RC Tabora afanya ukaguzi wa barabara ya Kazilambwa-Chagu yenye 36 Km kwa kiwango cha lami

Political Jurist

Senior Member
Sep 6, 2021
120
104
RC TABORA AFANYA UKAGUZI WA BARABARA YA KAZILAMBWA- CHAGU KM 36 KWA KIWANGO CHA LAMI

Tabora
08/01/2023
__________________

Mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe.Balozi.Dkt.Batilda Burian akiambatana na kamati ya ulinzi na usalama (M) Tabora pamoja na uongozi wa (W) Kaliua, amefanya ziara ya ukaguzi wa barabara ya Kazilambwa hadi Chagu inayoendelea kujengwa. Ukaguzi huo ulihusisha barabara inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa km36, ambapo km26 zipo mkoani Tabora na zingine km10 zikiwa mkoani Kigoma.

Na mara baada ya ukaguzi wa barabara hiyo, Dkt. Batilda alifanikiwa kukutana na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Ugansa, kata ya Usoke na kuzungumza nao. Ambapo kabla ya kutoa hotuba yake, alipata nafasi ya kusikiliza baadhi ya kero kutoka kwa wananchi hao, ambapo moja ya kero kubwa ilikuwa ni suala la ardhi ambapo Dkt. Batilda ameahidi kulisimamia suala hilo kwa kufuata kwa kushirikiana na idara husika. Achukizwa na ukiukwaji wa sheria na kuwataka TFS na TAWA kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria.

Kwenye hotuba yake, Dkt Batilda aliweza kujikita kwenye mambo yafuatayo.

Kwenye afya,
Dkt. Alifafanua juu ya uboreshwaji wa sekta ya afya katika mkoa wa Tabora ambao umefanywa na serikali ya awamu ya sita kwa mwaka 2022. Na kwamba hospitali 5 za wilaya, zahanati 52 na vituo vya afya 24 vimejengwa. Na kwamba serikali ya awamu ya sita inakusudia kuhakikisha kila Kijiji kinakuwa na kituo cha afya au zahanati. Amewataka watumishi wa sekta ya afya mkoani Tabora kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia maadili ya kazi, ili kutoa huduma zenye kuendana na uwekezaji unaofanywa na serikali.

Kwenye uchumi,
Dkt.Batilda aliwataka wananchi wa Tabora kutumia fursa mbalimbali za uwekezaji ambazo zinapatikana mkoani Tabora, na kwamba serikali ya awamu ya sita inaunga mkono uwanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo ambavyo vitatumia malighafi mbalimbali zinazopatikana mkoani Tabora. Kwani ukuaji wa sekta ya viwanda utachangia kuongeza pato la taifa na maendeleo ya jamii nzima, asisitiza kutumia malighafi zinazopatikana hapa kama asali, viazi na mihogo.

Maendeleo ya Elimu
Dkt, Batilda Buriani, alifafanua maboresho makubwa yaliofanywa na serikali ya awamu ya sita, ambapo jumla ya bilioni kumi na moja na milioni mia tatu (11,300,000,000) zimetumika kujenga shule na madarasa mapya ambayo yanakwenda kuanza kutumika katika mwaka wa masomo unaoanza hapo kesho. Awataka wenyeviti wa vitongoji na vijiji kusimamia suala la uandikishwaji wa Watoto wa kitado cha kwanza. Awahakikishia wananchi wa Tabora kuwa serikali iko tayari kukabiliana na changamoto zozote kwenye sekta ya elimu mkoani Tabora.

Suala la mradi wa Maji
Dkt.Batilda alifanunua kuwa, serikali ya awamu ya sita imedhamiria kutatua changamoto ya maji mkoani Tabora, kwani tayari serikali imeshatenga fedha kwa ajili ya usambazi wa maji kutoka ziwa Victoria katika awamu ya pili. Na kwamba ukamilishwaji wa mradi huo mkubwa, utachangia ukuaji wa sekta ya viwanda ambapo kwa kiasi kikubwa unahitaji maji ya kutosha.

Na mwisho Dkt.Batilda alitoa shukrani kwa serikali ya awamu ya sita chini ya usimamizi wa Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuleta miradi mingi ya maendeleo mkoani Tabora kwa maendeleo ya wanatabora na Tanzania kwa ujumla. Awataka wananchi kutumia uhuru wa kutoa maoni yao kwa usalama na kuepuka vitendo vyenye kuhashiria uvunjifu wa amani, hasa katika mkutano ya siasa ambayo imeruhusiwa hivi karibuni.

Awataka pia wananchi kutumia muda mwingi kuelezea kazi na juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita, kwani mengi yanaonekana. Awashukuru watendaji wote wa mkoa wa Tabora katika kukamilisha miradi yote ya maendeleo, na kuwataka kuchapa kazi kwa bidii zote.

IMG-20230109-WA0020.jpg
IMG-20230109-WA0018.jpg
IMG-20230109-WA0019.jpg
 
Back
Top Bottom