Uchumi unaimarika bei ya mchele yashuka kutoka sh.2600 hadi sh.1300 kwa kilo!

nahifadhi hizi comment zenu bidhaa zitakapo pand bei msiseme uchumi umeshuka hahahah

Bei za mazao kushuka bei ndiyo kuimarika kwa uchumi?

Kwa hiyo mwaka Jana bei ya mbaazi ilipoporomoka kutoka 3000/- hadi 300/- kwa kilo uchumi uliimarika?

Sasa kwa nini serikali ilihaha hadi kutuma ujumbe India kuwabembeleza wanunue?

Akili Ni nywele.
 
kweli mchele umeshuka Sana bei ya jumla hapakwetu mwanza ni tsh 1000per kg bei ya rejareja ni tsh 1300 -1500
 
Mkuu naandika sasa hivi MWANZA BEI YA MCHELE NI 950 KWA KILO
FIKA MABATINI UJIONEE,TUNASHKURU KWA MUNGU BEI HII KUSHUKA KUTOKANA NA MFUNGO WA RAMADHANI TUNAO JIANDAA NAO WIKI IJAYO
naomba radhi mkuu kwa hlo ila sio sehemu zote labda ni huko kikubwa safi sana tumieni fursa hiyo nunueni muweke akiba maana
 
Mnazingua!jana nimenunua Mchele Makambako mchele debe wanauza 42,000
 
Huku dar sioni nafuu yoyote au huku uchumi umedorora, mchele mzuri 2200 kilo lasivyo utumie wa 1700 uchambue saana, huku mtaan kwetu hilo gari la kushusha uchumi halijafika
 
Back
Top Bottom