Uchawi upo, usidanganywe

Ahsante, na wewe umeshautaja uchawi!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, story nliyoandika mimi sio hearsay, ni habari ya kweli nliyoshuhudia kwa macho

Mkuu nilikua sijsoma story yako nikiamini, kama story zingine zote za uchawi, huwa zinaacha loopholes and surely enough yako pia was no exception to this. Kwanza ni kawaida kwa waganga wa jadi kusema mbaya wako ni jirani yako au ndugu yako kama hujui hili hadi leo basi siwezi kushangaa kwanini unaamini uchawi upo.

Pili, kuuwawa na tembo au wanyama maeneo ya karibu na mbugani ni jambo la kawaida, sawa na mtu wa mjini kugongwa na gari. Nadiriki kusema ilikua coincidence tu na pengine huyo mtu asingekufa mganga angekuja na sababu zingine kama kawaida yao.

Nitakupa kisa kidogo, Juma alimwambia Obedi leo usiku utanikoma baada ya kukorofishana, Obedi usiku ule aligongwa na gari na kufariki pale pale unadhani Juma ni mchawi? Kwanini isiwe conicidence? Unaweza muongelea mtu mabaya bila kumaanisha na jambo baya likampata ila hiyo sio ithibati ya kuonyesha wewe ni mchawi.

Hizi ndo kasoro za story za uchawi, ni story za hearsay na mara nyingi zina loopholes ambazo watu hukimbilia kusema ni uchawi wakati zinaweza kujibika kwa njia zingine.

HAKUNA UCHAWI.
 
Wewe nakushusha ngiri kwanza halafu nakunyoa nywele huko huko uliko ili ujue uchawi upo.
Utatuambia mwenyewe na kuomba msamaha
 
Wewe nakushusha ngiri kwanza halafu nakunyoa nywele huko huko uliko ili ujue uchawi upo.
Utatuambia mwenyewe na kuomba msamaha

Tafadhali fanya hivyo, nikupe hadi lini?
 
Made in Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wao ndio walitega mtego na hii INA maana walienda pata feedback kwa mtega Bomu.naunganisha sentensi tu.
 
Nimegundua uhusiano wa tembo na kinyesi kilichotumika kwa mganga..huenda kingetumika cha simba angeuliwa na simba,, aya bna,, pia mtoa mada ni 30+ aged
 
Kukimbilia kujibu na hujasoma inadhihirisha loophole mahali fulani upstairs.
Hivi unajua hata Isack Newton hakwenda kukaa chini ya ule mti wa Apple akiwa kwenye research ya gravitational force? Ilikuwa coincidence tu, kama unavyoamini wewe. Lakini haiondoi ukweli kwamba alichogundua kinathibitika. Unadhani hakuna mtu aliyekuwa amewahi kuona kitu kinaanguka kutoka juu kwenda chini na kisirudi juu? Pengine waliamini ni coincidence kama unavyoamini wewe..
 
Huoni aibu kujibu story za kusadikika kwa mifano hai inayothibitika. Leo Kuna ndege, rockets nk kwa kutumia gravitational force, uchawi zaidi ya story za kitoto za kusimuliana vitu visivyomake any sense hauthibitiki.

Mtu kauwawa na tembo mbugani cha ajabu nini hapo au ulitaka agongwe na meli Serengeti! Badala useme mganga aliwapiga hela kumbe wewe pamoja na kukua akili imeganda pale pale.

Waafrika kuendelea bado sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahahah! Umejibu vyema, Leo kuna ndege na rocket kwa coincidence ya apple kuanguka kutoka juu kwenda chini. Lakini pia leo yule jamaa hayupo kwa coincidence ya yule tembo. OVA
 
Hahahahah! Umejibu vyema, Leo kuna ndege na rocket kwa coincidence ya apple kuanguka kutoka juu kwenda chini. Lakini pia leo yule jamaa hayupo kwa coincidence ya yule tembo. OVA
Ndege bado zinaruka vp huyo mganga wako bado anaua watu kwa tembo? Anaweza niua mimi nikiwa posta kwa tembo? Hata kama sio huyo unaweza tafuta mganga yoyote aniue kwa njia yoyote ya kichawi. Huwa mkifika hapa mnaruka mita laki

Nimejaribu sana kurogwa bila mafanikio.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, kwanza sijasema mahali popote kuwa mimi ni mchawi. Nimekusimulia kisa nlichoshuhudia 18yrs back. Ila pamoja na yote hayo hata kama ningekuwa mchawi nisingeweza kukuthibitishia kwa njia rahisi unayoitaka wewe. Hivi kwa kuamini sayansi, wewe leo unaweza kutengeneza rocket au ndege? Si unatumia zilizopo kama uthibitisho wake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…