Uchumi wetu baada ya Magufuli kugoma kuchukua hatua mwanzoni juu ya Corona

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,843
Congo, Zambia, Malawi Watarudi rasmi bandari za Msumbiji! Uganda Rwanda, Burundi watarudi bandari ya Mombasa!

Wakulima watasota na mahindi na maharage na mpunga ambao uwa wana export miaka 2 iliyopita.

Watu watapoteza kazi kwenye magari ya mafuta na bidhaa. Hali itakuwa tofauti wakati wenzetu wanaelekea kufungua uchumi sisi tutakuwa watazamaji.
 
Ukiachia tatizo la mlolongo mrefu wa vibali mara risiti za serikali hapa nnchi , tanzania ndio nchi pekee ambayo gharama ya nafaka ni chini mno na kupitisha mzigo toka nje kupitia tz ni nafuu ya muda na fedha na usalama asilimia 95..hakuna mfanya biashara mjinga kutoka lubumbashi, rwanda, burundi ,zambia ataacha kupitia tz eti kwakusikiliza wanasiasa hawa wanaovuna wasivyopanda...

Ingawa pia serikali yetu kuna vitu vingine muwe na strategies hili linalotokea sasa lingeepukika mapema sana haiwezekani wote mnaomshauri rais hamuoni kinachoendelea ujue hawa majirani zetu wengine hawatutakii mema na ili kutuaribia ndio wanavyotufanyia hivi wanaanza mdogomdogo mwakani wataibua jingine tena nia ni kuhakikisha majirani wema wanapata mashaka taratibu uu tukija kushtuka sumu imesha sambaaa na hapo ndio tutachemka kweli.
 
Lockdown ingefanyika mizigo ingepitishiwa wapi?

Kuwekwa kwa lockdown haimaanishi hayo yasingeendelea. Haswa kwenye vyakula na only essential services na wafanyakazi za essential pia kama kawa wangepiga kazi kwa uangalifu kama kawa. Tatizo bila hata restrictions za kiasi fulani ndio na maambukizi na vifo vinaendelea kupita.

South Korea wameonfoa restrictions haikupita muda, mtu mmoja kaingia club kaambukiza watu 83. Sasa hivi wanasaka close contacts walio kwenye maelfu kutokana na mtu mmoja tu huyo.
 
May 2020

Tanzania kupotea na kukosa ushawishi

Bernard Membe aliyehudumu kama Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania chini ya serikali ya Jakaya Kikwete atoa maoni yake juu ya Tanzania kujitenga



Wasiwasi wa mwanadiplomasia nguli Bernard Membe katika uhusiano unaolegalega baina ya Tanzania na nchi wanachama wa SADC na EAC.

Anasisitiza ni muhimu nchi zote kushirikiana kwa pamoja ktk masuala mbalimbali ikiwemo magonjwa, uchumi na biashara.
 
Zambia kwa sasa wanalima mahindi kutuzidi kwahiyo Zambia sii ile ya zamani

Rwanda wanaagiza kutoka Mexico mahindi yao ambayo watapitishia Mombasa

Kenya ndio hawatuhitaji kabisa

Burundi wao korona ikishashamiri na wakaanza kufa sawasawa watakimbilia Ngara na Kigoma yaani watatuletea Corona na faida ya maambukizi mapya

Kwahiyo tusijidanganye kuwa eti Tanzania hivi tanzania vile

Kwanza ni Mwalimu ndie aliyewashawishi wazambia kutumia Bandari ya Dar ili kuwawekea vikwazo makaburu

Wazambia walikuwa wakiagiza bidhaa zao kutoka South afrika ya makaburu kwa hiyo wakiona ungese wanarudi huko

Kwa hiyo hizi ngonjera za alinacha za abunuwasi ambazo ni porojo za kijinga tuziacheni wajameni bia yetu
 
ukiachia tatizo la mlolongo mrefu wa vibali mara risiti za serikali hapa nnchi , tanzania ndio nchi pekee ambayo gharama ya nafaka ni chini mno na kupitisha mzigo toka nje kupitia tz ni nafuu ya muda na fedha na usalama asilimia 95..hakuna mfanya biashara mjinga kutoka lubumbashi, rwanda, burundi ,zambia ataacha kupitia tz eti kwakusikiliza wanasiasa hawa wanaovuna wasivyopanda...

ingawa pia serikali yetu kuna vitu vingine muwe na strategies hili linalotokea sasa lingeepukika mapema sana haiwezekani wote mnaomshauri rais hamuoni kinachoendelea ujue hawa majirani zetu wengine hawatutakii mema na ili kutuaribia ndio wanavyotufanyia hivi wanaanza mdogomdogo mwakani wataibua jingine tena nia ni kuhakikisha majirani wema wanapata mashaka taratibu uu tukija kushtuka sumu imesha sambaaa na hapo ndio tutachemka kweli.
Umekataa kisha umekubali
 
Tz inaboronga vibaya sana katika mchakato huu tumekuwa aibu ya Afrika na hili liwe funzo kwa wale wafia ccm.
 
12 May 2020
London Uingereza

KIPINDI DIRA YA DUNIA
Ungana na Salim Kikeke kupata habari za Covid 19, ukanda wa Afrika wa EAC madereva wa malori ya mizigo ya safari ndefu Afrika ya MasharikI kupewa hati za kidijitali kuonesha afya zao.


Hayo yamejiri baada ya Viongozi wa Afrika ya Mashariki EAC kukukutana kwa njia ya mtandao. Viongozi hao ni Paul Kagame wa Rwanda, Uhuru Kenyatta wa Kenya, Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda na Salva Kir wa South Sudan wakati Rais John Pombe Joseph Magufuli hakuhudhuria kikao hicho cha mtandaoni kupitia picha-video-mubashara.

Kivukio cha Namanga cha mpakani mwa Tanzania na Kenya cha mulikiwa kurunzi kufuatia mlolongo mrefu wa maroli kushindwa kuvuka mpaka. Hii ni kutokana na taratibu za kiafya za kiprotokali za Kenya na Tanzania kutokupatiwa ufumbuzi.

Dr. Mukhisa Kituyi, katibu mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la biashara UNCTAD akiwahojiwa na BBC toka Geneva, Switzerland anachambua changamoto na mizaha ya viongozi kuona Covid-19 kuwa ni kagonjwa kadogo. Pia shirika la afya duniani WHO laonya baadhi ya nchi kuathirika vibaya kwa kupuuzia kuchukua hatua mapema kukabiliana na Covid-19.

Dr. Mukhisa Kituyi wa UNCTAD amesema ni wakati wa viongozi wa Afrika kuja pamoja kipindi hiki cha Covid-19 kuelezea nchi tajiri na mashirika kama IMF , World Bank kusaidia nchi zao kutokana na madhara ya kiuchumi yaliyokumba nchi zao.
Source : BBC News Swahili
 
Hakuna wa kuikwepa Tanzania

Nyie vijana wa Chadema msiwe km kasuku

Kama hujui mambo ya Uchumi kaa kimya, Mipasho na vioja peleka kwa wazazi wako nyumbani

Jadili Madhara ya majirani kutotumia bandari ya Dar es salaam

Wewe Unajadili habari za Chadema na ccm
Certified idiot
 
Back
Top Bottom