kadakokigondile
JF-Expert Member
- May 17, 2013
- 1,872
- 635
Anayo namba nyingine ambayo ni Hot Line anapatikana wakati wowote we piga 112 kisha toa shida yako watakusaidia
Amepokea?
Ingia mbugani kuwasaka. Wale wasaka naniii watakupa techniques.
Mwambie akupunguzie bana. Kwani una mpango wa kubeba kilo ngapi?
Kilo 45 tu, yaani hata mfuko mmoja wa simenti haujatimia
Wee Marketing Manager wake ndio nakutegemea, nikivusha kilo 2 zako.
Ingawa inaonekana kama maskhara,habari ndo hiyo!Majambazi,na wote wenye biashara haramu hizo ndo zao.
Una mpango wa kuvushia pande zipi ili niwe na uhakika kuwa 10% yangu itapita bila kuwa screened? Vinginevyo, bora unipatie zangu mapema, kikikunuka huko mie sipo. Kama ikishindikana kuna aina mpya ya kuvusha mzigo. Hii wala huitaji kugangia. Ni teke linalokujia tuu. Kuna fununu kuwa hili teke linalokujia mpya tayari imeshaanza kutumika hata hapa Bongo. Ila inabidi kucheza na jamaa ili wacheleweshe wale mbwa wa kunusa.
![]()
Wakati nchini Zimbabwe wanawake wakitumia pampers kukuza ukubwa wa makalio yao, nchini Marekani wamekuwa wakitengeneza pampers za cocaine, ambazo huvaliwa na kusafirisha dawa hizo nchi mbalimbali pasipo kugundulika. Mbinu hiyo mpya imedaiwa kuwagharimu muda mrefu waandaaji kutengeneza pampers hizo na baada ya kukamilika huvaliwa kitaalamu nje ya nguo zao za ndani na huvalia suruali au baibui tayari kwa kuanza safari.
Maofisa wa forodha kwenye Uwanja wa Ndege wa JFK wamegundua mbinu hiyo mpya mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuwatia mbaroni wanawake wawili kutoka Bronx wakiwa wamevalia madawa hayo. Wanawake hao wamekamatwa na kilogramu 6.5 za dawa za kulevya aina ya cocaine ambazo walikuwa wamezivalia kwa mtindo wa nepi nje ya nguo zao za ndani.
Kukamatwa kwa pea hiyo ya wanawake, kulitokana na walinzi kushangazwa na hali ya mbwa waliokuwa nao kuwafuatilia zaidi wanawake hao na kuanza kufoka ilhali walikuwa hawana mizigo, jambo lililowasukuma maofisa hao kuamua kuwakagua vilivyo. Baada ya kuchunguza kwa makini katika mizigo yao, hawakuweza kuona madawa yoyote, lakini walipojaribu kuwavua nguo zao walikutana na idadi kubwa ya dawa za cocaine yaliyokuwa yamefungwa mithili ya pampers nyuma ya makalio yao.
Lakini hata kama wakikumata bado unaweza kucheza na waganga wa kienyeji na kushinda kesi mahakamani kwa kuwawekea laana waendesha mashtaka. Victor Baurne (37) aliyekuwa meneja mizigo wa ndege hiyo alikamatwa katika kituo hicho hicho cha (JFK) John F. Kennedy International Airport kwa kosa la kusafirisha dawa za thamani zaidi ya Pauni 330 za cocaine toka mwaka 2000 mpaka mwaka 2009.
Baurne alidaiwa kuwa kwa kipindi chote cha miaka tisa, alikuwa akisafiri mpaka Afrika kwa ajili ya kudidimiza mwonekano wowote wa kazi yake ya kusafirisha dawa hizo. Wakati wa kesi yake, Baurne alikuwa akisafiri mara kwa mara mpaka Afrika kwa ajili ya kudidimiza kesi yake kwa uchawi, ambapo alikutana na waganga kadhaa ambao waliweka laana juu ya waendesha mashtaka, kulingana na nyaraka za mahakama.
Bourne pia alisisitiza kuwa wachunguzi wa kesi yake walikuwa wametoa maelezo ya uongo jambo ambalo lilikataliwa na mahakama. Hata hivyo mauzauza kadhaa yalikuwa yakionekana mahakamani hapo wakati kesi ya Bourne ikiendelea kusomwa kabla ya kupewa agizo la kifungo cha miaka 300 jela. Kiongozi huyo wa wafanyakazi wa American Airlines, Bourne alikuwa ametengeneza mamilioni ya dola ambayo aliyatumia kuhakikisha anafanya biashara yake anavyotaka, alisema hakimu Brooklyn.
Mbinu mpya za kusafirisha dawa za kulevya zaanikwa Marekani - Kimataifa - mwananchi.co.tz
HA ha ha ha ha ha h ha, jamani hii ni kali ya mwaka.
Kutokana na mofoloji yangu, bora niongeze kitambi nitaeleweka zaidi.
LANGO KUU LA KUZIMU LA DAR ES SALAAM
.......
Lango kuu la kuingilia kuzimu la Upanga Dar es Salaam linajulikana kwa jina la MUSTALLAH. Ndani ya shimo la Mustallah kuna aina kumi na mbili za majini makatili sana yanayoangamiza jamii ya watu wa jiji la Dar es Salaam. Wachawi wa nchi huenda mara kwa mara shimoni kuongeza nguvu za uchawi wao, kabla ya kuingia shimoni ni lazima ufunge kwa siku tatu.
Tuangalie sasa aina za haya majini ya Mustallah na kazi zao.
.......
6.Hazinan hili jini linalosimamia pombe, uvutaji wa sigara, madawa ya kulevya na mirungi.
.............