Uchunguzi wangu binafsi kuhusu madai ya Tuntemeke & Co

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,857
7,615
Hivi karibuni kulifanyika mabadiliko ndani ya Chadema, mabadiliko yaliyoishia kumwondoa Bwana Erasto Tumbo katika nafasi yake ya ukurugenzi wa Habari. Nafasi hii ni nyetisana. Lakini pia Bwana Mwigamba na yeye aliishia kuondolewa katika nafasi yakeya Uhasibu wa Chama.

Wote kwa pamoja wameonekana kutomsaidia vyema Katibu mkuu katika nafasi zao walizopewa na kama ilivyotarajiwa watu hawa wakapandwa najaziba na hasira kali dhidi ya uamuzi huu na pamoja na kuwa uamuzi huu ulikuwa umetolewa kupitia vikao halali, waheshimiwa hawa waliamini kuwa Dr. Slaa ndiyeadui wao na aliyewachomea utambi.

Nianze na Mwigamba.Huyu Bwana amedaiwa kuwa mcheleweshaji mkubwa sana wa ripoti za fedha za chama. Na kila ambapo ripoti hizo zikihitajika, hasa pale ambapo Dr. Slaa akitakiwakuzitolea maelezo/ufafanuzi au kuziwasilisha kwenye vikao halali kwa mujibu wakanuni na taratibu za chama ripoti huja kwa kuchelewa lakini zikiwa nachangamoto kadhaa na wakati mwingine kasoro. Ndipo wazo (ambaloLILIPINGWA VIKALI) la kutafuta accounting package lilipopatikana na Bi Josephine kuombwa kusaidia upatikanaji wa Package hiyo. Ikumbukwe kuwa Bi Josephine nimtu anayeendesha ofisi yake binafsi na yenye wafanyakazi kadhaa. Mbali nakufanya shughuli zingine kwenye ofisi yake, Bi Josephine ni mtaalamu aliyebobeakatika mambo ya programming na system analyst mzuri. Shahada yake ya kwanza yaChuo kikuu alisomea mabo hayo. Kwahiyo kwake yeye ishu hii haikumuumiza kichwa,alifanya kama alivyoombwa.

Katika uchunguzi wangu nilioufanya, HAKUNA MAHALA POPOTE….nasisitiza…HAKUNA MAHALA POPOTE…nasisitizatena HAKUJAONEKANA MAHALA POPOTE ambapo Bi Josephine aliomba, ama alidai aualilazimisha kupewa japo hela ya kupoteza muda wake achilia mbali hizo Mil. 10 zinazodaiwa kulipwa kwa Josephine.Mwana mama huyualijitolea yeye kama yeye na pia aliitoa hiyo package ili ijaribiwe naikionekana itafaa kwa matumizi ya chama ndipo waitumie

Bwana Mwigamba sio tualishindwa kuitumia hiyo package bali pia alijitetea kuikataa kwake kwa kudaiati ile package ya Josephine ni database tu na hivyo isingekuwa na msaada wowote kwa chama. Alipoulizwa Bwana Mwigamba kama anajua tofauti ya Accounting Packagena Database ndugu yetu huyo akabaki kutoa macho na mwishowe akadhihirisha kuwahakuweza kuitumia package hiyo mpya. Baada ya mapungufu na ubovu kadhaa kujionyesha dhahiri ndipo Bwana Mwigamba aliondolewa rasmi kwenye nafasi aliyokuwa nayo. Na yeye imemuumiza na kumkasirisha pamoja na kumfedhehesha sana

Erasto Tumbo. Huyu ndugu kila mwana JF anayejua ukweli wa mambo atakubaliana na mimi kuwa hakuwa akimsaidia Dr. Slaa katika suala zima la uenezi. Zaweza kupita propaganda hata kumi ambazo yeye alitakiwa awe "sharp" kuzipangua lakini utakuta anakaa tu nakungojea posho za vikao au posho binafsi pale ofisini. Huyu nae alipoenguliwa kwenye nafasi yake, alilalamika na kwakweli hakuridhika kabisa na mpango huo nakumwona Dk. Slaa kama adui namba 1

Katika kuthibitish kuwa Erasto Tumbo anahaha kuthibitisha madai yake, hadi sasa yuko bussy akichambua Payment vouchers za Dr. Slaa ili aje nazo hapa JF kama ushahidi kwamadai/utetezi alioutoa Dr. Slaa kuwa wanaomsakama waje na ushahidi hapa jukwaani. Alifika pale Ofisi za chama, akaomba apatiwe payment vouchers, Dr.Slaa alipotakiwa ku-authorise ombi lake alikubali kuwa apatiwe atafute anachokitafuta. Hadi sasa sijajua kama amepata ushahidi au la.

Sitaki niseme kama Tuntemeke na wenzake kuwa ni Mwigamba na Tumbo maana name calling kwa JF ni criminal offence, lakini kila aliye timamu anaweza kuhoji na kufuatilia kuona mtiririko wa mambo unavyokwenda.

Ukweli ni kuwa Dr. Slaa anapokuwa kwenye case kule Arusha, shughuli za Chama huwa zinafanyika pia. Vipo vikao vya siri vya chama vinafanyika ambavyo Slaa mwenyewe anapaswa kuwepo nakushiriki. Lakini pia kwa status ya Slaa pamoja na umuhimu wa vikao vyake pamoja na watu anaokutana nao, HAIWEZEKANI NA HAITAKUJA KUWEZEKANA akaendelea kukaa kwenye hoteli za Sh 40,000/=. Huu ukweli upo dhahiri na kwa mtu anayefikiria ndani ya box anaweza kuelewa kwa undani nini maana ya kuwa Katibu Mkuu wa chama kinachoongoza upinzani Tanzania tena Mtu wa aina ya Slaa. Uhai wake, na ulinzi wake pamoja na umuhimu wake sio vitu vya kuendelea kuviwekarehani hata kidogo.

Lakini pia kuna suala la mtoto mdogo Junior. Huyu mtoto mbali na usalama wa wazazi wake kuwa kitu muhimu, mtoto huyu kwa umri wake ni lazima na yeye aishi mahali penye usalama kila anapokuwa nje ya makazi ya wazazi wake.Makazi yenye usalama ambayo yako dhahiri kwa mtoto huyo na wazazi wake hayawezi kupatikana kwenye hoteli za kawaida za gharama za chini. Hii ndio siasa, na haya ndio mafuta ya siasa na gharama kama hizi ndizo zinazotokea kwenye siasa.

Nimefuatilia kuhusu madereva wanaompeleka Josephine kanisani, HAKUJAWAHI KUTOKEA HILO JAMBO. Huu niuongo tena umesukwa mahususi na ndugu zetu hao ambao nataka niwahakikishie wanaJF wanaosuka mpango huu HAWANA UHUSIANO NA WALIOSHINDWA BAVICHA. Josephine anadrive gari yake mwenyewe. Na analihudumia gari lake mwenyewe kwa pesa halali ya jasho lake hata pale anapokuwa anafanya baadhi ya kazi za kukisaidia Chama. Kama kuna madereva wanalipwa basi ni kutokana na kazi zao kwa mujibu wa mikataba yao ndani ya chama.

Kifupi tu nimalizie kwakusema kuwa, kama umeshindwa kazi na mamlaka halali zikakutoa kwenye nafasi uliyokuwa nayo, ni vema ukawa na adabu na kutulia ikiwezekana kuomba radhi nahuenda ukapewa onyo ukarudishwa kwenye nafasi yako. Uzushi wa kabila hili kamaulivyotolewa na kina Tuntemeke hauwasaidii wao wala hauna tija kwao.
Kusema ukweli wanaofanya fitna hizi hawana link ya moja kwa moja na waasi wa BAVICHA kwa sasa.

 
Sasa naanza kupata Picha huyu Tuntemeke alisema kwamba yuko Arumeru kipindi kile hata kampeni hazijaanza.Naanza kudhani kuwa ni Mwigamba,lakini pia mwigamba ni m/kiti wa CDM Arusha na huyu tuntemeke katika moja ya post zake alidai kuwa dr slaa amemtoa aliyekuwa m/kiti wa Arusha na kumpeleka makao makuu.Hivyo inaweza kuwa sio yeye.Anyway issue sio kujua nani ni nani,ishu ni hoja zinazoletwa humu.

Kwa mfano.Mimi naweza kuja na hoja John wewe umeiba sh 300 Million,John atakuja na ku kataa.Mimi inabidi nije na vithibitisho vya kwa nini John umeiba.Hapo ntakua nimemtia john hatiani.Kujificha nyuma ya keyboard na kutoa tuhuma ambazo kama ni mtunzi vizuri unaweza kuzifanya zikaonekana ni kweli,ni jambo hatari.Ingekua vizuri hawa wapenda chama (Tuntemeke &Co) wajitokeze hadharani tuwafahamu wakati wakitoa hoja zoa ,tuwapime na wao kama ni watu ethical enough kuweza kutoa allegations kama hizo,tutawatambua na tutajua,ahaaaa,kumbe ni huyu jamaaa,huyu atakua anatunga kutokana na hsira zake.

Dr Slaa ana mapungufu yake.Ingawa haya yanayosemwa hapa zaidi yamejaa uchonganishi na ni mambo ambayo yameletwa wakati mwafaka CDM kikiwa kwenye mapambano Arumeru.Kunaweza kuwa na ajenda zaidi ya tunazofikiria hapa kwamba ati jamaa wanapigania chama.

Katika siasa za upinzani hata tanzania anaweza puppet akapandikizwa kwenye chama tangu akiwa mtoto,hiyo sio ajabu.Akakua katika chama hicho na hatimaye kuja kukibomoa.Dr Slaa peke yake si CHADEMA,CDM is more than him,ni taasisi.Akifa leo (Mungu aepushie mbali) CDM haiwezi kufa,itakuwa na itazidi kushamiri.
 
Tumeiona ila inasikitisha na kukatisha tamaa! Kweli taifa letu litafikia ukobozi wa kweli? Naona wanasiasa wengi wa bongo ni wachumiatumbo,kwa mtazamo wangu nilikuwa najua ni magamba na TISS! Lets change the system guys!
 
Mkuu mbona tulishafahamu haya! Daima haki haishindwi! Kama mtu unania njema kwanini unapotakiwa kuwajibika unakuwa mbogo! Ugomvi huu umeshavamiwa na maadui wa ndani na nje ya chama!

Chadema inabidi itofautishe mambo ya kitaalamu na siasa! Mwanasiasa alafu ndio mhasibu? Ni tatizo! Waajiri wahasibu ambao wakifukuzwa haitakuwa tabu kama unapofukuza mhasibu alafu anamaslahi ya kisiasa! Erasto kufanya haya sawa lakini Mwigamba sikumtegemea kabisa!

Bora chama kisafishe mamluki mapema! Kuhusu Tuntemeke huyu ni kijana wa mzee Tuntemeke na ni victim wa uchaguzi wa bavicha ila hapa ameongezewa nguvu tu! Intelijinsia itafanya kazi kuwaumbua wote!
 
Mzito K,
Yaani miaka yote hii chama kilichosheheni wasomi hakina Accounting package inayoeleweka? Kuhusu huyo Tumbo, siku zote nimekuwa natahadharisha juu ya hawa wapima upepo wanaokimbilia kwenye vyama baada ya kushamiri kwa vyama hivyo, na sio wao wenyewe kushiriki kuvijenga vyama hivyo. CDM wapo wengi sana. Anton Komu, Joseph Selasini, Msafiri Mtemelwa nk. Watu aina hii ni hatari sana, nashangaa wanapokkuja na nyie kukimbilia kuwatunuku mavyeo. Hivi huyu aliyepumzishwa uhasibu, kama amesomea mbona nafasi ni nyingi tu, aliambiwa uhasibu wake lazima aufanyie CDM?
 
CHADEMA waendelee na utamaduni wake wa kufanya maamuzi magumu hata kama walengwa watakasirika lakini chama kibaki salama. CCM wanapata shida kwa sababu ya kumumunya maneno, mara vua gamba, mara hakuna kitu kama hicho, ili mradi hakuna msimamo unaoeleweka.

Nijuavyo mimi Bi Josephine amewahi kufanya kazi na UNHCR kama database analyst. Na kituo chake kimojawapo ni kambi ya wakimbizi toka DRC huko Kigoma. Hivyo uzoefu wa data base anao. Na hii system ya CHADEMA Bi Joseph ali-VOLUNTEER. Wanaouliza watafute kwanza maana ya neno VOLUNTEER. Hata hivyo binafsi sina shida kama Bi Josephine alifanya kazi za CHADEMA (iwe bure au kwa malipo), cha muhimu hapa ni je, taratibu zilifuatwa? Na je, system yenyewe inasaidia kazi za CHADEMA? Haya ndio mambo ya msingi.

Kuhusu Erasto Tumbo, huyu bwana simfahamu lakini kama ni yeye aliyekuwa anasimamia kuregenzi ya habari CHADEMA wako sahihi kabisa kumuondoa kwenye nafasi hiyo. Kwa muda mrefu wadau wengi hapa JF wamelalamika sana kuhusu mawasiliano hafifu ya CHADEMA. Regia Mtema (RIP) ndiye aliyekuwa anaokoa jahazi mara kwa mara kwa kuwapa watu updates (hata wakati wa matukio makubwa). Ni vigumu kuamini kuwa CHADEMA walikuwa wanamlipa mtu kuendesha hii kurugenzi.

Na kama Bwana Tumbo anasoma hapa JF, kwa nia njema na moyo safi basi nakushauri uachane kabisa na mambo ya mawasialiano. Perfomance ya kitengo hiki chini ya uongozi wako ilikuwa hafifu mno!. Inawezakana ukawa na ujuzi mkubwa sana kwenye mambo mengine lakini for sure sio mawasiliano. Leave that one to someone else.

Kwa kumalizia, CHADEMA wanaweza kutoa official statement kuhusu huu utitiri wa tuhuma once & for all. Lakini wafanye hivyo baada ya kumalizika kwa uchaguzi mdogo huko Arumeru Mashariki.
 
Tunashukuru kwa uchunguzi/utafiti wako, muda si mrefu itajulikana tu chanzo cha haya yote na walio nyuma yake.

Swali langu ni moja tu kumhusu mtuhumiwa mmoja, Samson Mwigamba mwenye mchundo(FTC) katika Electronics & Telecommunication Eng. toka Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) ashindwe kujua tofauti ya package na Database? Kama angekuwa amesoma hivi vyuo vya mtaani vinavyotoa diploma ya miezi mitatu ningekubaliana na wewe moja kwa moja! Ama huyu Samson Mwigamba unayemsema hapa ni mwingine?
 
CDM ni mm wewe na yule alikuwepo mzee Mtei nw kapumzika Dr Slaa nae atapumzika atakuja na mwingine so tujenge chama kama taasisi yetu na wala si kwa ajili ya mtu mmoja kama akina Tumbo walivyowekwa pembeni kina Tuntemeke nao wajitokeze hadharani na hoja Dr atawekwa pembeni kazi iendelee majungu ya nini? Wapo wengi wanaoweza kuongoza hiki chama, Prof. Safari, Dr Kitila, Prof Baregu, Kina Zito et al na wengineo.
Kwa sasa tunaimani na Dr wamwache afanye kazi kama wanamapenzi na chama otherwise watoke hadharani waprove his guilt akae pembeni.
 
Mimi nilishasema hapa!! Watanzania hatutaendelea kwa kuendekeza majungu, fitina, chuki na uzandiki!!
Hii hata kama usingetolea ufafanuzi, haikuhitaji phd kugundua uzandiki uliokuwa vichwani mwa waleta mada!!
Yaani watu wanashindwa kazi wanakimbilia kwenye mitandao!! Ingekuwa kama hapa ugaibuni kitanzi kinawahusu!!
 
Mzito K,
Yaani miaka yote hii chama kilichosheheni wasomi hakina Accounting package inayoeleweka? Kuhusu huyo Tumbo, siku zote nimekuwa natahadharisha juu ya hawa wapima upepo wanaokimbilia kwenye vyama baada ya kushamiri kwa vyama hivyo, na sio wao wenyewe kushiriki kuvijenga vyama hivyo. CDM wapo wengi sana. Anton Komu, Joseph Selasini, Msafiri Mtemelwa nk. Watu aina hii ni hatari sana, nashangaa wanapokkuja na nyie kukimbilia kuwatunuku mavyeo. Hivi huyu aliyepumzishwa uhasibu, kama amesomea mbona nafasi ni nyingi tu, aliambiwa uhasibu wake lazima aufanyie CDM?
it could be a sad fact, but we have to take it positively

what about other political parties?
 
Back
Top Bottom