Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,050
- 50,998
Kwema Wakuu!
Nimefanya uchunguzi mdogo nao ni huu;
"Wale wanaoonekana ni wajinga ndio wanawatawala werevu.
Wale wanaoonekana waovu ndio waliobarikiwa kimaisha.
Wale wanaoonekana wahuni na Malaya ndio wanaoimudu ndoa.
Wale wanaoonekana wengi ndio wanaotawaliwa na waliowachache.
Wale wenye Ujuzi na maarifa ndio wanaotafuta kazi.
Wale waliovipofu tena wasioona maana wapo vipofu wanaoona, sasa hawa ni vipofu wasioona kabisa ndio wanawaongoza wenye macho wanaoona
Wale wanaoonekana ni Wazalendo ndio wezi na wahujumu uchumi.
Wale wanaoogopa sheria ndio wanaokutwa na hatia, Ila wasioiogopa sheria na kuzivunja huwa wenye haki wasio na hatia.
Wale wanaoogopa kuoa na kuzaa kisa maisha ndio hao hao wenye maisha magumu kuliko Wale waliooa na wanaozaa.
Wale wanaoonekana kujibana kiuchumi ili wafanye maendeleo ndio haohao wanaoshindwa maendeleo na Wale wanaotumia pesa Rafu.
Wale wanaoonekana wazuri wa Sura na maumbile ndio haohao wanaokosa wenza wa kuwaona/kuolewa nao ndio wanaolalamika, wakati wasio na mvuto wakiolewa na kuoa kila uchwao.
Wale wanaopenda Kwa watu na vitu vya watu, kwao na vyao ni vibaya.
Wale wanaoonekana ni watumishi wa Mungu ndio haohao wachawi na mashetani Wabaya.
Wale wanaoonekana ni watumishi wa Shetani ndio haohao watumishi wa Mungu aliyehai.
Wale waliofeli Hesabu shuleni ndio wanaofaulu Hesabu za maisha. Huku Wale waliofaulu Hesabu za shuleni wakishindwa Hesabu za mtaani.
Wale WANAOPENDA kulala hawana vitanda na magodoro mazuri lakini ndio wanaolala usingizi mnono.
Wale WANAOPENDA kusoma, husoma habari za watu waliokataa na wasiopenda kusoma, walioshindwa shule.
Wale wanaolima chakula ndio huwa wakwanza kupata njaa, wakati wasiolima wala hawana habari wao chakula kipo Tele siku zote.
Wale wanaoonekana Wana silaha na ulinzi mkali ndio haohao usalama wao mi mdogo na hawana Amani wakati wasio na ulinzi wowote wanausalama Mkubwa na Amani ya roho
Wale wanaozingatia Sana mambo ya Afya ndio haohao hukumbwa zaidi na magonjwa tofauti na Wale wasiozingatia"
Hayo nayo niliyaona kwenye Siasa za Dunia.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam