Uchumba unapogeuzwa pango la ngono........!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchumba unapogeuzwa pango la ngono........!!!!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Sep 27, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Sep 27, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mpaka miaka ya hivi karibuni mambo ya uchumba yalikuwa hayawezi kufanyika bila ya kuwepo wazazi na familia. Mitoko mingi na kualikana ilifanyika majumbani wakiwapo wanafamilia wote. Kujitokeza kwa usafiri na ugunduzi wa magari kumesaidia sana kuharibu utaratibu mzuri wa mitoko ya kimapenzi na uchumba kwa ujumla.

  Magari si tu kwamba yamesababisha mitoko isifanyike majumbani, lakini pia yamesababisha ifanyike bila kuwashirikisha wazazi. Gari siku hizi limebadilishwa kuwa kitanda kinachotembea chakufanyia ngono wakati wa mitoko.Vijana wadogo sio kwa hapa nchini tu bali hata huko katika nchi za magharibi na ulaya wamejinyakulia uhuru mkubwa mno kutoka kwa wazazi wao, na kuzipondoponda chini mila na desturi ambazo ziliweka misingi imara katika kulinda maadili ya uchumba kwa vijana.

  Lakini pia Teknolojia mpya na matumizi yake mabaya nayo imechangia kwa kiasi kikubwa kusambaratisha mila na desturi zetu zilizokuwa zikilinda maadili yetu. Simu na mitandao ya mawasilano, ni moja ya mabadiliko yaliyotufikisha hapa.

  Imani na misingi ya kidini zilianza kupata mashambulizi makali toka kwa wasomi na wanafalsafa wa karne na karne. Charles Darwin na wafuasi wake walianza mashambulizi dhidi ya imani ya Mungu na mamlaka yake. Na hii ilipelekea wanatheolojia wa Ulaya kuanza kulegeza kamba kwa mambo muhimu ya kidini.Kupuuzwa kwa mila na desturi na maadili ya kidini kumechangia sana kuharibu tabia za vijana ikiwa ni pamoja na mambo ya urafiki, uchumba hadi ndoa.

  Ni baada ya vita ya kwanza ya Dunia ndipo saikolojia na Sosholojia vilileta njia ya Kisayansi iliyoheshimika zaidi, nakuanzia hapo mamilioni ya watu walianza kuamini mafundisho ya akina Sigmund Freud, Margaret Mead na Alfred Charles Kinsey.
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  sijakuelewa bana
   
 3. Tegelezeni

  Tegelezeni JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2011
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 268
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama wewe hujajitambua huwezi kuelewa..............
   
 4. Tegelezeni

  Tegelezeni JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2011
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 268
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Zamani wakati sisi tulikuwa tunakesha kuwavizia watoto wa kike vichochoroni, lakini vijana wa siku hizi wamerahisishiwa sana, mitandao ya simu na hii ya Intenet imepelekea swala la kutongozana kuwa rahisi. Usafiri nao, kama ulivyosema ni sana na Vitanda vinavyotembea...............mara nyingi vijana hufanyia ngono kwenye magari ya wazazi wao. mzazi anapoombwa gari na mwanae kwa ajili ya kwendea Disco, basi ajue litatumika kwa shughuli nyingine, yaani kufanyia ngono.

  Maadili ya kumpata mwenza yamewekwa kisasa zaidi, zile taratibu za kuchunguza familia atokako mke au mume, kwa ajili ya kujiridhisha kama binti anaolewa katika familia sahihi, au mume anaoa katika familia sahihi, hazipo na badala yake watu tunachukuana tu, na ndio maana ndoa hazidumu, watoto hawana adabu, kutoka nje ya ndoa kusiko na simile, na kila aina ya uchafu, ili mradi fujo tu...............
   
 5. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ni sahihi kabisa kila kitu kimeathiriwa na utandawazi si masuala ya mahusiano pekee. Enzi za zamani ilikuwa mpaka siku ya harusi ndiyo wanandoa wanado lakini siku hizi mpaka bibi harusi aidha atoe mimba au afunge akiwa mjazito lakini hili si kwa wote wajameni. Hilo tu ni kiashiria tosha kuwa mambo yamebadilika sana na hata ukienda katika mambo mengine ya kijamii maadili yameshuka vibaya mno.
   
 6. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #6
  Sep 27, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Umenikumbusha zile ndoa za KISARAWANDA................
   
 7. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  kumekucha!!!
   
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Sep 27, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Vipi tena Feis Buku...........
   
 9. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,500
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Hii ni Kweli kabisa mtambuzi manake kuna kipindi wakati naishi pale mabibo hostel, kulikuwa na gari katika angalia yangu vizuri nikaanza kushangaa gari (lilikuwa tinted hivyo huoni ndani) linanesanesa yaani juu chini, juu chini mwanzo mwisho na baada ya kama nusu saa akatoka dada na pande la mtu "libaba" na kama haitoshi hapo wakakumbatiana na kula denda. Nikahisi tu hawa watu walikuwa wana.........
   
 10. v

  valid statement JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  huyo dem alijishushia heshima ivo?dah huyo ni cheapest not cheap.
   
 11. mojoki

  mojoki JF-Expert Member

  #11
  Sep 27, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 1,333
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  mbona hamjisemi nyie wazee wa zamani kwamba siku hizi mmebadilika sana na ndo mnaongoza kwa kutembea na mabinti wadogo kama watoto wenu wa kuwazaa...hii teknologia imemuharibu kila mtu sio babu sio mjukuu
   
 12. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #12
  Sep 27, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  unasemaaaaaaaaaaaa
   
 13. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #13
  Sep 27, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Wanasayansi wanakwambia 'sex ni basic need'. Sasa unategemea nini kwa hawa watu walioipokea hii idea?? Kamwe hawawezi ishi maisha ya nyuma!
   
Loading...