Uchumi kwanza, Katiba isubiri. Acheni chokochoko!

Suphian Juma

Senior Member
Apr 2, 2019
133
546
UCHUMI KWANZA, KATIBA ISUBIRI. ACHENI CHOKOCHOKO.

Ilikuwa asubuhi na mapema mwezi uliopita wa Sita mwaka huu 2021 naamka na kukutana na ujumbe wa simu kutoka kwa rafiki yangu James Michael, Afisa TEHAMA wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kagera__"Kaka Suphian naona CHADEMA wakisapotiwa na wanaharakati kama Kigogo, Dada yako Maria Sarungi na wengine wameanzisha na kumshinikiza Rais Samia aanzishe mchakato wa Katiba Mpya, una maoni gani au tufanyaje?"

"James nimepata ujumbe wako, naomba nifuatilie nione madai yao, ili kama yanafaa kuungwa mkono basi tuyaunge ama kama yatakuwa hayana maantiki basi tuyapinge kwa hoja." nilimjibu rafiki yangu huyo.

Huu ndio ulikuwa mwanzo wa kuanzisha Hashtag pendwa na iliyobeba maslahi na maono mapana kwa SASA kwa Watanzania iitwayo #UchumiKwanzaKatibaIsubiri kupingana kwa hoja na wenzetu hao "wachache" walioanzisha Hashtag yao ya #KatibaMpyaMovement

Hivi kwanini madai ya Katiba mpya yameibuliwa ghafla na Chama cha CHADEMA, ACT Wazalendo wakishirikiana wa wanaharakati? WHY NOW? Ni madai 'mtambuka' ya wananchi wote au tu agenda yao ya kisiasa ya kujijenga kivyama mbele ya wananchi baada ya Rais wetu Samia kuzidi kutekeleza kila aina ya agenda walizokuwa nazo awali? Tuendelee kutafakari.

Wakati Rais Samia anashika usukani mwezi Machi mwaka huu tujiulize hao wadai Katiba Mpya walidai nini kama kipaumbele au vipaumbele vyao vikuu? Katiba Mpya? BIG NO. Walikuwa na agenda zifuatazo ambazo zimetibiwa haraka na Serikali ya Rais Samia na kuwashangaza na hivyo kubadili gia angani.

Kwanza walichokidai ni utawala wa Sheria, walitaka viongozi, wanachama na washirika wao waliosekwa magerezani wawe huru. Rais Samia aliwasikiliza: mashekhe wa UAMSHO, akina Mdude, viongozi zaidi ya 20 wa CHADEMA mkoa wa Singida walifutiwa kesi zao haraka bila kusahau na zile 300M walizowahi kulipa CHADEMA mahakamani kulipwa kwao kwa amri ya Mahakama Kuu. Najua 'inauma hiyo' agenda zinapukutika.

Sio hivyo tu hata viongozi wa Serikali waliowahi kulalamiwa kuwaonea wengine kupitia nyadhifa zao nao wameanza kuchukuliwa hatua ikiwemo kufunguliwa mashtaka kama ilivyotokea kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Ole Sabaya.

Kama ni Uhuru wa Kujieleza ambao hao akina CHADEMA, ACT wazalendo na washirika wao walilia nao sana, Mama alishatangaza wawe huru kumkosoa yeye na Serikali yake, na ni kweli leo hii watu wanakosoa mno tena wengine vijana wao akina Mdude kuongezea na vitisho na kebehi lakini si Rais wala Serikali na vyombo vyake ambavyo vimemkamata yeyote.

Agenda nyingine ilikuwa Uhuru wa vyombo vya Habari, vyama vya Upinzani kwa nyakati tofauti tangu 2015 na hata alipoingia Ikulu Rais Samia, wamekuwa wakilaumu vyombo vya Habari kufungiwa na kuzibwa midomo katika kutekeleza Kazi zao. Rais Samia alishaagiza vyombo vifunguliwe na vyote viachwe huru, tujiulize kuna chombo chochote kimewajibishwa kwa kuikosoa Serikali? Leo hii Tvs, Online Tvs na Magazeti yanaandika hata Habari za "ufukunyuzi" wa Serikali kama watakavyo, hakuna kiongozi yeyote wa Serikali anawapa onyo wala kuwafungia.

Demokrasia: Leo hii vyama vya Upinzani vinajiachia, vinafanya mikutano ya ndani, viongozi wao wanazunguka nchi nzima: juzi juzi tu Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amefanya ziara mikoa kadhaa nchini, amekamatwa na nani? Tena tukumbuke pia Rais alishatangaza kuwaomba aonane na vyama hivi vya Upinzani wajadili agenda zao, na za kitaifa... Ingawa sijui watajadili nini maana agenda zao zote zinazidi kutimizwa kwa kasi ya 5G haha

Kama ni suala la wafanyakazi kupata stahiki zao, Rais alishatangaza Mei Mosi kupandishwa madaraja, kulipwa malimbikizo na ajira mpya, vitu ambavyo havikufanyika zaidi ya miaka mitano iliyopita. Juzi tu nimeongea na Rafiki zangu walimu kadhaa wanasema mambo ni safi kwenye accounts zao... Nani kama Mama?

Najua "inauma hiyo" kwa vyama janjajanja kuona agenda zinatekelezwa. Wengine hupenda tabu na kero ziwepo kwao na wananchi ili wapate agenda. Sasa Hakuna pa kushikilia. "Inauma hiyo" haha ha ha.

Rais amesema tumpe muda atatekeleza agenda ya Katiba Mpya, auhuishe uchumi wetu kwanza, mnakataa kumwamini kwanini wakati agenda zenu zote amezitekeleza ama anazidi kuzitekeleza kwa kiwango kisichomithilika?

Uchumi wetu mpka umeporomoka kwa kiwango kikubwa kwa takribani 3% sababu kuu ikiwa ni gonjwa la Corona, na Rais anapambana na Serikali yake kuweka mazingira mazuri ya Uwekezaji na ndio maana mwaka huu (miezi michache tu alipoingia Ikulu Rais Samia) wawekezaji wapya waliojitokeza kwa mujibu wa Taarifa ya Serikali ni maradufu ya waliojitokeza mwaka jana.

Hamuoni hii ni kheri? Sio nyie ambao ulikuwa mnapiga kelele 'vyuma vimekaza'? Sasa Mama anavilegeza ili wananchi watunishe mifuko yao nje mnamletea chokochoko, nyie ni wawakilishi wa wananchi kweli?

Kwanini Mama asiweke mazingira Mazuri kwanza kwa wananchi wasipate maji safi, umeme wa uhakika, barabara bora kama Chama chake cha CCM kilivyoahidi kwenye Ilani yake ya 2020/2025, halafu Katiba ifuate? Hamjui mshika mbili moja humponyoka??

Kwanza hamjui mchakato wa Katiba unatumia mabilioni ya hela na raslimali nyingi za nchi? Mnataka wananchi wanyimwe madawa, wafanyakazi wapunguziwe stahiki walizoanza kulipwa? Wahitimu waendelee kusota mtaani bila ajira? Watoto wetu waliofaulu kwenda Chuo wakose mkopo? Kupanga ni kuchagua, sasa ni Uchumi kwanza, Katiba Isubiri.

Si Rais Samia tu bali CCM pia inapenda Katiba mpya na ndio maana Rais Mstaafu Kikwete (wa CCM) alikubali kuanzisha mchakato wa Katiba mwishoni mwa Uongozi wake, lakini ni nani aliyeukwamisha mchakato huo kama sio nyie CHADEMA baada ya kuona agenda yenu ya kuuvunja Muungano kugonga mwamba? Katiba Isubiri.

Leo hii ghafla mmeona Rais Samia ana mwendo unatia fora, anatatua kero za wanasiasa na wananchi wote, mnaamka na agenda ya Katiba Mpya ghaflaghafla ilimradi tu mumutoe kwenye reli asiwahudumie wananchi mfaidike nyie kisiasa. Katiba Isubiri.

Hold on: Hivi mnavyosema wananchi wanataka Katiba Mpya kwa uharaka huo, ni wananchi gani hao? Asilimia ngapi? Utafiti huo mliufanya lini mwaka huu? Mbona hamuukuweka wazi wala kuuzindua? Hii ni agenda yenu ya vyama vya siasa na si ya wananchi wote. Kaeni kwa kutulia. Katiba Isubiri.

Binafsi nilidhani kwa kuwa Sheria ya vyama vya siasa na hata katiba zenu zinawaelekeza kuwatetea na kusimamia maslahi ya wananchi, mngejikita kumpa sapoti Rais Samia kuuboresha uchumi wetu ikiwemo kutoa mawazo Mbadala na hata kufanya lobbying nje wawekezaji waje wengi, tukuze uchumi wa wananchi badala ya hizi chokochoko za Katiba Mpya.

Pia nadhani mngemshukuru Rais Samia kutangaza kutopuuza suala la Katiba Mpya kwa kuonesha nia ya kulishughulikia, maana kwa utaratibu wa Kikatiba Tanzania, Chama kitakachoongoza Serikali ndicho Ilani yake itatekelezwa. CCM ni Chama Tawala, na kwenye Ilani yake ya 2020/2025 Katiba Mpya haipo. Katiba Isubiri

Tunaelewa mna uhaba mkubwa wa agenda Kwa sasa, kutokana na uimara na Usikivu wa Serikali ya sasa chini ya Rais Samia, ambapo agenda zenu nyingi zimemezwa. Kuweni wabunifu. Anzisheni agenda mpya zinazoendana na muktadha wa sasa. Ila Katiba Isubiri.

Msitake kuleta chokochoko alizosema Rais Samia, lengo mlete ufitini kati ya Serikali na wananchi kwa masuala ambayo majibu yapo wazi. Mama ni Mpole, amejaa busara na hekima, msitake kuvuruga amani kwa makusudi ili mkidhibitiwa, mpate agenda eti mnaonewa na kwamba Rais ni Dikteta. Katiba Isubiri.

Najua wapinzani na washirika wao wataachana na hoja, wataanza kunishambulia Mimi Suphian mtoa hoja. Nawaasa waache siasa za kale, hoja hujibiwa kwa hoja. Wasinilazimishe niikubali misimamo yao kisa nilikuwa Mpinzani. Wasijione wao wanahodhi ukweli. Mimi ni CCM nitasimama na misimamo 'bora'ya CCM na Mwenyekiti wetu kwa faida ya wananchi wote na Taifa. Katiba Isubiri.

Wito wangu kwa Watanzania naomba tumuunge mkono Rais wetu kuuhuisha uchumi wetu na masuala mengine mtambuka ya kitaifa kwa kutoa maoni yetu kwa mitandao ya kijamii kwa kutumia Hashtag tuliyoianzisha ya #UchumiKwanzaKatibaIsubiri

Hashtag hii inasaidia hoja zenu ziwafikie wengi na kurahisha 'visibility' yaani kuonekana kwa hoja zenu pindi mtu akitaka kufuatilia. Ni muda sasa kusimama na Mama ili kuukuza uchumi wetu uliobomoka. Ni muda sasa kuzipuuza siasa janjajanja, na kusimama na maendeleo ya wananchi.

Mwisho nawashukuru sana vijana mbalimbali kutoka mikoa yote nchini na hata viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, na AZAKI waliojitokeza kusapoti #UchumiKwanzaKatibaIsubiri narrative, tuliyoianzisha hususani katika mtandao wa Twitter. Tuendelee kupaza sauti. Tumsaidie na kumwombea Rais Samia atuvushe salama tuwe nchi bora ya kuigwa kwa kila mema.


Suphian Juma,
Mwanachama wa CCM,
Singida, Tanzania.
Julai 10, 2021.

Mawasiliano:
Simu: 0717027973
Email: yessuphian@gmail.com


FB_IMG_1625919418360.jpg
 
Wewe utakuwa mjinga no-1

1. Wenzenu wachache akinanani?

2. Ulifanya sensa lini au utifiti kutambua wachache? Wangapi?

👇👇



 
Msikilize Athony Diallo Suphian Juma

Je, wewe ni mmoja wa vichaa? CCM wenzako wanataka katiba mpya. Chache au wingi unaupataje?

 
Suphian Juma ,

..nadhani unakosea kuamini kwamba Raisi " akitekeleza " basi wapinzani au vyama vya siasa vinaishiwa hoja au ajenda.

..kwa kifupi ni kwamba kila Raisi na serikali wanapotekeleza kunaibuka changamoto na hoja mpya ambazo inabidi zifanyiwe kazi.

..changamoto hizo mpya ndiyo huwa ajenda zinazobebewa bango na vyama vya siasa ili zitekelezwe na serikali iliyoundwa na chama tawala.

..Nakushauri uondokane na dhana / imani kwamba Raisi anaweza " kutekeleza " mpaka vyama vya siasa vikakosa ajenda, au wananchi wakawa hawana changamoto. Hali hiyo haijawahi kutokea mahali popote pale duniani.
 
Ni jambo zuri kuweka namba ya simu na email address, in case of anything. But katiba mpya ni kwaajil ya maslahi na ustawi wa Taifa na c kwa individuals.
 
... March 17, 2021 was the greatest milestone of this nation. Ni tarehe ambayo, sio kwamba umuhimu wake ni tukio lenyewe, bali ni mwanzo wa fikra na mtazamo mpya kama taifa.

Ni tarehe ambayo inatukumbusha matokeo ya maamuzi yetu kwa umoja wetu; tunafikiri sawa sawa kabla ya kuamua? Au tunaamua tu kwa ushabiki wa kimakundi bila kuzingatia athari za maamuzi yetu hayo?

Nyenzo zetu (Katiba, sheria, mifumo, n.k.) iko stable kutusaidia pindi tukikosea kimaamuzi au tuliyemwamini akatutenda ndivyo sivyo? Au tunaamua kukabidhi mamlaka na madaraka yetu kwa wachache watende kwa niaba yetu huku tukibaki "yatima, watazamaji, hatuna la kufanya, n.k." baada ya kukabidhi madaraka yetu? Aliyekuwa "amelala" na aamke sasa!

Apumzike kwa amani Beatrice Kamugisha angeidadavua vizuri sana mada hii!
 
Vijana tunayumba sana hata kuaminika kunaisha kabisa! Mara uko CHADEMA, muda mfupi uko ACT, hujamaliza miaka hata mitano uko CCM. Huwa najiuliza, hata jamaa, ndugu, watoto wako na mke wake wanakuelewaje?
 
"Katiba Mpya isubiri kwanza wakati kila siku mnahangaika bungeni kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali" - Jaji Warioba.
 
Kijana unayumba!! Hivi ni chama gani kiliunda Tume ya Warioba kukusanya maoni ya Katiba Mpya kwa wananchi? Vipi kuhusu mwitikio wa wananchi juu ya maoni yao? Au mwezetu ulikuwa sayari ingine?
 
Sufhian naona unataka kupotosha kwenye hoja ya takwa la katiba mpya (mimi nikiwemo). Tatizo kubwa la katiba haliko kwenye mtu, liko kwenye "institutions" (mahakama, bunge e.t.c) tuna taka katiba itakayoweka "strong institutions" zitakazotuongonza kama nchi, sasa kwasababu tu wewe unaamini raisi Samia amekuwa kiongozi(mtawala?) mzuri haimaanishi takwa la katiba mpya halina maana. Noooo! Tunaoamini katiba mpya ni muhimu tunataka madaraka yarudi kwa wananchi pamoja kuwa na "strong institutions".
 
Acha ujinga wewe!!!! Yule dhalimu kwa miaka mitano kazuia demokrasi nchini lakini bado uchumi ukaanguka. Huyo samia asitafute kisingizio cha kukuza uchumi wakati hana uwezo wa kufanya hivyo kwa sababu alikuwemo kwenye Serikali ya dhalimu magufuli. Wasaliti kama wewe ni hasara kubwa kwa Taifa. Sasa hivi umeamua kuwa malaya wa kisiasa ili kufukuzia TEUZI!!


86663FE8-7586-416B-A65A-089790D4DFDE.jpeg
 
Sijasoma makala yako ndefu ambayo bila shaka najua haina chochote cha maana kwani nafahamu lengo lako ni kujipendekeza ili kuganga njaa kwani kila uchao hali inazidi kuwa ngumu.

Elewa kwamba nchi hii haijaanza kujenga huo uchumi leo, hata baada ya vita na Uganda kumalizika mwaka 1979 Nyerere alituambia tufunge mkanda kwa miezi 18 tujenge uchumi na imeenda hivyo hadi leo bado "wanajenga uchumi".

Hivyo uchumi isitumike kama kisingizio cha kuzuia watu tusipate katiba mpya uchumi utajengwa siku zote hakuna siku wataacha kujenga huo uchumi.
 
Acha ujinga wewe!!!! Yule dhalimu kwa miaka mitano kazuia demokrasi nchini lakini bado uchumi ukaanguka. Huyo samia asitafute kisingizio cha kukuza uchumi wakati hana uwezo wa kufanya hivyo kwa sababu alikuwemo kwenye Serikali ya dhalimu magufuli. Wasaliti kama wewe ni hasara kubwa kwa Taifa. Sasa hivi umeamua kuwa malaya wa kisiasa ili kufukuzia TEUZI!!


View attachment 1848600
duh!. hivi vijamaa bana..
 
Acha ujinga wewe!!!! Yule dhalimu kwa miaka mitano kazuia demokrasi nchini lakini bado uchumi ukaanguka. Huyo samia asitafute kisingizio cha kukuza uchumi wakati hana uwezo wa kufanya hivyo kwa sababu alikuwemo kwenye Serikali ya dhalimu magufuli. Wasaliti kama wewe ni hasara kubwa kwa Taifa. Sasa hivi umeamua kuwa malaya wa kisiasa ili kufukuzia TEUZI!!


View attachment 1848600
Asante sana kwa kumjibu huyu poyoyo
Anatafuta nini
Alipojiunga upinzani ilikuwa ni kwa lengo gani
Anaona au anafikiri WaTz ni wajinga
Kuna baadhi ya hawa wanasiasa uchwara wanatanguliza imani zao
Alipokuwa Magu hakuwahi kumuunga mkono sababu ni...
Leo chama cha kuponya nchi hakipo amejiunga na watesi

Ni hivi mtoa mada
Tunajua lengo na kusudi lako
Usiwagawanye WaTz kwa uhuni wako
Wenye chama muondoeni huyu hana la kuwasaidia
Tz ni ya Imani zote na wasio na imani sijui dini

Unajitahidi sana kutuma ujumbe but guess what ....umegundulika songa au ficha ujinga wako...


Ni sahihi kukosoa mapungufu na kuunga mafanikio
Sio wewe mwenye kuunga kila ulilolipinga kwa sababu ya imani ya mtu..
 
Shukurani sana. 🙏🏾

Asante sana kwa kumjibu huyu poyoyo
Anatafuta nini
Alipojiunga upinzani ilikuwa ni kwa lengo gani
Anaona au anafikiri WaTz ni wajinga
Kuna baadhi ya hawa wanasiasa uchwara wanatanguliza imani zao
Alipokuwa Magu hakuwahi kumuunga mkono sababu ni...
Leo chama cha kuponya nchi hakipo amejiunga na watesi

Ni hivi mtoa mada
Tunajua lengo na kusudi lako
Usiwagawanye WaTz kwa uhuni wako
Wenye chama muondoeni huyu hana la kuwasaidia
Tz ni ya Imani zote na wasio na imani sijui dini

Unajitahidi sana kutuma ujumbe but guess what ....umegundulika songa au ficha ujinga wako...


Ni sahihi kukosoa mapungufu na kuunga mafanikio
Sio wewe mwenye kuunga kila ulilolipinga kwa sababu ya imani ya mtu..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom