Uchumi unaimarika bei ya mchele yashuka kutoka sh.2600 hadi sh.1300 kwa kilo!

Imeelezwa na maafisa masoko wa jiji la Dsm kuwa bei ya mchele imeshuka kutoka sh.2600 hadi sh.1300 kwa kilo na itaendelea kushuka hadi kufikia sh.1000 kwa kilo. Hali kadhalika bidhaa nyingine muhimu za chakula bei zimeendelea kushuka ikiwa ni ishara ya kuimarika kwa uchumi. Source Eatv habari!
mchele umeshuka hadi sh 800 kwa kilo, sababu siyo kuimarika kwa uchumi bali ni kwa kuwa mpunga umeiva na wakulima ndo wanavuna Sana, acha siasa jamani hapa ulitaka kumsifia Rais, mbona vitu vingine vipo juu Kama uchumi umepanda?
 
Hata pale Kyela kwenye mashine ya kukoboa kutoka mashambani hauuziwi hivyo mbali na kwamba ni mpunga mpya ambao haujaiva vizuri! Huo mchele mnaouziwa hivyo utakuwa unapatikana huko Lumumba ndani na mlikula jana na limwenyekiti lenu lilipoenda kuwatembelea.
 
Bei ya Mchele mzuri Sumbawanga kwa Wakulima ni Tshs. 1400/=, wa kati ni 1200/= Vimeo ni 800/= kwa kg 1.
 
Mleta thread naomba kujua 'ilimu' yako ilikomea wapi. Kuimarika kwa uchumi ni mchele kusjhuka bei tu? da! huyu atakuwa mchumi wa Lumumba.
 
Njoo vijiji vya kata ya Mwamala wilaya ya Nzega mkoani Tabora gunia ni 36,000 mwisho 45,000 na bado wanavuna hapo.

Duru zinadai kilo itafika hata 800 huko lakini hii wala siyo ishara ya uchumi kuimarika,Kuna watu wataumia.
nahifadhi hizi comment zenu bidhaa zitakapo pand bei msiseme uchumi umeshuka hahahah
 
Imeelezwa na maafisa masoko wa jiji la Dsm kuwa bei ya mchele imeshuka kutoka sh.2600 hadi sh.1300 kwa kilo na itaendelea kushuka hadi kufikia sh.1000 kwa kilo. Hali kadhalika bidhaa nyingine muhimu za chakula bei zimeendelea kushuka ikiwa ni ishara ya kuimarika kwa uchumi. Source Eatv habari!
Kweli wewe ndiyo kilaza yaani unakubali kuuza utu wako kwa buku 7?
 
Acha kupotosha watu humu wewe uliyezoea kulishwa taarifa! Yaani uutoe mchele shinyanga kijijini au kule pawaga au mlimba uje uuze sh. 1300/=? Unaijua bei ya kukodi gari? Ya diesel nayo unaijua? Gharama za mkulima nazo ni sifuri? Jiongeze dogo na piga simu kwenye vyanzo vya mpunga huko kyela na madibira ujuzwe sio unajiropokea humu! Yaani ni hujui lolote!
Ni kilaza tu wa lumumba hajui atapataje buku 7
 
Back
Top Bottom