Uchumi wa Magufuli: Precision Air Yapumulia Machine. Yapunguza Wafanyakazi 136!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,601
Wanabodi,

Makali ya Uchumi wa Magufuli, yanazidi kukaza, leo shirika la ndege la Precision Air, limepunguza wafanyakazi 136 wakiwemo cabin crew 10!.

Najua wengi humu mtasema hali hii imechangiwa na kufufuka kwa ATCL na ushindani toka Fastjet, lakini this is not the case, nimepanda zote, ATCL, Fastjet, na Precision, zote hazijai, hivyo purchasing power ya Watanzania kusafiri kwa ndege, imepungua, soon mtashuhudia mashirika mengine yakipunguza frequency na mtashuhudia mabenki yakifungasha na kuondoka.

Japo tunaelezwa Uchumi wa Magufuli unakua kwa kupaa kwa asilimia zaidi ya 7% kunakochangiwa, pamoja na sekta nyingine, na sekta ya usafirishaji, lakini sekta tegemeo la wengi ambayo ni sekta ya kilimo, ukuaji wake unazidi kudidimia kwa kukua kwa less than 3%, hivyo Watanzania walio wengi zaidi leo ni masikini kuliko jana!.

Mwalimu Nyerere alitufundisha kuwa maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu na sio maendeleo ya vitu!. Jee nani anaweza kuniambia kuna maendeleo gani ya watu?, uhusiano wa kukua huku kwa uchumi kunakozungumzwa na hali ya umasikini inayozidi kutopea?, kila mahali ni vilio vya hali ngumu!, hii neema ya ukuaji wa uchumi inamfaidia nani kama mwananchi wa kawaida anazidi kupigika?.

Nimesoma mahali kufichuka kwa siri ya Tanzania tumechukua mkopo dola $ milioni 500 kutoka benk, ya Credit Suisse kwa riba ya asilimia 80%!, hivyo tutalipa dola milioni 900 baada ya miaka 5!. Wachumi wetu humu, jitokezeni mtufafanulie huu ni ukuaji gani wa Uchumi kwa kuogeza deni la taifa, huku maisha ya Mtanzania wa kawaida, kila leo yanazidi kuwa magumu, karibu kila unayemsikia, kilio chake ni Magufuli!, kwa kusema maisha ya leo...ni afadhali ya jana?!.

This is not good at all.

Paskali
Rejea
Tuache Siasa ktk Uchumi: Wachumi tuelimisheni Dhambi ya Fixed Deposit na Faida ya Fedha Kukaa tu BoT

Maendeleo ya kweli TZ Yataletwa na Elimu na Ukweli. Tusidanganye, Tusidanganywe, Tusidanganyike!.

Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows!.

update mchango bora
Paschal sidhani kama hiyo argument yako ina mashiko yoyote. Ungekuja na takwimu za abiria kwa soko la ndani tukakuelewa. Kwa hesabu za mamlaka ya viwanja vya ndege, kuna ongezeko la wasafiri kwa soko la ndani.

Matatizo ya Precision yamekuwapo kwa muda mrefu sana. Mara tu baada ya kuondoka CEO (Mkenya) aliyepita, walijikuta wakiwa na madeni makubwa sana yaliyosababishwa na maamuzi ya kibiashara yasiyo na tija. Maamuzi hayo ni pamoja na manunuzi kwa bei zisizo na uhalisia kama ukodishaji wa ndege, matengenezo ya ndege, huduma, na manunuzi ya bidhaa zinazohusiana na uendeshaji wa shirika la ndege.

Baada ya kujitengeneza madeni makubwa, walipatwa na balaa lingine la kupotea kwa umilki wa soko baada ya fastjet kuanza safari zake huku wakijificha nyuma ya bei za chini ili kumuangamiza precision kisha watoze bei kubwa. Precision mwenyewe kama sio huo ubabe wa fastjet angetumaliza kwa bei za juu ili kufidia madeni yake kwa kusaidiwa na ukiritimba (monopoly) wa soko aliokuwanao.

Hivyo pamoja na uhuni wa fastjet, kuna faida pia kuwa alituepusha watanzania na balaa la kufidia madeni ya precision yaliyotokana na uzembe wa menejimenti hasa CEO na mkuu wao wa fedha CFO (mkenya pia). Hicho kidogo walichokuwa wakiambulia baada ya ujio wa fastjet kimezidi kupungua baada ya ATCL kuingia kazini. Makali ya madeni yao sasa ni dhahiri na hawana jinsi bali kufunga mikanda na kuhakikisha hawafi au kufilisiwa kwa madeni.

Kumbuka kuwa hadi sasa hawajamaliza kulipa mikopo ya ndege zao walizonunua kwa udhamini wa benki fulani na mashirika ya fedha ambayo huruma ya kukukopesha huisha ghafla unaposhindwa au kuonyesha kuwa uwezo wa kulipa umepungua. Kenya airways anafuatilia kwa makini dalili za kifo cha precision maana ni faraja kwake.

Nasema ni faraja maana alikuwa na uwezo wa kumnusuru toka zamani kama angetaka kufanya hivyo. Alikuwa na uwezo wa kumpa ndege kubwa precision kwa ajiri ya safari za masafa marefu kutoka Dar es salaam moja kwa moja lakini hakutaka kufanya hivyo ili amtumie kama ndoo ya kujaza pipa. Kumruhusu precision kuwa na uwezo huo kungepunguza abiria ambao wanapelekwa kujaza ndege za Kenya airways hapo Nairobi. Precision akikaribia kukata roho si ajabu Kenya airways akamsaidia asikate roho kwa kuweka fedha kwa masharti kuwa mtaji wa kenya airways ndani ya Precision utaongezeka na kumuacha kilema badala ya kufa kabisa.

Paschal, kwa ufafanuzi huu wa hali ya chini ni wazi kuwa swala la kupunguza wafanyakazi wa precision halihusiani na Makali ya Uchumi wa Magufuli bali ubadhirifu wa uongozi uliopita, kufuka kwa ATCL na ushindani toka Fast Jet, na ujanja wa Kenya Airways.

Mwangaluka bhabha.
Thanks, very objective contribution
P
 
Paschal sidhani kama hiyo argument yako ina mashiko yoyote.

Ungekuja na takwimu za abiria kwa soko la ndani tukakuelewa. Kwa hesabu za mamlaka ya viwanja vya ndege, kuna ongezeko la wasafiri kwa soko la ndani.

Matatizo ya Precision yamekuwapo kwa muda mrefu sana. Mara tu baada ya kuondoka CEO (Mkenya) aliyepita, walijikuta wakiwa na madeni makubwa sana yaliyosababishwa na maamuzi ya kibiashara yasiyo na tija. Maamuzi hayo ni pamoja na manunuzi kwa bei zisizo na uhalisia kama ukodishaji wa ndege, matengenezo ya ndege, huduma, na manunuzi ya bidhaa zinazohusiana na uendeshaji wa shirika la ndege.

Baada ya kujitengeneza madeni makubwa, walipatwa na balaa lingine la kupotea kwa umilki wa soko baada ya fastjet kuanza safari zake huku wakijificha nyuma ya bei za chini ili kumuangamiza precision kisha watoze bei kubwa. Precision mwenyewe kama sio huo ubabe wa fastjet angetumaliza kwa bei za juu ili kufidia madeni yake kwa kusaidiwa na ukiritimba (monopoly) wa soko aliokuwanao.

Hivyo pamoja na uhuni wa fastjet, kuna faida pia kuwa alituepusha watanzania na balaa la kufidia madeni ya precision yaliyotokana na uzembe wa menejimenti hasa CEO na mkuu wao wa fedha CFO (mkenya pia). Hicho kidogo walichokuwa wakiambulia baada ya ujio wa Fastjet kimezidi kupungua baada ya ATCL kuingia kazini.

Makali ya madeni yao sasa ni dhahiri na hawana jinsi bali kufunga mikanda na kuhakikisha hawafi au kufilisiwa kwa madeni. Kumbuka kuwa hadi sasa hawajamaliza kulipa mikopo ya ndege zao walizonunua kwa udhamini wa benki fulani na mashirika ya fedha ambayo huruma ya kukukopesha huisha ghafla unaposhindwa au kuonyesha kuwa uwezo wa kulipa umepungua.

Kenya airways anafuatilia kwa makini dalili za kifo cha precision maana ni faraja kwake. Nasema ni faraja maana alikuwa na uwezo wa kumnusuru toka zamani kama angetaka kufanya hivyo. Alikuwa na uwezo wa kumpa ndege kubwa precision kwa ajiri ya safari za masafa marefu kutoka Dar es salaam moja kwa moja lakini hakutaka kufanya hivyo ili amtumie kama ndoo ya kujaza pipa.

Kumruhusu Precision kuwa na uwezo huo kungepunguza abiria ambao wanapelekwa kujaza ndege za Kenya airways hapo Nairobi. Precision akikaribia kukata roho si ajabu Kenya airways akamsaidia asikate roho kwa kuweka fedha kwa masharti kuwa mtaji wa kenya airways ndani ya Precision utaongezeka na kumuacha kilema badala ya kufa kabisa.

Paschal, kwa ufafanuzi huu wa hali ya chini ni wazi kuwa swala la kupunguza wafanyakazi wa precision halihusiani na Makali ya Uchumi wa Magufuli bali ubadhirifu wa uongozi uliopita, kufuka kwa ATCL na ushindani toka Fast Jet, na ujanja wa Kenya Airways.

Mwangaluka bhabha.
 
Hii inatafsiri kwenye mapato ya serikali,ukiona makampuni yanapunguza wafanyakazi,ujue mapato serikalini yanapungua(PAYE---kodi ya mishahara)

Ukiona biashara zinapungua,jua hata TRA mapato yanapungua,ukiona bar hazina watu,jua kampuni za bia haziuzi bia, na kama haziuzi basi TRA hawapati kodi

Unaweza kujifanya mjuaji ukasema unanyoosha wananchi kumbe "unajinyoosha mwenyewe" hao wafanyakazi wa serikali unawalipa kutokana na kodi unayokusanya mitaani,lakini umezungukwa na kundi la watu wanaokuimbia "wanyooshe" bila kujua kwamba mwisho wa siku ukishindwa kuendesha serikali haohao watakugeuka

Serikali imeshindwa kuajiri,haina pesa,hata wale watu binafsi walioajiri,inawawekea mazingira ya kuwafukuza kazi watanzania,
 
"kuna watanzania wachache wanapata raha ajabu,hao mimi nitalala nao mbele.Msiwaunge mkono watu hao" JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI(20/09/2017 ufunguzi wa barabara Mererani)
-siku hizi bombardie zinajaa kama mabasi ya mwendokasi
-wapiga dili ndio wanalalamika
-mishahara ni ileile haijashushwa sasa maisha magumu yanatoka wapi?
 
Mfumo wa uchumu wa Magufuli fake ''Ameweka mifumo mizuri ya kukusanya kodi lakini Halipi Madeni ya Ndani hapo hawezi kufanikwa Hiyo mifumo Hailipi kodi anaye lipa kodi ni mimi na wewe, ni sawa na kumkamua Ng'ombe halafu bila lishe ''No welfare for his people''
 
Back
Top Bottom