Uchawi haupo, ni imani tu

Uchawi haupo, ni imani tu

Mkuu,nimesema Uchawi km uchawi haupo,kilichopo ni ile hali ya watu kuamini kuhusu uchawi,namna walivyoziseti akili zao.Uchawi ni kitu cha kufikirika tu ukikiwazia sana lazima kikupelekeshe mpeta mpeta,lkn km huna mawazo kuhusu huo uchawi mbona utapeta sana.
Ndugu uchawi kama uchawi upo kabisa kama ambavyo wokovu upo na Yesu yupo. Huwezi kuukaaa uchawi kwamba haupo, je unakataa kwamba shetani yupo? Uchawi ni kazi ya shetani na mapepo yake kama zilivyo kazi za Roho Mtakatifu na Yesu. Uchawi sio kitu cha kufikirika ni halisi kabisa, iwe unaamini au huamini wazeza kudhurika na uchawi. Wewe hukudhurika kwasababu ulisali na kujiweka mikononi mwa Yesu, hiyo ndio dawa ya uchawi.
 
Nimeu-experience sema ni kitu ambacho hauwezi kuamini kama hujakishuhudia...na mtu hawezi kukuaminisha mpaka uje ukutane na matukio ambayo yako juu ya uwezo wa binadamu. Ambayo unasema kabisa hili haliwezekaniki kibinadamu.

Ukishakutana na miujiza na matendo makuu anayofanya Mungu maishani mwako...hilo la uchawi haliwezi kukusumbua kuamini kuhusu uwepo wake.
Asante sana mtumishi kwa mchango wako mzuri.
 
Kwenye kitabu hicho hicho anachokiamini, kimeongelea uchawi, labda ndani ya kitabu kimoja kuna anayoyaamini, na asiyoamini.
Ni kweli yameongelewa lkn hiyo haimaanishi kuwa tujenge imani hapo.Ktk Biblia mambo mazuri na mabaya yote yamezungumzwa,halikadhalika watu wema na wabaya.Sasa ni kazi kwako kufahamu Mungu anakutaka uelekee upande upi?.
 
Kwanini ulipeleka mbegu kanisani kuombea, huku ukiamini ushauri wa kitaalamu, kwenye kilimo.
Je kilichofanikisha wewe kupata mazao mengi, ni kanisa au kufuata kanuni za kitaalamu.
Je, mtu akienda kupanda mazao yaliyoombewa, bila kufuata kanuni za kitaalamu kwenye zao husika atavuna mazao mengi.
Je mtu akifuata tu kanuni za kitaalamu, bila kwenda kuombea mbegu atavuna kwa wingi.
Na kama hivyo vitu viwili havitengani, je wanaolima huku wakiwa hawaamini Mungu hawavuni mazao mengi.

Yote kwa yote, sayansi haimshirikishi Mungu, ingawa watu wa Mungu wanatambua sayansi, na kuitumia.
Naona umejihoji na kujijibu mwenyewe.Asante kwa mchango.
 
Ndugu uchawi kama uchawi upo kabisa kama ambavyo wokovu upo na Yesu yupo. Huwezi kuukaaa uchawi kwamba haupo, je unakataa kwamba shetani yupo? Uchawi ni kazi ya shetani na mapepo yake kama zilivyo kazi za Roho Mtakatifu na Yesu. Uchawi sio kitu cha kufikirika ni halisi kabisa, iwe unaamini au huamini wazeza kudhurika na uchawi. Wewe hukudhurika kwasababu ulisali na kujiweka mikononi mwa Yesu, hiyo ndio dawa ya uchawi.
Mimi siuimini sasa,vipi unataka kutest?.
 
Mbaka hapo hoja huna
Wakristo wanasema yesu ni mungu mkuu,,
Pasi na kutoa maelezo

Na waislam nao wanasema yesu si Mungu
bila hoja yeyote ya kuthibitisha

Alafu ukiulizwa toa ufafanuzi
Majibu ,, ndio nishasema
huo ni uchache wa hoja
Simama kutetea hoja yako kwa hoja

hauwezi kusema jela hakuna eti kwa sababu mm mwenyewe najishuhudia sijawahi kwenda jela,,

Kwa hiyo waliopo jela ni wajinga
Uchawi hakuna basi kwa akili zako

Unaulizwa nn maana ya uchawi jibu huna
basi kwa taarifa yako
Ukisikia mtu anafanya miujiza
Tambua tu anafanya uchawi

Yesu alifanya uchawi
Musa alifanya uchawi
Ibrahim alifanya uchawi
Nuhu alifanya uchawi
Muhamad alirogwa na wachawi
Soma vitabu vingi upata habari kasome habari za wakina kisisina ndio walioshusha vitabu vya tiba..
Mkuu mbona unakufuru???.Point zako bila hoja zilizoshiba ni kufukuza upepo tu.
 
Mkuu mbona unakufuru???.Point zako bila hoja zilizoshiba ni kufukuza upepo tu.
ndio maana nilihoji
Nini maana ya neno uchawi
Uchawi una tafsiri pana
Miujiza , karama ni uchawi pia

Farao alihita wachawi wake , wale wachawi wakatupa vijiti vingi Chini vile vijiti vakageka nyoka,

Naye nabii Musa akatupa ile fimbo yake chini akatokea nyoka mkubwa akawameza wale nyoka wote wa Farao
Kisha Musa akamshika yule nyoka mkiani akainua juu ule mkia wa nyoka
Nyoka ikapotea ikageuka fimbo ile ile ya awali
Kufuru yangu hapo ipo wapi?
Au kwa sababu nimemtaja na yesu??
 
Haya wewe inayeweza,hebu ututafsirie sasa.

Katika Bible umeelezewa uwepo wake kama hivi

"Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani" (1 Timotheo 4: 1).

Walawi 19:31 '' Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute; ili kutiwa unajisi na wao; Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.''

Katika Quran pia umeelezewa

“Na sema: Mola wangu Mlezi! Najikinga kwako na wasiwasi wa mashet'ani. Na najikinga kwako, Mola wangu Mlezi, wasinikaribie.” Quran surat al-an-muumin aya ya 97-98).

Kutokuamini katika nguvu za giza na kutegemea Mungu it's okay ila si kusema uchawi haupo.
 
Miujiza iliyofanywa na Musa huwezi kusema kuwa ni uchawi,bali ilifanyika kwa nguvu ya Mungu.Na lengo hapo ni kuonyesha kuwa Mungu ni mwenye nguvu.Siku nyingine usirudie tena kuiita miujiza ya Mungu ni uchawi.
 
Katika Bible umeelezewa uwepo wake kama hivi

"Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani" (1 Timotheo 4: 1).

Walawi 19:31 '' Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute; ili kutiwa unajisi na wao; Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.''

Katika Quran pia umeelezewa

“Na sema: Mola wangu Mlezi! Najikinga kwako na wasiwasi wa mashet'ani. Na najikinga kwako, Mola wangu Mlezi, wasinikaribie.” Quran surat al-an-muumin aya ya 97-98).

Kutokuamini katika nguvu za giza na kutegemea Mungu it's okay ila si kusema uchawi haupo.
Narudia tena,Uchawi haupo kwa mwenyewe bali kwenye akili za watu.
 
Haya wewe inayeweza,hebu ututafsirie sasa.
Kama unataka uamini uchawi upo pata utajiri! Ukipata utajiri na ukawa huna msimamo wowote kiroho yaani nuru/giza ukawa vuguvugu tu lazima uondoke/ufe chap! Ni either Yesu awe Mungu na mwokozi wa maisha yako haswahaswa au uwe na mganga wako ndipo utasurvive!
Fatilia utaona, kaa na watu waliofanikiwa kimaisha hata ambao si matajiri sana utagundua!
Matajiri wengi wako vizuri Sana kiroho,siyo blabla tu
 
Back
Top Bottom