Uchawi haupo, ni imani tu

Ndugu uchawi kama uchawi upo kabisa kama ambavyo wokovu upo na Yesu yupo. Huwezi kuukaaa uchawi kwamba haupo, je unakataa kwamba shetani yupo? Uchawi ni kazi ya shetani na mapepo yake kama zilivyo kazi za Roho Mtakatifu na Yesu. Uchawi sio kitu cha kufikirika ni halisi kabisa, iwe unaamini au huamini wazeza kudhurika na uchawi. Wewe hukudhurika kwasababu ulisali na kujiweka mikononi mwa Yesu, hiyo ndio dawa ya uchawi.
 
Asante sana mtumishi kwa mchango wako mzuri.
 
Kwenye kitabu hicho hicho anachokiamini, kimeongelea uchawi, labda ndani ya kitabu kimoja kuna anayoyaamini, na asiyoamini.
Ni kweli yameongelewa lkn hiyo haimaanishi kuwa tujenge imani hapo.Ktk Biblia mambo mazuri na mabaya yote yamezungumzwa,halikadhalika watu wema na wabaya.Sasa ni kazi kwako kufahamu Mungu anakutaka uelekee upande upi?.
 
Naona umejihoji na kujijibu mwenyewe.Asante kwa mchango.
 
Mimi siuimini sasa,vipi unataka kutest?.
 
Mkuu mbona unakufuru???.Point zako bila hoja zilizoshiba ni kufukuza upepo tu.
 
Mkuu mbona unakufuru???.Point zako bila hoja zilizoshiba ni kufukuza upepo tu.
ndio maana nilihoji
Nini maana ya neno uchawi
Uchawi una tafsiri pana
Miujiza , karama ni uchawi pia

Farao alihita wachawi wake , wale wachawi wakatupa vijiti vingi Chini vile vijiti vakageka nyoka,

Naye nabii Musa akatupa ile fimbo yake chini akatokea nyoka mkubwa akawameza wale nyoka wote wa Farao
Kisha Musa akamshika yule nyoka mkiani akainua juu ule mkia wa nyoka
Nyoka ikapotea ikageuka fimbo ile ile ya awali
Kufuru yangu hapo ipo wapi?
Au kwa sababu nimemtaja na yesu??
 
Haya wewe inayeweza,hebu ututafsirie sasa.

Katika Bible umeelezewa uwepo wake kama hivi

"Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani" (1 Timotheo 4: 1).

Walawi 19:31 '' Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute; ili kutiwa unajisi na wao; Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.''

Katika Quran pia umeelezewa

“Na sema: Mola wangu Mlezi! Najikinga kwako na wasiwasi wa mashet'ani. Na najikinga kwako, Mola wangu Mlezi, wasinikaribie.” Quran surat al-an-muumin aya ya 97-98).

Kutokuamini katika nguvu za giza na kutegemea Mungu it's okay ila si kusema uchawi haupo.
 
Miujiza iliyofanywa na Musa huwezi kusema kuwa ni uchawi,bali ilifanyika kwa nguvu ya Mungu.Na lengo hapo ni kuonyesha kuwa Mungu ni mwenye nguvu.Siku nyingine usirudie tena kuiita miujiza ya Mungu ni uchawi.
 
Narudia tena,Uchawi haupo kwa mwenyewe bali kwenye akili za watu.
 
Haya wewe inayeweza,hebu ututafsirie sasa.
Kama unataka uamini uchawi upo pata utajiri! Ukipata utajiri na ukawa huna msimamo wowote kiroho yaani nuru/giza ukawa vuguvugu tu lazima uondoke/ufe chap! Ni either Yesu awe Mungu na mwokozi wa maisha yako haswahaswa au uwe na mganga wako ndipo utasurvive!
Fatilia utaona, kaa na watu waliofanikiwa kimaisha hata ambao si matajiri sana utagundua!
Matajiri wengi wako vizuri Sana kiroho,siyo blabla tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…