 1971 hizo ni ndoa. Kazini pia tunatambua mke mmoja japokuwa kisheria kwa wenzetu waislamu wanaweza kuwa na wanawake wanne at a time.
 

Lakini kiongozi mbona hoja za TUNTEMEKE zipo open kabisa?! Sawa, anadhalilisha uongozi wa juu wa chama...na hoja zake za msingi ni kwamba mambo mengi aliyoyafanya Dr Slaa hayakupata baraka za chama! Sasa kuna taabu gani hapo kwa Dr Slaa kuonesha kwa vielelezo kwamba aliyoyafanya yalipata baraka za chama?! Kwani vikao vyenu havina minutes?! Unataka kuniambia viongozi wanakutana tu na kukubaliana kwa mdomo?! Ikiwa hata SACCOS za uswahilini zina minutes za meetings zao, ije kuwa CHADEMA?! Sasa kama kweli TUNTEMEKE anafanya makusudi ili kumchafua Dr Slaa, kkwanini Dr asijisafishe kwa kutoa nyaraka?! Juzi, Josephine alitoka hapa jamvini kwa mbwembwe kwamba anaenda kuleta vielelezo, mbona hadi sasa hajatokea?! Shelves za documents zenu zinapatikana wapi? Ili mradi ushahidi unaotakiwa si mkubwa sana zaidi ya muhtasari ya vikao, basi kadri watakapochelewa kutoa vielelezo hivyo ndivyo uhalali wake utakapokuwa na shaka!! KWANINI? Kwa kawaida, minutes za vikao huwa zinafailiwa sehemu maalumu na pale zinapohitajika ni rahisi tu kuzipata! Hivyo, kuchelewa kutoa vielelezo hivyo wakati Josephine alidai anaenda kuleta ushahidi, napata shaka kwamba kuna documents zinapikwa!
Mkuu Nas Das, kwamba hoja zipo open mimi sikatai. Ni kweli zipo Open lakini za Uongo usiomithilika.
Huyo Dr. Slaa mnaemsema ameiba hela za Chama ili ajenge nyumba yake ndiye huyu aliyehamia kwenye nyumba yake bila hata ya kuwa na umeme? Ndiye huyu aliyehamia kwenye nyumba yake hata kabla haijaisha? Ndiye huyu anayehaha hivi sasa kutafuta fedha za kumalizia nyumba yake?
Na kama ni suala la kutoa ushahidi, si mtoa kashfa anatakiwa kutoa ushahidi wa madai yake? Iweje leo tumsumbue Dk.Slaa kuleta nyaraka? Hivi leo nikisema Mwenyekiti wa CCM ni malaya ana watoto kila kona, na mwenyekiti akaita media kukanusha wa kuleta ushahidi ni mwenyekiti wa CCM au mimi niliyetoa tuhuma ndiye wa kuleta ushahidi kama ni birth certificates au picha za hao watoto?. Just be fair to Dr.Slaa
 
Mkuu kwenye blue nashukuru kama unatambua hilo
Lakini kwenye Red sikibaliani na wewe kwa asilimia mia moja.
Kisheria Josephine ni mke wa somebody Mushumbuzi na wana ndoa halali ambayo haija vunjwa, na ndio maana kama sikosei mwezi wa kwanza Josephine amafungua shauri mahakamani kutaka ndoa yake na Mushumbuzi ivunjwe rasmi na mahakama

Nimekusoma. Kwenye red, kama ndivyo basi Josephine anakuwa ameolewa na watu wanaume wawili kwa wakati mmoja hivyo ngoma inaangukia kwake na sio Dr Slaa. Sasa swali linakuja, je sheria ya ndoa Tanzania inatambua mwanamke kuolewa na wanaume wawili kwa wakati mmoja? I believe jibu ni hapana, so, she has sort out the mess! Kwa wanaume hii inakubalika maana kuna ndoa za kimila na pia kwa upande wa uislama mume anaruhusiwa kuwa na zaidi ya mke mmoja.
 
Kimbunga,
Kwa taarifa nilizonazo ni kwamba Samsoni Mwigamba ni multi professional. Baada ya FTC alisoma B. Com University of Dar es salaam!

Kusoma B.Com bila kuwa na CPA ama equivalebt hakumfanyi mtu kuwa mhasibu wa kushika mapesa yote hayo. Sijui NBAA wako wapi manake kila mtu anajiita mhasibu ili hali si mhasibu bali Accounting Technician!
 
Kimbunga,
Kwa taarifa nilizonazo ni kwamba Samsoni Mwigamba ni multi professional. Baada ya FTC alisoma B. Com University of Dar es salaam!

Huyu si ndiye ana kesi ya uchochezi mahakamani. Sasa mnamfuta kazi atapata wapi pesa za kuendeshea kesi?
 
Ndio nimesema hawezi hata akifundishwa kwa sababu Uhasibu ni taaluma unayosemea kwa miaka kibao. Uhasibu sio kujaza data bali kuelewa vitu vingi vinavyohusika.. Huwezi kunambia msomi aliyekuwa akifunga vidonda vitani, akifundishwa kusoma MRI basi anaweza kuifanya kazi ya Udaktari.. sii kweli.

Na labda, awe Mweka Hazina badala ya Mhasibu!
 
Kimbunga,
Kwa taarifa nilizonazo ni kwamba Samsoni Mwigamba ni multi professional. Baada ya FTC alisoma B. Com University of Dar es salaam!
sikukujibu mara ya kwanza uliposema Mwigamba ni mtaalam wa telecom, nilijua utakwama mahali. Nashukuru umeonyesha hekima yako kwa kuwa mkweli.
Kilichopo ni kuwa Mwigamba alikuwa na utaratibu wa kuleta ripoti zilizokuwa zimekaa kiubabaishaji na zilikuwa zinachelewa kutoka. Accounting package iliyoletwa na Josephine iliziba mianya ya wao kufanya ubabaishaji wao. Baada ya yeye kugundua hilo akaikataa kwa kujitetea kuwa ile ni database tu. Alipoambiwa ataje tofauti ya database na accounting package ndio ukawa mtihani. Nadhani umeelewa sasa
 

Kuanzia juzi usiku hadi leo tu, tayari imeniwezesha kuifahamu CHADEMA tofauti na nilivyokuwa nimeifahamu kwa miaka kadhaa iliyopita!
Bila shaka mkuu wangu wlaa hujakosea. Chadema ni chama kichanga sana wanaokoteza watu huku na huko na kibaya zaidi hakuna sifa nzuri ya Mdanganyika kama ujnafiki yaani unachukua huku na kuyapeleka kule. Huu mchezo umekuwepo kwa muda mrefu sana na mimi huwasoma tu watu wanavyogeuka mara wakipewa wadhifa ama kuondolewa.

Huwezi kuyakuta haya CCM kwa sababu wanapikwa kwanza na huwezi kuingia CCM kabla hujapitia mtihani mkubwa wa kimaadili hata iwe upande gani. Kinachotokea Chadema leo ni zile zile hadithi za mtu mweusi - KUIGA, yaani siu zote tunayafanya mabadiliko kwa kuiga mtu mwingine kwa sababu vichwa vyetu viomechoka kubuni isipokuwa kutazama tuige wapi?. Ndio maana nawasifu sana watu kama Hamad Rashid wanazungumza vitu wakiwa madarakani bila unafiki na vinaonekana wazi..
 
Ndipo wazo (ambaloLILIPINGWA VIKALI) la kutafuta accounting package lilipopatikana na Bi Jsephine kuombwa kusaidia upatikanaji wa Package hiyo. Ikumbukwe kuwa Bi Josephine nimtu anayeendesha ofisi yake binafsi na yenye wafanyakazi kadhaa. Mbali nakufanya shughuli zingine kwenye ofisi yake, Bi Josephine ni mtaalamu aliyebobeakatika mambo ya programming na system analyst mzuri. Shahada yake ya kwanza yaChuo kikuu alisomea mabo hayo. Kwahiyo kwake yeye ishu hii haikumuumiza kichwa,alifanya kama alivyoombwa.

Kwa upande mwingine, hapo panaweza kuwa na tatizo. Pamoja na kuwa ni mtaalamu kwenye hayo mambo, pamoja na kwamba alikuwa ana volunteer, bado mlitakiwa kufikiria out of the box and probably a step further. Haya mambo ndio huwa yanaleta migongano baadae ndani ya organisation/institution.

Kama mngefuata taratibu za kawaida za kutafuta hiyo package kama kutangaza tenda, n.k kuna uwezekano mkubwa haya yasingetokea. Inawezekana kwa kumtumia huyo mama mlikuwa mnajaribu ku-save costs na pia kutumia ujuzi wake for free, lakini ni muhimu kujua kuwa vitu au services za bure zinakuja na gharama zake pia.

Naamini Chadema ni chama makini kama kinavyojiita. Sometimes, for the avoidance of any problem/conflict in future vitu kama hivi inabidi vifanyike kwa kufuata taratibu. Sidhani kama itakuwa ni utaratibu mzuri kama Chadema ikiingia madarakani, na Dr Slaa akawa Rais basi package za accounting system za Ikulu ziwe zinafanywa na huyu mama kwa sababu ni mjuzi na atafanya for free.

Wanachadema mtaniponda but I am just providing a constructive criticism.
 
Mkuu lakini huko makazini waajiri huhitaji cheti cha ndoa aidha cha kanisa/msikiti ama cha serikali. Kwenye stahili kazini hawara ama mtu unayeishi naye kinyumba huwa hatambuliki! Ndoa za kimila pia huwa hazitambuliki makazini Mkuu japokuwa kwa sheria ya ndoa ya mwaka 1971 hizo ni ndoa. Kazini pia tunatambua mke mmoja japokuwa kisheria kwa wenzetu waislamu wanaweza kuwa na wanawake wanne at a time.

Mkuu Kimbunga, jibu liko hapo kwenye red: Sheria haikutungwa kwa ofisi moja moja, ni sheria kwa watu wote wenye ofisi na wasio na ofisi.
 
Nimekusoma. Kwenye red, Joseph anakuwa ameolewa na watu wanaume wawili kwa wakati mmoja hivyo ngoma inaangukia kwake na sio Dr Slaa. Sasa swali linakuja, je sheria ya ndoa Tanzania inatambua mwanamke kuolewa na wanaume wawili kwa wakati mmoja? I believe jibu ni hapana, so, she has sort out the mess! Kwa wanaume hii inakubalika maana kuna ndoa za kimila na pia kwa upande wa uislama mume anaruhusiwa kuwa na zaidi ya mke mmoja.


Mkuu kisheria suala la Josephine liko mahakamani na mahakama itaamua.

Kwa imani ya KIKRISTO ni kwamba Josephine si mke wa Dr. Slaa bali ni Mke wa somebody Mahimbo. Ref. 2 Wakorintho 2,3. Kwa kuwa Josephine ni Mkristo basi hawezi kujinasibu kwamba ni mke wa Dr. Slaa.
 
Nimekusoma. Kwenye red, Joseph anakuwa ameolewa na watu wanaume wawili kwa wakati mmoja hivyo ngoma inaangukia kwake na sio Dr Slaa. Sasa swali linakuja, je sheria ya ndoa Tanzania inatambua mwanamke kuolewa na wanaume wawili kwa wakati mmoja? I believe jibu ni hapana, so, she has sort out the mess! Kwa wanaume hii inakubalika maana kuna ndoa za kimila na pia kwa upande wa uislama mume anaruhusiwa kuwa na zaidi ya mke mmoja.
Mkuu unataka kuleta mambo ya Sioi wewe ha haaa........
Ili mwanamke aweze kuwa mkeo kwa kukaa nae kwa kuishi naye huo muda ulio usema kunahitaji awe na sifa fulani mkuu, si kila mwanamke...
Vipi akiwa mawanafunzi wa miaka 25
vipi akiwa ni binti wa miaka 17
Vipi akiwa hana akili timamu
Vipi ikiwa umemlazimisha bla ya ridhaa yake
Ongeza sasa na vipi akiwa tayari ni mke wa mtu mwenye ndoa halali ambayo haijafunjwa? nk nk nk
Nadhani jibu utakuwa nalo tayari
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Mkuu Kimbunga, jibu liko hapo kwenye red: Sheria haikutungwa kwa ofisi moja moja, ni sheria kwa watu wote wenye ofisi na wasio na ofisi.

Tatizo ni sheria ya kazi mkuu. Bila cheti cha ndoa spouse hatambuliki!
 
uongozi unahitaji hekima na busara za kipekee,unapoona mtu anakuwa mbogo anapotolewa ktk nafasi fulani ya uongozi hasa nafasi kama za vyama ujue huyo ni mzigo,kuna watu kwa uwepo wao husababisha mambo yasiende.nashauri watu wachache wasiwe sehem ya kuvuruga chama chetu na kwa tabia waliyoionesha ni udhaifu mkubwa kiuongozi,waachie nafasi kwa hekima wasilete mambo ya kitoto.vema waoneshe kukua kisiasa,kimaadili na kifikra.wanacdm tujikite ktk kufuatilia ukweli na mara nyingi binafsi nionapo baada ya mtu kuenguliwa ktk nafasi fulani halafu yanazuka mambo nikibaini yanatokana na muenguliwa mara nyingi hupuuza,maana unapokuwa mkweli kwanin usubiri kuenguliwa??hawa ni mzigo ktk chama na ikibidi waondolewe hata makao makuu kwa utovu wa nidham.
 
Back
Top Bottom