Uchawi- Mtwara Mjini

ndugu yangu inaonesha hata mimi nikikujua naweza nikakuwasha,hao ndio wanaitwa WASHAWASHA,kuna njia nyingi za kumuua paka,hapo ukweli hakuna ni zengwe tu,stuka! Nalog off

Duh we ni m-bishi kama tomaso wa Yesu, sasa hapo zengwe linakuaje mkuu wakati watu wanaaibika? na inakuaje huyo waziri wa kikwete akapiga mkwara wasiende kijijini kwao??
 
Hao wasanii tu hawana lolote, wanatengeneza jina wapate wateja au umesahau yale ya Dk. Manyaunyau wa Gongola mboto sasa anamiliki MaDCM kibao ya Gongolamboto Posta

Ndugu watu wa msumbiji unawajua kweli wewe?? Hao ndo kila kitu
, kwa sababu ukileta masihala wanakuua man.
 
Hawa jamaa huwa wanaitwaga...yaani mnakaa kikao wananchi mnaamua kuwaita kwa kibali cha serikali(nasikia kikwete kawaruhusu), halafu inabidi mupate kibali cha watendaji wa kijiji...sasa hapa ndipo kuna kikwazo,(hawa jamaa mara nyingi wanakataaga, mpaka muwatishie kuwaua ndio wanatoa kibali). So nadhani ndio hivyo:spy:

Wanahitajika huku kanda ya kaskazini sana
 
Uchawi wa maendeleo ni kitu cha kawaida hasa nchi zilizoendelea za ulaya ila hakizungumzwi hadharani kama ilivyo ngono ila ukija kwetu huku sasa..ni balaa kabisaaa watu hawataki kusikia kitu kinachoitwa uchawi wala ngono lakini watu wanateswa na uchawi na wanawake wanashika mimba zisizotarajiwa ikiashiria kuwa ngono inafanyika mtindo mmoja.
 
pepo hazina sifa ila pawapo jehanam,kipimo cha uzuri ni ubaya.mchawi hawezi kumuumbua mchawi.ila watu wanaomtii mungu pekee ndo wawezao.
 
Uchawi wa maendeleo ni kitu cha kawaida hasa nchi zilizoendelea za ulaya ila hakizungumzwi hadharani kama ilivyo ngono ila ukija kwetu huku sasa..ni balaa kabisaaa watu hawataki kusikia kitu kinachoitwa uchawi wala ngono lakini watu wanateswa na uchawi na wanawake wanashika mimba zisizotarajiwa ikiashiria kuwa ngono inafanyika mtindo mmoja.

Umemaliza kila kitu...no comment, cha ajabu sehemu zote zenye haya mambo hazina maendeleo.
 
Fanya hivyo kwn watu wamewamaliza wenzio kiujanja Kamanda we fanya nao mahojiano ujuwe na utujuze!

Nasikia hata ile ajali mbaya ya machame iliyohusisha lori la nyanya ilipangwa na watu...duh balaa sana hapa tanzania.
Nikifanikiwa nitakujuza kamanda, bt no guarantee, kwa sababu hao watu mi mwenyewe nawaogopa kinoma...bwibwiiii
 
Mtwara wachawi two week ago nilikua huko........ zile meli zinazoondoka siku nzima zimejaa crude oil nilizikubali........ ni uchawi wa hali ya juu.... meli kuondoka zimejaa crude oil, na serikali haioni? Na mbaya zaidi wale wazungu wanaishi Dar Es Salaam, mchana saa 7 wanaletwa Dar kula hadi saa tisa na saa kumi mbili wanarudi Dar kulala. Wadada wa SAUT, UTUMISHI etc ndio viburudisho kwenye meli kwa 200,000/=. Kweli Mtwara wachawi............... Niliambiwa wakati wa korosho ndio kbs..........
 
mtwara wachawi two week ago nilikua huko........ Zile meli zinazoondoka siku nzima zimejaa crude oil nilizikubali........ Ni uchawi wa hali ya juu.... Meli kuondoka zimejaa crude oil, na serikali haioni? Na mbaya zaidi wale wazungu wanaishi dar es salaam, mchana saa 7 wanaletwa dar kula hadi saa tisa na saa kumi mbili wanarudi dar kulala. Wadada wa saut, utumishi etc ndio viburudisho kwenye meli kwa 200,000/=. Kweli mtwara wachawi............... Niliambiwa wakati wa korosho ndio kbs..........
duh hivi vibinti vya utumishi vitaangamiza taifa la mtwara
 
Yaani leo umeamua kuandika na rangi rangi ili tuelewe zaidi au?? (Joke)

Kumbe uko Mtwara mbona hatuambizani wajameni?? Mie niko Masasi nafundisha shule ya msingi (Jina kapuni)
 
Duh we ni m-bishi kama tomaso wa Yesu, sasa hapo zengwe linakuaje mkuu wakati watu wanaaibika? na inakuaje huyo waziri wa kikwete akapiga mkwara wasiende kijijini kwao??
sio mbishi mie mwenyewe ndio michezo yangu,ila poa nisiwaharibie wengine kazi.Nalog off
 
Back
Top Bottom