Uchawi upo, usidanganywe


Hazithibitishi chochote na kama ilivyo kawaida ya story za uchawi zote huwa ni hearsay, kama hiyo number moja, inawezekana huyo mzee mgeni kijijini, kama nyie, aliambiwa kwamba huyo mzee wa hapo ni mchawi sana.

Hiyo number mbili labda mwizi ana ustahimilivu mkubwa wa maumivu kama walivyo wezi wengi au pengine mwizi aliumizwa na magongo hayo mabua yalikuja kukamilisha kazi tu au labda kuna more into the story ambayo wewe kwa kujua au kutojua hukuona/hujaandika ukizingatia unasema mlikua mnageuza shingo kwa kuogopa kuona kipigo.

Story za kusadikika za uchawi zina trait moja sawia; zote huwa ni story za hearsay na hazithibitiki hata siku moja.
 
Mkuu, story nliyoandika mimi sio hearsay, ni habari ya kweli nliyoshuhudia kwa macho
 
Story za uchawi, ushirikina, wanga na ulozi ni story za kusadikika zinazoaminiwa na wavivu wa kufikiri.
Story ndio zinaaminiwa na wavivu wa kufikiri, Nlichokiona kwa macho pengine ungekiona leo ungekuwa kwenye kundi hilo(la wavivu wa kufikiri)
 
Jomoni. Nipeni address au contact za mganga mmoja wa ukweli. Nimevunjiwa nyumba yangu. Nataka kuanza na dereva wa tingatinga. Boss wake na aliyetoa oda.
 
Ulivyotaja KUMWIKA S/Msingi umenikumbusha M/Mkuu aliyemfata Mwl.OBOGO anaitwa Mwl.MASHEBE wa hiyo shule alikuwa akipiga bakora za MOJA MZINGA au MBILI REJAREJA.
 
Ulivyotaja KUMWIKA S/Msingi umenikumbusha M/Mkuu aliyemfata Mwl.OBOGO anaitwa Mwl.MASHEBE wa hiyo shule alikuwa akipiga bakora za MOJA MZINGA au MBILI REJAREJA.
Hahah! Namkumbuka Obogo alikuwa anakaa kule Muriba... Na mwalimu Sererya, kina Meng'anyi. Duh! Kitambo.
 
Bahati mbaya mambo ya kiroho hayaelezeki kwa maneno...unapewa picha tu ila huwez kuelewa moja kwa moja mpk ushiriki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
duuuhh mkuu, hata mjin tembo anaweza kufika??!

*I shall kindly Knee to leave my Pride*
 
Pengine uko sahihi mkuu siwezi kukupinga. Ila uzuri nimejitahidi sana kuelezea kwa kadri nilivyoweza kwenye post hiyo. Bahati nzuri nimeishi kotekote mjini na kijijini, ushuani na kwenye mbavu za mbwa. Hivyo nina uzoefu kwenye maeneo yote hayo.
 
Kweli uchawi upo
mimi mdogo wangu wa kike aliingia ndani kulala yeye na kabinti kengine walikuwa wanalala chumba kimoja..
Tulikuwa wengi hapo nje tunapiga stori baada ya kumaliza kula chakula cha usiku, wazazi pia walikuwepo hapo nje.
Ajabu dada yangu mkubwa kuingia ndani ya chumba kile alikuwa na shida HAKUMUONA mdogo wetu huyo kitandani ila mwenzie alikuwepo.. ndio akaleta taarifa huku nje na kuuliza kama amelala chumba kingine mule ndani..
Tukajua mzaha ktk kumtafuta kweli akawa haonekani.. Mwenzie akaamka akasema wameingia wote ndani na kweli kwa macho yetu wote tulishuhudia wakienda ndani kulala.
Tukatafuta vyumba vyote hadi uvunguni hakuna mtu.. Akina mama wakaanza kulia wakijua mtoto amepotea.. Ikabidi tumfate balozi akaja tukatafuta nae bila mafanikio.
Wakafatwa ndugu wa karibu usiku huo wakaja tukamulika pande zote huko nje hakuna..
BASI jamaa 1 akatoa wazo la kufungua chumba cha kuku na bata ambacho huwa kinawekwa kufuri mapema tu.. AJABU akakutwa mtoto huyo ameinama style ya kuswali kiislam.
 
Wengine tunaamini uchawi wa mabarabara, mifereji iliyofunikwa, treni zinazoenda sambamba na UDA, huduma za afya bora, ustawi wa jamii kwa yatima, wazee na watoto, elimu bora, kazi na uchumi bora, huu ndio uchawi..
 
Tulipomwamsha akawa amezubaa kama alikuwa mbali tena usingizini...
Watu hatukuamini sababu kile chumba nicha nje tena cha mifugo na kilikuwa na kufuri . Lakini ndimo tulifungua tukamkuta ktk hali ya ajabu sana.
Kuna maoni kabla mtoto hajapatika eti tukaripoti polisi usiku huo huku wengine tuendelee kumtafuta.. Hakuna ambae alikuwa anahitaji kulala bila kumpata mtoto huyo kwani tuliamini tukilala bila kumpata basi hatutamuona tena na kama ni nguvu za giza basi watakuwa wamefanikiwa kirahisi.
Baada ya kumpata tukalala kukacha .. Ndipo Kesho yake watu wakaja kwa wingi kumjulia hali anaendeleaje na yukoje.. kwa kweli hakuwa nafuraha alikuwa amepooza sana sio mchangamfu.
Baadae wazazi walienda kwa mganga IKAJULIKANA kuna mzee mmoja wa tena ndugu alitaka KUMBEBA KICHAWI mtoto yule.
Basi toka hapo mtoto yule alianza kuugua.. alisumbuka sana kwa waganga miaka mingi hadi ilifikia akawa anakimbia kama anataka kuwa mwehu.. mara majini.. mara azirai.
 
Aliteseka sana hadi kuna madarasa aliyasoma mara mbili kutokana na kuchukua muda mwingi kwa waganga wa kienyeji.. Alipofika secondary hali yake pia ilikuwa ya kubadilika mara iwe sawa mara awe mgonjwa tena.
Kuna muda alikuwa hawezi kuona maandishi ubaoni , akapimwa na akapewa miwani ya kusomea.. Anadai kuna muda alikuwa anawaona hadi wachawi wanaokuja usiku kuwanga.. Tena anawataja kwa majina na walikuwa wanamuogopa sjui tu walimfanyaje mtoto huyo akawa anawaongelesha kwa kuwatukana usiku huo hadi mnashangaa.
Kwa ufupi alipata mganga mwingine akiwa amemaliza elimu ya secondary ndie alimsaidia akapona kabisa hadi leo.. Yupo ni mzima japo hakupata post nzuri kwenye mtihani wake wa kidato cha 4.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…