Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,194
- 4,112
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Burian @batilda.burian amesema jalada la uchunguzi wa tukio tata la Watoto pacha waliozaliwa kabla ya muda katika Kituo cha Afya Kaliua na mmoja wao kunyofolewa jicho la kulia na ngozi ya paji la uso, limekamilika na Watumishi wanne wa Kituo hicho watafikishwa Mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.
Akiongea na CG FM Dkt. Batilda amesema uchunguzi umebaini miili ya Watoto hao ilitunzwa katika chumba cha Wauguzi na sio katika wodi ya Wazazi kama ilivyosemwa awali na Wauguzi hao.
RC Batilda amewataja Wauguzi hao kuwa ni Theresia Kakiziba, Asha Magidi, Paulo James na Benson Maikase na kwamba amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kuwasimamisha kazi Wauguzi wengine wawili walioongezwa katika kesi hiyo.
Itakumbukwa tukio hilo lilitokea May 9, 2023 katika Kituo cha Afya Kaliua ambapo inadaiwa Mtoto mmoja kati ya wawili pacha waliozaliwa kabla ya muda na kufariki alinyofolewa jicho na kuondolewa ngozi ya paji la uso hali iliyozua taharuki iliyopelekea Familia ya Isaka Rafael kugoma kuzika miili ya Watoto hao hadi leo.
Pia soma: