Uchumba unatakiwa usizidi muda gani?

Uchumba unatakiwa usizidi muda gani?

MUYOOL

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2012
Posts
561
Reaction score
446
Hi!

Wataalamu wanasema uchumba ukidumu kwa muda mrefu sana kabla ya ndoa basi unaweza kuvunjika hasa ukizingatia huu uchumba wa kuvunja amri ya sita.Pia wengine wanashauri uchumba usiwe wa muda mfupi sana kwani kuna hatari ya kuuziwa mbuzi kwenye gunia.

Je ni muda gani unafaa kuwa ktk uchumba?Hata Wanandoa karibuni kuchangia maana najua nyinyi mna experience za kutosha kwani kuna wengine mmepata na wengine wamepatikana.
 
Kwa nini kuwe na muda maalum wakati hamna uchumba maalum?

Kama kuna uchumba wa aina tofauti (dini, tamaduni etc) kwa nini kusiwe na mida tofauti ya kuchumbiana?

Unakusudia uchumba wa aina gani?

Unaweza kuuliza hivyo ukaambiwa "uchumba" wa "ndoa ya mkeka" hata dakika tano zinatosha.
 
Unaposema uchumba unamaanisha nini? Engagement? Kwa maana ya kiafrica (hereby meaning wenye utamaduni wa kulipa mahari) uchumba ni baada ya kuridhiana kwa mahari. Wenzetu wazungu ni baada ya ridhaa ya wazazi na kupena pete mostly. Sasa kama mmeshafikiria kuoana mnawekana kiporo juu ya nini? Mara shetani 'awajaribu' buree. As soon as you can buy the dress lol
 
Uchumba hasa ni baada ya kutoa posa ikakubalika na hapo unapangiwa mahari ili ukamilishe uchukue jiko lako. kwa utaratibu huo uchumba unapaswa uwe wa muda mfupi kwani hadi kwenda kutoa posa humaanisha tayari umeridhika naye.

Uchamba feki unakuja kwa vijana kuvishana pete bila hata kutoa posa, yaani wanakutana wenyewe wanapanga na kuvishana pete na kusema eti ni wachumba.
 
Kwa nini kuwe na muda maalum wakati hamna uchumba maalum?

Kama kuna uchumba wa aina tofauti (dini, tamaduni etc) kwa nini kusiwe na mida tofauti ya kuchumbiana?

Unakusudia uchumba wa aina gani?

Unaweza kuuliza hivyo ukaambiwa "uchumba" wa "ndoa ya mkeka" hata dakika tano zinatosha.

Mimi nadhani kuna baadhi ya wazazi hawakutimiza wajibu wao kwa vijana wao wakati wanakua AU kuna vijana hawakuwasikiliza wazazi wao walipokuwa wanafundishwa kuhusu urafiki, uchumba na ndoa.

UCHUMBA ni neno relative, especially kwa kizazi hiki cha sasa.

Ila kwa nilivyofundishwa ni kuwa urafiki unaweza kuwa as long as you want it, uchumba usizidi mwaka...ndoa! Vijana wengi siku hizi wanakimbilia kuchumbiana kwa ile notion ya, "kumuwahi" asijechukuliwa na mwingine. Which is - to me - a grave mistake.

Ndipo hapo mnaishia kupeana ultimatum za lini ndoa ifungwe nk nk. Otherwise, ingependeza sana wakati wa urafiki muutumie vyema kufahamiana, kuwajua marafiki zake, ndugu na hata wazazi - kama rafiki wa binti/kijana wao.

Ni hayo tu kwa leo...usisite kuniuliza zaidi.
 
Utapeli wa vijana wanaotaka kuchovya kwa gia ya uchumba mwingi, mtu anabeep kwa gia ya uchumba, anajibiwa, anajikuta hana la kusema.

Mara ooh, matatizo ya kifamilia. Mara ooh sijakaa sawa, uchumba mwaka wa saba unapita.

Mwishowe mtoto wa kwanza anazaliwa katika uchumba.

Kwanini tusiondoe ndoa kabisa na kuishi na uchumba wa milele? Think about how the challenge of wooing your everlasting fiancee everyday would spice things up.

Think about how the freedom of "no marriage, no divorce, you just walk out the door" would strengthen the relationship, or not hinder anyone from easily pursuing their other options.

Let's face it, "uchumba" mwingine tayari ni "common law marriage". Mtu mnakaa pamoja zaidi ya miaka miwili mnagegedana zaidi ya waliooana, halafu bado "mchumba" tu?
 
Unajua kuna uchumba ni neno nyeti sana na ni la kuheshimiwa mno. Mara nyingi huwa watu wanaanzia kwenye urafiki japo bado kwetu sisi huuita uchumba. Urafiki unapaswa kuwa wa muda kidogo yaani hii inategemea na geographical location. Sasa let say tukisema uchumba uwe wa miezi sita wakati huo huo hao wachumba watakua wameonana mara mbili tu ktk kipindi hicho cha six month , hii haiko sawa. Ni vema kupeana muda wa kutosha wa kufahamiana na kujuana , hii itakusaidia kujua tabia ya unaemuoa. Baada ya hapo sasa ndio mnapelekana kwa wazazi ikiwa tayari mmeridhiana kuoana na huu ndio unaitwa uchumba au mwanzo wa uchumba.
Madhara ya kukutana muda mfupi na kupelekana kwa wazazi tayari kwa maandalizi ya ndoa hii haijakaa vizuri, Japo zipo ndoa za aina hiyo zilizodumu. Hapa mtakua hamjafahamiana vizuri kwani ni kipindi kifupi sana mlichopeana cha kufahamiana na yeyote kati yenu anaweza kuwa na tabia za kupretend tu na si halisi. Sasa inakua vigumu kuzoeana mkiwa tayari kwenye ndoa manake unaweza ukakumbana na tabia ambazo hungependa kua na mtu wa type hiyo. Japo hata mkiwa na muda wa kutosha wa kufahamiana hautazijua tabia zote za mchumba wako lkn at least ziko tabia zisizofichika. Kwa mfano pengine ungependa kuwa na mchumba ambae ni thinker mzuri , sasa kama hamkukaa muda kidogo ni vigumu kujua kichwa cha mchumba wako, wako wanaoonekana smart sana kwa kuwatazama lkn kumbe kichwani sio smart na wewe hitaji lako ulifocus sana kwenye kichwa so ukiishi na mtu wa namna hii hautafurahi
 
kwa upande wangu uchumba ni pale unapokamilisha hatua kamili za kuitwa mchumba wa fulani ni kama vile kujitambulisha kwa binti na kuanza process zinazoitakiwa na kama haujafanya haya basi wewe si mchumba wa fulani.
Turudi kwenye mada hapa kuna vitu kama viwili kukaa muda mrefu siyo tatizo maana kuna mambo yanatojitokeza na kusababisha kutofikia leengo la ndoa kwa wakati muwafaka. Lakini pili ni vitu gani vinavyofanyika katika kipindi chenu cha uchumba hapa ni hii hali ya kukaa kama mke na mume hili nalo ni tatizo kidogo maana uwalali wa kuwa mke na mume unapotea kwani mnakuwa mmejihalalisha kuwa mke na mume kabla ya muda kufika. Ushauri kukaa muda mrefu kama wachumba hii haina formular inategemea makubaliano yenu kati ya watu wawili
 
Kama kweli mpo vizuri na mnajua mnachokifanya, kwa mtazamo wangu mwaka usizidi hamjafanya kweli
 
Mwenz mmoja tosha ukizid ni majanga

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Utapeli wa vijana wanaotaka kuchovya kwa gia ya uchumba mwingi, mtu anabeep kwa gia ya uchumba, anajibiwa, anajikuta hana la kusema.

Mara ooh, matatizo ya kifamilia. Mara ooh sijakaa sawa, uchumba mwaka wa saba unapita.

Mwishowe mtoto wa kwanza anazaliwa katika uchumba.

Kwanini tusiondoe ndoa kabisa na kuishi na uchumba wa milele? Think about how the challenge of wooing your everlasting fiancee everyday would spice things up.

Think about how the freedom of "no marriage, no divorce, you just walk out the door" would strengthen the relationship, or not hinder anyone from easily pursuing their other options.

Let's face it, "uchumba" mwingine tayari ni "common law marriage". Mtu mnakaa pamoja zaidi ya miaka miwili mnagegedana zaidi ya waliooana, halafu bado "mchumba" tu?
Tanzania inaitwa presumption of marriage hiyo..aiseee..!!!!
 
Maandalizi ya harusi 🙂...Si unajua harusi za Kibongo lazima michango ifanyike toka kwa ndugu, jamaa na marafiki ili kufanikisha harusi kubwa ya kutumia mamilioni, baada ya harusi maharusi wanaenda kuanza maisha kwenye chumba kimoja huku wakiwa wameunguza mamilioni kwa masaa machache tu kusherehekea ufungaji wa pingu za maisha....Inategemea na wahusika pia wengine uchumba wa miezi sita unatosha kabisa wengine watakwambia apewe nonino mpaka mimba ijibu kwamba binti kizazi chake kiko bomba hivyo jamaa hatanunua mbuzi akiwa kafungwa kwenye gunia.

Ni nini kinafanyika ndani ya huo mwaka?
 
Hapa wachangiaji wengi tupo kwenye style ya kizungu tu,
Tuzungumzie uchumba wetu wa kiafrica ambao wazee wetu walipitia,nina hakika enzi za wazee wetu hapakuwa na style hii ya uchumba mnakaa mnazaa,halafu mnakuja kuowana,
Wao walipoona flani anafaa kuwa mke au mume basi taratibu za wazee zilifuata bila kupoteza muda wala kugegedana kwanza, ndio sababu mpaka leo baadhi ya wazee wetu wengi bado wanaishi pamoja yaani mpaka wanazeeka pamoja,
Sisi wazungu wenye kujua kuchagua wenye kujua uchumba kumaliza miaka 2 kwenye ndoa mtihani,nadhani uchumba wa zamani ulikuwa ni bora zaidi ya sasa.
 
Sasahivi hakuna uchumba wala nini. Ni kudanganyana tu ndo kumeshika kasi ya ajabu. Muda wa kukaa ktk Uchumba unaishia pale ambapo kudanganyana huishia na si vinginevyo. Kama mmekubali kudanganyana niaka 5,7, au 10 danganyaneni tu.
 
Back
Top Bottom