Uchumi wa kati: Tuwe waangalifu na takwimu, figures can lie!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,320
24,190
Nimefuatilia kwa karibu huu mjdala wa World Bank kuitaja Tanzania kuwa nchi ya kipato cha wastani wa $1080 kwa kila mtanzania.

This can be misleading. Hapo kuna mchezo wa hesabu ambao Watanzania wengi hawataelwa na kuona ukweli wa hai halisi.

Tatizo la hesabu za wastani ni kutochukulia ukweli kuwa unahitaji mtu mmoja tu au wawili kuongeza wastani wapato la taifa.

Mimi si mchumi lakini GNI, Gross National Income ni jumla ya pato la Taifa ukiligawanya kwa jumla ya watu wote wa Taifa hilo. Hivyo unapata wastani wa pato la kila mtu katika Taifa.

Hivyo basi ukipata kina Sininu Laizer 10, wenye mapato wa bilioni 10 kila mmoja, ati pato la mtanzania kwa wastani limeongezeka, kwa vile umepata mabilionea kumi!
Wakati huo huo yle mkulima wa mahindi Sumbawanga, yule wa pamba kule Misungwi haguswi kimaendeleo na chochote walichopata hao mabilionea 10.

Ndio maana nasema figures can lie, but liars can figure it out!
 
Hizo bilioni nane za laizer zinatumika Tanzania na watanzania mfano akijenga mall wauza vifaa vya ujenzi kibao watazipata ,wajenzi, vibarua ,mama ntilie nk Mall ikiisha itatoa ajira na kutajirisha watu kibao watakaoiuzia mall bidhaa nk wewe huelewi wastani wa kiuchumi unachukulia Kama hiyo pesa haizunguki!!!

Hesabu za uchumi hazidanganyi

Tatizo mnasoma kwa kukariri upate digrii sio kuelewa matokea ndio huu ujinga umeandika
 
Kukosa akili nako ni bahati ya mtu.
Maana ukiwa mbumbumbu huwa mtu anatembea kama zuzu.
Ssasa Laiza kapata bilioni zake nane kasoro, hongera umetajirika!
 
Nimefuatilia kwa karibu huu mjdala wa World Bank kuitaja Tanzania kuwa nchi ya kipato cha wastani wa $1080 kwa kila mtanzania.

This can be misleading.
Hapo kuna mchezo wa hesabu ambao Watanzania wengi hawataelwa na kuona ukweli wa hai halisi.
Tatizo la hesabu za wastani ni kutochukulia ukweli kuwa unahitaji mtu mmoja tu au wawili kuongeza wastani wapato la taifa.

Mimi si mchumi lakini GNI, Gross National Income ni jumla ya pato la Taifa ukiligawanya kwa jumla ya watu wote wa Taifa hilo. Hivyo unapata wastani wa pato la kila mtu katika Taifa.

Hivyo basi ukipata kina Sininu Laizer 10, wenye mapato wa bilioni 10 kila mmoja, ati pato la mtanzania kwa wastani limeongezeka, kwa vile umepata mabilionea kumi!
Wakati huo huo yle mkulima wa mahindi Sumbawanga, yule wa pamba kule Misungwi haguswi kimaendeleo na chochote walichopata hao mabilionea 10.

Ndio maana nasema figures can lie, but liars can figure it out!
I agree with you ...numbers don't lie but people do lie
 
Yah, Hizo GNI sio kipimo sahihi cha uchumi wa wananchi katika nchi husika. Ni pato la kufikirika la wananchi. Sio pato halisi.
 
Back
Top Bottom