Uchambuzi wangu mfupi juu ya Lowassa kurejea CCM

In
Upinzani uliobaki ni wa kuropoka kwa tafsiri ya ccm. Unasema unawanyima trust vijana. Nyie vijana mko kwenye kichaka gani mnasubiri trust kwa wengine? Kwanini vijana msijitokeze mtengeneze upinzani wenu utakaojenga trust? Unasema huko kuna demokrasia ya kweli, demokrasia ipo, kama ni ya kweli au la inategemea utashi wako, haikufai unaweza kuondoka maana chama sio nchi. Upigaji wa ruzuku uko chama chochote na kama ni kipimo basi ccm ni zaidi, huo upigaji ni tatizo letu kama taifa, iwe serekalini, kwenye taasisi za dini, michezo nk.

Unasema hata Lowassa ni powerful, Lowassa hakuwa powerful wala hatakaa awe powerful bali alikuwa anahonga watu kumsifia, hongo hizo alizitoa kwa wapambe wa kisiasa, nyumba za ibada nk. Sijawahi kumuona Lowassa ukiacha alivyokuwa waziri mkuu, akiongea zaidi ya dkt 15 akitoa falsafa zake na kushawishi kwa hoja. Watu wenye uelewa finyu ndio walichezeshwa propaganda za kwamba Lowassa ni powerful kupitia wapambe wake, vyombo vya habari na viongozi wa dini waliokula hela zake. Juu ya hayo hakuna mabadiliko yanaletwa na mtu/mzee aliye above 60yrs hasa mtu huyo awe yuko au ametoka ccm.

Unasema national strategy ya upinzani ni kuitoa ccm kwa hili uko sahihi, kumbuka kuitoa ccm ni ushindani na siku zote kwenye ushindani kuna mshindi na mshindwa. Pia ccm kwa sasa sio chama cha siasa kinachoshindina kisiasa bali ni chama chenye mafungamano na vyombo vya dola, hivyo kukitoa inabidi nguvu ya zaidi ya ushawishi wa kisiasa na box la kura. Hii ni nchi yetu na tunaona kinachoendelea kwenye box la kura jinsi gani taasisi za kimamlaka na vyombo vya dola vinavyoibeba ccm. Maandalizi ya mgombea urais yako vizuri na chama kiko hai hata kama kinafanyiwa hujuma za wazi na rais aliye madarakani. Ukija kujadiliana na mimi hakikisha hubebi hoja za kufuata mkumbo na kuokoteza okoteza maana utapata tabu sana.
Inaonekana unachambua kimahaba hivi kweli Lowasa sio powerful? Katika siasa kuwa powerful sio lazima uwe muongeaji sana. Inakubidi uwe na strarejia kali ambako huko Lowasa kafuzu.Inaonekama jamaa hujamuelewa hoja yake anayomaanisha.Kuna vijana wapo upinzani, wengine chama tawala na wengine hawafungamani na upande wangu.Wapo wengine ambao hawapo upinzani kwa sababu hawaupendi na wengine wanaona wanaona hauna muelekeo.Jambo ambalo liko wazi ni kwamba upinzani wa Tanzania ni wa ndimi mbili.Hauna itikadi wanayoisimamia wao wako tayari kufanya lolote ili mradi lilinde maslahi yao.Wao hawaangalii hili suala lina madhara kiasi gani.Unaposema kirahisi kuwa kula ruzuku hata chama tawala wanakula, kwa hiyo wewe unaona ni sahihi wao kutenda matendo ya chama tawala?Ipi tofauti yao na chama tawala?Kutokana na hilo ndipo utakuta kundi la vijana wasiofungamana na upande wowote.
 
In
Inaonekana unachambua kimahaba hivi kweli Lowasa sio powerful? Katika siasa kuwa powerful sio lazima uwe muongeaji sana. Inakubidi uwe na strarejia kali ambako huko Lowasa kafuzu.Inaonekama jamaa hujamuelewa hoja yake anayomaanisha.Kuna vijana wapo upinzani, wengine chama tawala na wengine hawafungamani na upande wangu.Wapo wengine ambao hawapo upinzani kwa sababu hawaupendi na wengine wanaona wanaona hauna muelekeo.Jambo ambalo liko wazi ni kwamba upinzani wa Tanzania ni wa ndimi mbili.Hauna itikadi wanayoisimamia wao wako tayari kufanya lolote ili mradi lilinde maslahi yao.Wao hawaangalii hili suala lina madhara kiasi gani.Unaposema kirahisi kuwa kula ruzuku hata chama tawala wanakula, kwa hiyo wewe unaona ni sahihi wao kutenda matendo ya chama tawala?Ipi tofauti yao na chama tawala?Kutokana na hilo ndipo utakuta kundi la vijana wasiofungamana na upande wowote.

Huenda umeona post moja kisha ukaja na hoja zako. Nimesema hao vijana wazuri wanasubiri nani awaanzishie chama cha upinzani makini? Kwahiyo wao wakae pembeni kisha wangoje wengine waanzishe chama ndio waende kuonyesha umakini wao? Huo umakini wao uko wapi sasa? Nchi hii inayoongozwa na wanasiasa walioko kwenye vyama, hakuna mgombea binafsi, hao vijana wasiofungamana na upande wowote wapiganie mgombea binafsi au wakae waangalie wenye vyama wakifanya yao.

Kula ruzuku/fedha ya umma ni tatizo la kijamii, lakini huwezi kuniambia eti wananchi hawawezi kukichagua chama eti kisa kuna wala ruzuku. Kwanza tatizo la uadilifu ni la kijamii kuanzia wapiga kura mpaka wapigiwa kura, ila cha muhimu yoyote anayeiba hela ya umma vyombo vya kisheria vichukue hatua bila kujali mtu/chama gani. Leo hii ccm wako madarakani na wanakula ruzuku, wamechaguliwa na majini?
 
Angalizo zuri Mwalimu, lakini wasomi wa kuwanukuu ni hawa?
1. Prof Lipumba
2. Dr. Mwakyembe
3. Jaji Mutungi
4. Prof Kitila
5. Prof Kabudi
6. Dr. Mwigulu
7. Dr. Bashiru
8. Dr Ryoba
9. Mambosasa
10. Pole pole
11. Makonda
12. Lowassa
13. Dr. Pombe
14. Ally Karume
15............
16.........

Hakuna shida shida ndugu yangu Hatihat hao wakiwa ndio wahusika. Uzuri wa kazi za kisomi/kitafiti/kizuoni hazitazami sura ya mtu, umbo lake, mitizamo yake, wala mwelekeo wake kisiasa na kijamii. Kazi za kitafiti/kizuoni zinapimwa kisanyasi na aina ya maarifa yaliyomo. Hivyo kama kuna kazi/machapisho/vitabu wameandika katika eneo husika, bado zina nafasi katika kutoa mchango wa maarifa, nadharia, na kuchochea fikra za kichambuzi. Kama kuna umengine yenye walakini katika maisha yao binafsi, unawaachia wenyewe.

MM
 
Ukisoma andiko la John. H. Barret linaitwa Individual Goal & Organizational objectives na maandiko yake mengine utafahamu sura ya maamuzi ya Mh.Lowasa kurudi CCM.

Katika maisha ya kila siku, binadamu huwa ana malengo makuu 2 ,moja ni lengo binafsi (Persons goals au individual goals) na malengo ya kitaasisi au malengo ya timu .(organizational goals,au Team goals).

Mfano ,ukiwa katika taasisi utakuwa na malengo binafsi ya kupata kitu ,kupandishwa cheo,heshima,kuwa mchapakazi mzuri na hapo hapo utakuwa na malengo ya kitasisi kusaidia taasisi kukuwa.

Viongozi wengi walio katika vyama vya Siasa wana malengo binafsi ya kuendelea kuwa wanasiasa wazuri pia wana malengo ya kitaasisi ,chama chao kuendelee kukuwa na kushika dola au kiendelee kushika dola.

2015, Mh.Lowasa alihamia Chadema hivyo kuwa mgombea urais kupitia ukawa ,kilichomfanya Mh.Lowasa kuhamia Chadema ni lengo binafsi (Individual goal) la kugombea urais ili kuwa Rais hivyo alihama kutafuta njia ya kutimiza lengo na adhma yake .

Mh.Lowasa hakuwahi kuwa na lengo la kitaasisi (Organizational goal) ambapo ina maana ya lengo la kusaidia chadema kuimarika ,hakuwahi kuwa na lengo hilo ,hii ni tofauti aliyokuwa nayo na viongozi wengine wa chadema ambao walikuwa na malengo 2 ,binafsi na ya kitaasisi.

Ukimsoma John H.Barret anasema "The organization contributes to individual goal attainment" Jumuiya au taasisi inasaidia sana mtu kutimiza lengo binafsi, hivyo alichoamini Mh.Lowasa ni kujiunga chadema (Ukawa) ili lengo lake litimie la kupata urais.

Ni jambo lisilo pingika alileta ushindani mkubwa hadi kufikia kupata kura milioni 6 dhidi ya Mh.Rais Magufuli kura milioni 8 ,kura hizi zilimpa ujasiri wa kuendelea kubaki upinzani huku akirefusha malengo yake ya kugombea urais kufikia 2020.

Kumbuka mahojiano akiwa Nairobi na kituo cha TV (Nation TV)tarehe 16/July/2017.Alisema,

"Watu wengi wananiuliza kuhusu 2020, Jibu ni Moja Tu. NITAGOMBEA"
Edward Lowassa
Nairobi Serena
16 July 2017"

Lakini lazima tufahamu kuwa Siasa hubadilika badilika ,Siasa sio static ! Siasa ni Dynamic ,ni changeable sio unchangeable.

Ukisoma kitabu cha "Political Dynamics " kilichoandikwa na Asmeritic Bier,Richard Hills,Michael Bernard na wenzao utaona walisema kubadilika badilika kwa Siasa kunategemea mahusiano na muingiliano kati ya viongozi wa kisiasa na wananchi (wapiga kura),wananchi wanaweza waza hivi leo ila kesho wakawaza vingine ukabaki unashangaa,wanasema ni vigumu kutabiri ya kesho katika Siasa.
."Political Dynamic determined by interaction between political leaders and voters,it is difficult to predict ".

Kuanzia 2015 kuelekea 2016 mwishoni upepo wa Mh.Lowasa ulikuwa mkubwa ,na yeye bado alikuwa akiamini katika kura milioni 6 alizopata kama mtaji 2020.

Wanachama wa Chadema na ukawa walitokea ghafla kuvutiwa na Mh.Tundulisu kuanzia 2017 kuelekea 2018 ,hasa katika masuala mengi aliyokuwa anayaibua na kuyashikilia ,hivyo upepo wa Mh.Lowasa ukaanza kufifi ndio maana ya Political dynamics.

Hadi changamoto alizopata Tundulisu na hata yeye kufikia waziwazi kusema akipendekezwa anaweza kubali kugombea 2020 ,pia hata wanachama wengi wa chadema wanapendekeza Tundulisu agombee 2020.

Hili ni Jambo ambalo kwa kawaidi moja kwa moja ,lilikuja kusambaratisha malengo ya Mh.Lowasa kugombea Urais 2020.

Lengo binafsi linasifa zake kwanza liwe specific, Mh.Lowasa alitaka kugombea urais (Specific) haoni tena suala hilo ,(Time bound ) alitaka iwe 2020 ,haoni tena ikiwa wengi wanampendekeza Lissu 2020, (Relevant) haoni tena relevance ya lengo lake sababu Kuna mwingine watu wameibuka nae sababu ya mabadiliko ya kisiasa hivyo haoni mbele tena ,(Attainable) ,je lengo hilo la urais angeweza kulitimiza na akapitishwa kura za maoni ,jibu aliona hapana sababu umma wanachama ulibadilika ghafla.

Hivyo hakuwa na chaguo lolote zaidi ya kurudi CCM ,ambapo anahisi atapata kuendelea kupata heshima yake kama waziri mkuu mstaafu ,na kufa akiwa katika chama chake kilichomlea hata kama akiwa mwanachama bila cheo au bila kugombea,kuliko kubaki chama ambacho alihamia tuu kwa lengo moja ambalo hakulipata .

Maamuzi yake yanatoa funzo kwa vyama pinzani kuandaa watu katika ngazi zote ,udiwani,ubunge ,hata urais .Wawe watu wenye malengo 2 ,binafsi na malengo ya kitaasisi (kukuza chama).

Shukrani.

Abdul Nondo.

Abdulnondo10@gmail.com

Sent using Jamii Forums mobile app
Kijana analysis yako na ushauri mzuri lakini sababu ya partisan politics umeamua kuonyesha CHADEMA wanatofautiana na Loawasa wakati kiujumla ulichokijadili katika mada yako kwetu sisi Independent tunakio a hakina tofauti na CHADEMA. CHADEMA walimchukua Lowasa kwa lengo la kushinda iwe iweje na siyo kwa lengo la kukiimarisha chama chao. Lengo lao halikua tofauti na waliyemuweka kugombea nalo ni uchu wa madaraka.
 
Maamuzi yake yanatoa funzo kwa vyama pinzani kuandaa watu katika ngazi zote ,udiwani,ubunge ,hata urais .Wawe watu wenye malengo 2 ,binafsi na malengo ya kitaasisi (kukuza chama).

Shukrani.

Abdul Nondo.

Abdulnondo10@gmail.com

Sent using Jamii Forums mobile app

Mapendekezo hayo yalitolewa baada ya uchaguzi wa 2010. Na kazi kubwa ikaanza kufanyika kuijenga CHADEMA katika ngazi hizo zote na kuwaandaa watu mbalimbali. Hadi pale "magenius" wa CHADEMA wakaambiana kuwa juhudi zao zote zile zisingelipa wakaamua kutafuta njia ya mkato. Kama viongozi wenyewe hawana malengo ya "kitaasisi" basi malengo binafsi mara zote yatatamalaki!
 
Kijana analysis yako na ushauri mzuri lakini sababu ya partisan politics umeamua kuonyesha CHADEMA wanatofautiana na Loawasa wakati kiujumla ulichokijadili katika mada yako kwetu sisi Independent tunakio a hakina tofauti na CHADEMA. CHADEMA walimchukua Lowasa kwa lengo la kushinda iwe iweje na siyo kwa lengo la kukiimarisha chama chao. Lengo lao halikua tofauti na waliyemuweka kugombea nalo ni uchu wa madaraka.

Umesema vizuri hapa; lakini pia kwa kuongezea ni kuwa siyo tu 'uchu wa madaraka' lakini ni ule uchu ambapo mtu badala ya kufanya kazi anaamua kutafuta njia ya mkato. Viongozi wa CDM na mashabiki wao waliamini kabisa kuwa Lowassa alikuwa ni njia ya mkato.
 
Hapa ni uzi unao husu lowasa kwenda ccm na we ukitaka pandisha uzi wa lowasa kuhama cdm

In God we trust
Mkuu ukitengeneza uchambuzi wa kuonya huoni ni vizuri ukawa muwazi kuliko kuwa mnafiki? Maana kimsingi mada haziwezi kuwa mbili zikimhusu mtu moja. Viongozi baadhi ya CHADEMA na Lowasa wana malengo yanayoshabiiana kama Nondo alivyosema. Upepo wa Lowasa walitaka kuuchukulia advantage ambayo haikufanikiwa. Kwanini tunasema lengo lao linafanana sababu tu Nomination ya Lowasa haikufuata maudhui ya chama bali ya wachache ambao walijua kama lengo lingefanikiwa wangepata vijinafasi kama asante kutoka kwa Lowasa.
 
Lissu aliwahi kutuambia kuwa Chadema ilifanya utafiti wake kwa kuwatumia wazungu na waliogopa kuwatumia watanzania wasije wakawadanganya na wale watafiti waliwajibu Chadema ili malengo ya Chadema yatimie ya kushika Dola lazima wampate Mh Lowasa.

Hivyo japo Lowasa aliamini lazima awe Rais wa Tanzania pia haindoi ukweli kuwa Chadema nao waliona 2015 lazima waishike nchi..! Tena imani hii kwao kwa 2015 ilikuwa kubwa kwa Mh Lowasa kuliko imani waliyokuwanayo 2020.

Lowasa hakuiwezesha Chadema kushika Dola lakini tusijidanganye leo hii kuwa ata viti vya ubunge walivyopata Chadema ni baada ya upepo kubadilika kwa ujio wa Lowasa Chadema.

Ujio wa Lowasa ndani ya Chadema lilikuwa lengo la Taasisi na Lengo lake Lowasa binafsi.

Tukisema Lisu ni sawa na Donald Trump ni tapeli mjanja ila wafuasi hawalijui hilo.
 
Good and valuable thread.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna kitu kuna mahali anaonyesha wazi kuwa ni zero kabisa.mfano kasema wanachadema walio wengi wanataka Tundu Lisu agombee uraisi kupitia chadema.Hizo statistics kazitoa source ipi kuonyesha wanachadema walio wengi wanataka Lisu hakuweka !!!! Kabaki kupiga bla bla tu kuwa Lisu ndie popular chadema na Lowassa kajiona hamfikii Lisu bila evidence yeyote ya reliable source ya Takwimu.Cha pili hajui hata utaratibu wa kupata mgombea uraisi chadema.Mgombea uraisi huteuliwa na UKAWA sio chadema sababu chadema iko kwenye muungano wa UKAWA.Wao ndio huamua nani agombee sio chadema!! Tatu kajipalia makaa ya moto kukaa na kujionyesha wazi kuwa yuko upande wa Tundu Lisu.Ndani ya chadema mle kuna makundi hasimu yasiyompenda Lisu sababu ya mipango yake ya kutaka kugombea uenyekiti Chadema kumngoa Mbowe.Hivyo Nondo kushindwa kusoma internal politics za chadema kajiingiza mkenge kichwa kichwa kujionyesha wazi kuwa yuko upande wa Lisu sio wa Mbowe !!!!
 
Ha ha ha! Kwamba binadamu ana malengo makuu mawili (2)?

Huo ni ukalilifu wa kupindukia - rudi tena kwenye misahafu
 
Back
Top Bottom