Ucheshi walionao Wapishi wa mahotelini, kweli wanaipenda hiyo kazi kiasi hicho?

Msukuma Msomi

Senior Member
Feb 6, 2017
173
149
Kila nikiwa Hotelini, either nimeenda mkoani kikazi...basi nitakaa wiki 2 au mwezi, moja kati ya maajabu ambayo huwa nakutana nayo ni Wapishi wa jikoni na Wahudumu wa Bar/Restaurant ya hapo hotelini: Wamejaa tabasamu, wamechangamka, ukienda Restaurant kuweka oda...nisipokuta mtu basi nafungua mlango wa jikoni, nawakkuta kinadada/kinamama/kina kaka wanapiga stori na kucheka kwa furaha....

Kwakweli huwa ninawaonea wivu sana, natamani na mimi ningekuwa mcheshi hivyo au mwenye furaha muda wote kwenye kazi yangu (sio kwamba sina furaha, nafurahia maisha yangu, lakini si kwa kiwango ambacho hawa watu wanatreat wateja....na hata ukikaa muda mrefu ukazoeleka, bado mdundo wa haiba yao ni ule ule).

Je, ni wao naturally au wanafeki? maana wengi mishahara yao ni chini ya laki 3 au 5, aki mi nisingeshinda natabasamu vile. Au wamekuwa trained? ipo kwenye mikataba yao ya kazi kwamba wawe friendly 24/7 kazini?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom