Jipe moyo mkuu, tutatoka tu ipo siku!Kuzaliwa Mwafrika ni kazi sana yaani...
Jipe moyo mkuu, tutatoka tu ipo siku!Kuzaliwa Mwafrika ni kazi sana yaani...
We unaongelea kula tu hilo mbona kubwa kuna mwingine ye hata akikuona ni mzima unapumua inamkera anatamani utoweke tu duniani na hana sababu kwanini anakuchukia.Dah ila umasikini shida sana ......sasa unaniroga kisa nakula biriani la mariamu
Tudokeze ilikuwaje hili na wengine wapate funzoHii kitu ilishanitokea nilitapika sana mpaka nikaishiwa nguvu
Sawa yawezekana uko sahihi ila hujaja na point yakutetea hoja yako njoo na point tujue ni kweli unchokisema au la!!jipige kifua huku ukisema maneno haya "mimi ni mpumbavu"
Ni kweli tahadhari ni muhimu, sasa utatambuaje ikitokea bahati mbaya kichanga wako kalogwa, dalili ni zipi?Kama mama kajifungua, wanaokupa kumsalimia yeye na mtoto wengi sio wazuri, kabla ya kumpa mtoto amshike unasema kwa sauti ila kwa utani "usimloge mtoto" hapo umeshashamloga mwenye nia mbaya. Hakika uchawi upo, muwe macho. Siku hizi hata watoto wanaloga.
Uchawi balaa, hiyo rekodi iliandikwa pande za wapi?Jamaa alikazia macho mkungu wa ndizi ukakatika kama mtu aliyekata kwa panga. Macho yaliyoangusha mkungu wa ndizi binadamu vipi? Uchawi upo!
Ugonjwa gani unaousemea wewe? Zongo au?Mimi pia nasubri tiba ya huu ugonjwa Kuna ndugu yangu anasumbuliwa
Ahsante kwa kutuongezea maarifa mengine ya namna ya kuepa mabalaa.Noma sana na Kuna Ile kama unakula ugenini unabebanisha mguu mmoja hivi unakula mpaka unamaliza unaenda zako na Kuna kutanguliza Jina la Yesu Yesu Huwa ashindwi na chochote
Papaaa mukuubwaaa Nina ndugu yefu ni Kama amerogwa au kufungwa akili, nakuja pm ili tukajaribu hukooNAMNUKUU MWANA JF MMOJA
Nyumba ya mganga na nyumba ya Chifu haipungukiwi ni msemo wa wazee huo. Umemtibu mtu analeta shukrani kwa alichofanikiwa.
Sifa za Mganga wa kweli.
Mganga wa kweli hakutozi hela nyingi kuliko alivyopangiwa na mizimu iliyompa uganga maana uganga wa kweli lengo lake ni kusaidia jamii, unganga ni jadi na lengo lake ni kuisaidia jamii toka enzi na enzi ni bahati mbaya sana kuufanya uganga kuwa dili la kuwaibia watu, hii sio lengo la uganga kwa asili yake.
Uganga wa kweli mara nyingi ni ule unaotokana na kurithi toka kizazi mpaka kizazi sio ule wa kujifunza,ukanjanja, udii na ulozi wa kuwatupia watu mabalaa kwa lengo la waje uwatibu.
Mganga wa kweli lazima atakukurahishishia shida ulionayo na kama imemzidi uganga atakwambia au atakuposti kwa wajuaji zaidi wa shida yako (Waganga wanafahamiana kwa uwezo na nyanja kama walivyo walozi).
Mganga wa kweli atakutibu ili upone ndo akufaidi zaidi kwa shukrani na zawadi na uaminifu wako kwake na ndio faida ya uganga wa kweli. Huyu mganga hutamwacha kamwe kwenye kulingana na alivyotatua shida yako. Kuna jangiri alijeruhiwa na nyati porini nyati alivunja vunja miguu, yule mwamba wenzie walimbeba mpaka kijiji cha jirani huko Katavi kwa mganga. Mganga akawaambia wale wenzake mje mumchukue baada ya wiki tatu muache debe moja la unga. Wenzie waliporudi baada ya wiki 3 walikuta anatembelea fimbo na akapona mifupa na akarudi kwenye ujangiri wake na akipata mnyama lazima apeleke nyama kwa Mganga.
Onyo: Nazungumzia waganga wa kweli sio matapeli wa mjini na mapropesa.
Watu wanaibiwa na wanachanganya sana kati ya Ulozi, Ugagula, Uganga na Mazingaombwe, kiini macho.
MIMI NAANDIKA NA NINA MGANGA WA UHAKIKA
Kama mtu anataka mganga wa uhakika mganga wa Tanga aje pm ilaa aandae kunitumia 5000 Kwa akili ya connection.
Alisikika m Tanzania mmoja akisema Vibora vinagharama Quality is Expensive kama hutaki unataka cheap chukua ya kwenye nguzo utapeliwe.
Nikimtapeli mtu anireport nipigie life ban
Karibuni PM/DM
watu wanaamini uganga hausaidii watu asikudanganye mtu waganga uzunguni ni matajiri sana kama unataka uamini
Ingia TikTok Kuna jamaaa anaitwa DANIEL MACDONALD anaulizaga wazungu matajiri what do you do for a living wengi ni waganga na wale dream tellers watafsiri wa ndoto na conclude
SawaPapaaa mukuubwaaa Nina ndugu yefu ni Kama amerogwa au kufungwa akili, nakuja pm ili tukajaribu hukoo
Kama ni tabibu mzuri na ndugu atapona maana kafikia hali mbaya, Basi nitakupa zawadi nzuri ndugu yangu.[emoji120][emoji120]
Mkuu nimempigia kasema yupo bize kwa sasa, labda nimtafute juma 5Sawa
Namna gani mtu avunje uchawi unaomsumbua maishani? Nitafurahi nikipata jibu lako.Uchawi wa macho a.k.a Evil eye ni aina ya uchawi unaotupiwa muhusika ukuue au kukutaabisha kupitia jicho la mchawi.
Mara nyingi uchawi huu ufanyika katika maeneo yenye umati mkubwa wa watu mfano magengeni, mikahawani, minadani, n.k
Uchawi huu ni Kijicho kwa maana ya wivu wa kichawi na roho mbaya kwa mtu asiye na hatia.
Unapokuwa ukila chakula na mchawi akakubaini kuwa unakula mbele yake ni kana kwamba unamtambia najua wewe uwezi nunua ndiyo maana wanitolea macho ebu angalia ninavyofaidi.
Sasa kukukomesha mchawi unuia kimoyomoyo kwa kunung'unika na ukukazia macho yake "ambayo ukiyatizama nikama yanakwambia nakuchukia kama kifo au kufa tu" papo hapo uchawi huu utoka ndani yake na kumdhuru yule aliyekusudiwa.
Zongo hili umkumba mchawi aliyeununua au mwenye kuumiliki kama vile arosto ya madawa ya kulevya mara anapoona mazingira ya uchawi wake hawezi jizuia kukuroga hata kama ni mwanaye wa kumzaa.
Pindi unaporogwa na haina hii ya uchawi uwezi chukua round ni dakika chache tu baada ya kumaliza kula, kunywa au kumeza funda la mate tiyari utaanza kuhisi hauko sawa, tumbo litakuuma mno au kuvurugika hapo hapo utahisi homa, kichefuchefu na ukiwa na bahati nzuri utatapika.
Kinachofuata hapo kama utakimbizwa hospitalini hakuna watakachobaini na badala yake itatuchukua masaa kadhaa tu ya siku au siku chache kukusahau kama uliwahi kuwepo.
UNAJILINDA VIPI
1. Kama wewe si mshirikina chukua tahadhari acha mazoea ya kula ovyo ovyo mbele za watu usiowafahamu au kwenye umati mkubwa.
2. Dadisi au tafuta taarifa toka kwa wenyeji wa maeneo husika ulipofikia juu ya tabia za kishirikina katika maeneo yao hasa ukiwa maeneo ya vijijini ambapo kwa asilimia kubwa uchawi huu umeenea.
3. Tembea na kijiwe kidogo mfukoni au ukiweke katika sikio lako la upande mmoja kama wanavyoegeshea penseli mafundi seremala, hii ni kinga dhidi ya uchawi huu.
4. Chomeka njiti moja au mbili za kuchokonolea meno (toothpick) katika nywele zako za kichwani kwa wale wenye nywele ndefu hakikisha haionekani, hii pia itakusaidia ukirushiwa uchawi huu wakati unafakamia msosi au kinywaji usidhurike.
5. Hakikisha kila unapokula hasa mgahawani tafuta sehemu inayokupa faragha kiasi cha kutoangaliwa sana na wapita njia.
6. Ukishajua unakula katika mazingira ambayo ni hatarishi, usikwepeshe macho au kuona aibu kuwasoma watu unaokula nao au wanaokutazama, mara kwa mara wakazie macho na wao wakikutazama hili hata kama ipo nia atapotezea atajua mlengwa ana machale au kishashtukia mchezo na nikimroga hapa atanijazia nzi.
7. Usimpe nafasi uliyebaini au kumuhisi ndiye kakuroga nafasi atoroke, muumbue na hamasisha watu walio karibu wamdhibiti asitoroke hata kama huna uwakika kumbuka wapo watakaokuja kumtetea watatoa na nondo za muhusika kuwa innocent na wengine wataenda mbali kiasi cha kukutajia muhusika (kumbuka wenyeji wanawajua fika wahusika isipokuwa wewe hapo uliyefika katika mazingira yao)
Ikitokea ukamfumbia macho mwanga utakufa wewe na kesho ataendelea kuua wengine, ila ukimtaitisha papo hapo, basi utapata msaada kwa wenyeji kumlazimisha akukorogee uji wa mahindi wa moto kwa kutumia mkono wake kama mwiko (hapo ndipo utajua kuwa uchawi upo)
Akishamaliza kuukoroga uji huo hapo hapo katika eneo la tukio utapewa unywe na baada ya sekunde tu utatapika vyote ulivyokula na ndiyo pona pona yako hiyo.
Kitakachokushangaza ni kuwa kile ulichokula pengine ni ugali na samaki, ulimtafuna minofu kabla ya kummeza ila hapa utamtapika mzima kabisa na ameoza ananuka balaa na ana funza wakutosha, itoshe kusema uchawi haufai na unatesa watu.
Uchawi huu umeenea sana maeneo ya kanda ya ziwa kule ukerewe na rorya na kaskazini huko uchagani, tanga na maeneo mengi tu hapa nchini, kikubwa nimekusanua tu hili uchukue tahadhari haijalishi unaamini au hauamini kama uchawi upo.