Peter Mwaihola
JF-Expert Member
- Jun 23, 2022
- 227
- 333
Ni ukweli wala sio utani kwamba baadhi ya wanawake ambao bado hawajaolewa hawavutiwi tena na hatua ya uchumba kabla ya ndoa.
Utafiti mdogo uliofanyika unaonyesha kuwa wanawake wamechoshwa na uchumba sugu, kudanganywa na wanaume wanao ahidi kuwaoa kisha kutelekezwa baada ya muda fulani kupita.
Aidha wanawake wengi wanaona sulihisho la tatizo hili ni kukataa kukaa kwenye hatua ya uchumba kwa muda mrefu na wanaume wanaojitokeza kuwapenda ili kupunguza uwezekano wa kuachwa solemba.
Miongoni mwa wanawake walioguswa na utafiti huu wanasema hawawezi kuingia kwenye uhusiano na mwanaume ambae hana nia ya kuoa hivi karibuni.
"Kama mwanaume ananipenda basi anatakiwa aende nyumbani ajitambulishe kisha afuate taratibu atakazoambiwa ili anione" anasema Taji ambaye ni mwanafunzi wa shahada ya sheria moja ya chuo kikuu nchini Tanzania.
Anasema wanaume wengi wamekuwa waongo kwa wanaweke wengine huwazalisha na kutokomea kusiko julikana na kukwamisha ndoto za wanaweke.
Hata hivyo wanaume nao wana msimamo wao kuwa hawawezi kuoa mwanamke wasiyemjua vizuri tabia, na mwenendo hivyo ni vema kupitia hatua ya uchumba kabla ya ndoa ili kupata muda wa kumsoma vizuri na kujua namna ya kuishi nae katika ndoa.
Aidha wanaume wanaeleza kuwa baadhi ya wanawake hatawataki uchumba kwa sababu ya tabia zao mbaya ili zisiijulikane mapema hivyo wanatafuta mwanaume atakae waoa kwa haraka bila kuwachunguza jambo ambalo ni kama kuuziwa mbuzi kwenye gunia.
Sababu nyingine zilizobainika kupelekea baadhi wanawake kutotaka uchumba ni kuepusha shinikizo la wazazi na jamii katika kuvuruga uhusiano wa wahusika kabla ya kufikia ndoa.
Je wewe una mtazamo gani kuhusu kuingia kwenye uchumba kabla ya ndoa?.
(Imeandikwa na Peter Mwaihola)