Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,589
- 1,679
Habari zinazotembea hivi sasa ni kuwa punde hivi Uchina itaiomba Tanzania (kama bado haijafanya hivyo) iwapatie kituo cha kijeshi (military base). Kama ilivyoomba nchi kadhaa ikiwemo UAE, Pakistan, Tajikistan (UAE imekwishawapa).
Najua ombi hilo likifika Tanzania kuna wale watakaosema 'lakini siasa ya Tanzania ni kutofungamana na kokote!' Au, 'wajua sisi Tanzania ni nchi ya amani' au 'mbona hiyo itatuletea matatizo'na mambo mengi yanayoonesha ugandaji wa fikra za karne ya 20.
Zama zimeendelea mbele na hivi sasa kuna uhalisia mpya. Ukitazama jinsi mataifa yanavyofukuzana kushindana katika kutengeneza na kulimbikiza silaha, utajua kuwa it is a matter of time, kabla ya vita kuu ya dunia 3 kutinga. Katika vita kama hiyo hakuna atakayejali kuwa Tanzania ni 'nchi isiyofungamana na dola lolote'.
Linalotakikana sasa ni kuwa 'pragmatic' na kukubali ombi la nchi hii ambayo tayari ni namba 1 katika mambo mengi isipokuwa machache tu ambayo Marekani bado inaongoza (utengezaji wa ndege za abiria/kivita, nano technology, AI...).
Ni vizuri kuwa juu ya mgongo wa ndovu wakati chui anashambulia kuliko kuwa unatembea kwa miguu.
Kuna saikolojia inayomfanya mwingine aone anaweza kukuamini pindi unapokuwa tayari kumsaidia wakati wa dhiki, kuliko wakati tayari amepata ofa nyingine.
Faida za kuwepo military base Tanzania zitakuwa nyingi ikiwemo kupata ujuzi wa vyombo vya kisasa na pengine kuanzisha viwanda vya kutengeneza silaha za kisasa. Ili mradi tu mkataba utakaoingiwa uwe unatazama maslahi mapana ya Tanzania.