Uchawi haupo, ni imani tu

Ndugu,km umesoma vizuri uzi wangu nadhani umejieleza vizuri,kuwa Uchawi haupo kwa wenyewe, bali upo ktk mindset za watu, labda natumia lugha ngumu kidogo,hivyo mnashindwa kunielewa.Hebu nifafanue kidogo,ni hivi Ukiamini kuwa Uchawi upo utakuwepo tu,si umeamini?!!!.Lkn ukiamini kuwa haupo ila ni sarakasi za kihuni tu nakwambia hivi hutapatwa na chochote.Hata ktk maandiko matakatifu Uchawi unaotajwa humo ulitokana na kuamini,Imani ina nguvu sana,haijalishi iwe mbaya au nzuri,kazi kwako.
 
Sasa wewe umaamini Yesu wa nini sasa kama hamna uchawi? Hata yeye hakuna haja ya kumuamini kwa sababu anaamini mapepo na majini yapo na ndio uchawi wenyewe.
Soma vizuri uzi wangu utanielewa namaanisha nini.Inawezekana umesoma haraka haraka sana,Wewe soma taratibu.
 
Baraka ya watu,vitu,n.k.ni kawaida kwa Imani yangu km Mkristo Mkatoliki,nafanya hivyo km ishara ya kumkabidhi Mungu jitihada zangu ili kupitia maombi ya Mtumishi wake niweze kufanikiwa.
Kama unaamini baraka za Mungu basi ni kwamba unajua kuna upande wa pili unaoondoa hizo baraka
 
Yesu anao moto gani??, mbona alishindwa kuwawashia wale waliomtungika msalabani???. Akabaki kulia tu; ewe Baba ewe Baba mbona waniacha??
Hii siyo mzuri, acha mtu na imani yake
 
Kwenda nawe hoja kwa hoja ni kitwanga maji kwenyenu
 
Biblia yenyewe inakubari Uchawi Upo! Wewe ni nani mpaka Ukatae!???

Point ya msingi ni kuwa UCHAWI UPO ILA UKIAMINI JINA LA YESU LIPO JUU YA UCHAWI, UGANGA NA MAJINI!!!
that's it!
 
Yesu anao moto gani??, mbona alishindwa kuwawashia wale waliomtungika msalabani???. Akabaki kulia tu; ewe Baba ewe Baba mbona waniacha??
Sawa bhana naona umedhamiria kukufuru,lkn Yeye ninayemwabudu siku zote atatudhihirishia kuwa ndiye mwenye nguvu,uweza,mamlaka na enzi.Wewe endelea kudharau lkn nakwambia hivi njoo na kauchawi kako uone jinsi yatakavyokutokea puani.Yesu ni Mungu anaweza yote, anajua yote,hbr ya yeye kulia msalabani ni fumbo la Imani linaloweza kuelezeka kiimani zaidi kuliko kwa akili za kibinadamu,Mungu akusaidie uweze kuelewa fumbo hilo la mateso,kifo na ufufuko wa Yesu Kristo.
 
Biblia yenyewe inakubari Uchawi Upo! Wewe ni nani mpaka Ukatae!???

Point ya msingi ni kuwa UCHAWI UPO ILA UKIAMINI JINA LA YESU LIPO JUU YA UCHAWI, UGANGA NA MAJINI!!!
that's it!
Mkuu ukishaamini kuwa Uchawi upo,hilo ni tatizo,wewe amini kuwa Haupo,utaishi kwa raga mustarehe.
 
Kama unaamini baraka za Mungu basi ni kwamba unajua kuna upande wa pili unaoondoa hizo baraka
Baraka za Mungu haziondolewi na kitu chochote isipokuwa mtu mwenyewe aliyezipokea atakapokwenda kinyume na mapenzi ya Mungu hapo ndipo Baraka za Mungu zinaondoka.Uchawi hauna ngebe hizo.
 

Imani ni nini?

Imani ni hakika ya mambo yatarajiwayo. Ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Resubmit!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…