Uchambuzi wangu mfupi juu ya Lowassa kurejea CCM

Dr. Slaa hakutoka cdm kwa utashi wake. Sote tunajua mazingira yalivyokuwa na mengine siyo busara hata kujadili hadharani. Yameshapita hayo tugange yajayo. Ya Lipumba ndiyo kabisa hatuhitaji hata kujadili kwani kila mtu anaona kwa macho yake kazi aliyopewa. Kifupi, Nyerere's country is gone to the dogs, period!
MTU akihama upinzani kwenda ccm sio utashi wake, ila akihama ccm kwenda upinzani ni haki yake ya msingi na ndio demokrasia ya kweli....ama hakika safari bado ndefu katika Uhuru Wa fikra na tafsiri sawa ya demokrasia ya vyama vingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Write your reply...katika jambo ambalo chadema walifanya makosa in kumpokea Lowasa.Hii imewaweka wazi kuwa ni watafuta madaraka na si wapigania haki za wananchi.Chadema walijijenga vyema hasa katika kuwatetea wanyonge,ghafla watu waliowataabisha wananchi wakapokelewa chadema.kimsingi kuna haja yakuwa na chama mbadala cha upinzani kitakacho kuwa na uwezo wa kusimamia maslahi ya Taiga.
Na ghafla Hao wagandamiza haki wakaanza Kuhama tena kwenda/kurudi Team ya NDULI,hili nalo walionaje si wamerudi Nyumbani kwao kwa NDULI?, means uchafu uliokuja umerudi ulikotoka na kama chama pendwa kilichafuliwa na hyo oil chafu basi sasa kime mwaga uchafu na kubaki salama zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lowassa kwenda CHADEMA mnazungusha mikoni na kudeki barabarani, lakini akirudi CCM inakuwa nongwa. Halafu mnajidai mnapigania demokrasia, sasa mbona mnakwazika na uamuzi wa Lowassa?
Yeyote Anaryhusiwa kuhamia popote, So kama E.L karudi Team NDULI hakuna wakumkataza. mijadala lazima iwepo ,watu lazima watoe maoni na mitazamo yao na hiyo ndio demokrasia japo team NDULI wanaweka mipaka ya demokrasia ndani ya UHURU wa demokrasia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kijana wangu Nondo,

Umefanya vema sana kuchambua jambo hili kitaaluma ukitumia nadharia za kutaasisi na kimifumo (Institutional and Organisational Theories) na sio kisiasa (political biasness) kama ilivyozoeleka humu jukwaani. Kwa kufanya hivi umeitendea haki JF kama maskani ya tafakuri tunduizi na wewe mwenyewe kama mtaalamu (mtarajiwa!!) wa sayansi ya siasa.

Hata hivyo ninaona kasoro moja kubwa ambayo inaonekana mara nyingi kwetu sisi watanzania tunapofanya marejeo ya nadharia, vitabu, au makala za kitaaluma katika uwasilishaji wetu: kwamba tunaendeshwa au kutukuza sana fikra na tafakuri za kisomi za wataalamu na waandishi wa nje na haturejei kabisa wataalamu wa ndani hata katika fani kama yako ambayo ina uhusiano mkubwa sana na mazingira na matukio ya kila siku ya kijamii. Utanisahihisha kama siko sahihi, ila dhana hii imejenga fikra kwa watanzania wengi kwamba mtu anapomnukuu msomi/mwandishi/kiongozi mtu fulani wa Ulaya, Amerika, au Mashariki ya mbali, basi mtu huyo huonekana msomi/mjuaji zaidi na anachokiongea kina tija zaidi na hili huonekana sana katika muktadha wa kisasa (ambayo imetawala sana maisha yetu) na wasomi au wanazuoni kama wewe. Nini msingi wa hoja yangu?

Utakubaliana nami kwamba ukisoma nadharia za kitaasisi, mifumo, na oganaizesheni (institutional, systems, and organisational theories), pamoja na mambo mengine, utaona msisitizo wa umuhim wa kuzingatia mazingira halisi au muktadha (context) katika kuchambua, kutafiti, kutafuta maana, na kuchokonoa tafakuri tunduizi zitokanazo na matukio na michakato ya kitaasisi na mifumo: hasa unapotumia dhana za kinadharia (concepts or constructs emerging from theoretical perspectives). Hivyo kwa uchambuzi kama huu ambao umetumia nadharia za kitaasisi, mifumo, na sayansi ya siasa kwa jambo lililotokea katika mazingira yetu, nilitegemea kuona nukuu na rejea za wabobezi wa taalama hizo toka Afrika, Tanzania au chuo chako: na mahususi idara unayosoma. Nadhani idara yako ni moja ya idara zenye wanazuoni bingwa (maprofesa) wa utawala, mifumo, na siasa kuliko nyingine nyingi katika CKD (walifariki,, waliostaafu, walioko kwenye tafiti, na "waliokwenda mjini"). Kwa nini hakuna fikra zao katika uchambuzi kama huu? Ni kwa sababu hatuziamini? Ni kwa sababu hawaandiki vitabu/majarida? Au ni kwa sababu wanachoandika hakina uzito/mashiko?

Nimalize kwa kusema kuwa, pamoja na kwamba hoja yangu imekulenga moja kwa moja katika ulichoandika, haimaniishi nakukosoa wewe binafsi au kukushanbulia, Nimekusudia tu kuleta changamoto na kuibua tafakuri na maswali juu ya nafasi ya wazalisha maarifa katika jamii na mazingira yetu na namna sisi wengine tunavyoheshimu, kuthamini, na kutumia maarifa hayo katika chambuzi zetu, kuibua mijadala na tafakuri tunduizi. Hivyo usisome nilichandika kwa mtizamo binafsi (individual perspective) wenye lengo binafsi (in serving individual goal) bali katika mtizamo wa kimfumo (system perspective) kwa manufaa ya jukwaa (serving a system goal).

Again, hongera kwa kuitendea haki elimu yako. If mentored/ guided, you can make a good researcher /academic.

Mwalimu MM
Angalizo zuri Mwalimu, lakini wasomi wa kuwanukuu ni hawa?
1. Prof Lipumba
2. Dr. Mwakyembe
3. Jaji Mutungi
4. Prof Kitila
5. Prof Kabudi
6. Dr. Mwigulu
7. Dr. Bashiru
8. Dr Ryoba
9. Mambosasa
10. Pole pole
11. Makonda
12. Lowassa
13. Dr. Pombe
14. Ally Karume
15............
16.........
 
Ukisoma andiko la John. H. Barret linaitwa Individual Goal & Organizational objectives na maandiko yake mengine utafahamu sura ya maamuzi ya Mh.Lowasa kurudi CCM.

Katika maisha ya kila siku, binadamu huwa ana malengo makuu 2 ,moja ni lengo binafsi (Persons goals au individual goals) na malengo ya kitaasisi au malengo ya timu .(organizational goals,au Team goals).

Mfano ,ukiwa katika taasisi utakuwa na malengo binafsi ya kupata kitu ,kupandishwa cheo,heshima,kuwa mchapakazi mzuri na hapo hapo utakuwa na malengo ya kitasisi kusaidia taasisi kukuwa.

Viongozi wengi walio katika vyama vya Siasa wana malengo binafsi ya kuendelea kuwa wanasiasa wazuri pia wana malengo ya kitaasisi ,chama chao kuendelee kukuwa na kushika dola au kiendelee kushika dola.

2015, Mh.Lowasa alihamia Chadema hivyo kuwa mgombea urais kupitia ukawa ,kilichomfanya Mh.Lowasa kuhamia Chadema ni lengo binafsi (Individual goal) la kugombea urais ili kuwa Rais hivyo alihama kutafuta njia ya kutimiza lengo na adhma yake .

Mh.Lowasa hakuwahi kuwa na lengo la kitaasisi (Organizational goal) ambapo ina maana ya lengo la kusaidia chadema kuimarika ,hakuwahi kuwa na lengo hilo ,hii ni tofauti aliyokuwa nayo na viongozi wengine wa chadema ambao walikuwa na malengo 2 ,binafsi na ya kitaasisi.

Ukimsoma John H.Barret anasema "The organization contributes to individual goal attainment" Jumuiya au taasisi inasaidia sana mtu kutimiza lengo binafsi, hivyo alichoamini Mh.Lowasa ni kujiunga chadema (Ukawa) ili lengo lake litimie la kupata urais.

Ni jambo lisilo pingika alileta ushindani mkubwa hadi kufikia kupata kura milioni 6 dhidi ya Mh.Rais Magufuli kura milioni 8 ,kura hizi zilimpa ujasiri wa kuendelea kubaki upinzani huku akirefusha malengo yake ya kugombea urais kufikia 2020.

Kumbuka mahojiano akiwa Nairobi na kituo cha TV (Nation TV)tarehe 16/July/2017.Alisema,

"Watu wengi wananiuliza kuhusu 2020, Jibu ni Moja Tu. NITAGOMBEA"
Edward Lowassa
Nairobi Serena
16 July 2017"

Lakini lazima tufahamu kuwa Siasa hubadilika badilika ,Siasa sio static ! Siasa ni Dynamic ,ni changeable sio unchangeable.

Ukisoma kitabu cha "Political Dynamics " kilichoandikwa na Asmeritic Bier,Richard Hills,Michael Bernard na wenzao utaona walisema kubadilika badilika kwa Siasa kunategemea mahusiano na muingiliano kati ya viongozi wa kisiasa na wananchi (wapiga kura),wananchi wanaweza waza hivi leo ila kesho wakawaza vingine ukabaki unashangaa,wanasema ni vigumu kutabiri ya kesho katika Siasa.
."Political Dynamic determined by interaction between political leaders and voters,it is difficult to predict ".

Kuanzia 2015 kuelekea 2016 mwishoni upepo wa Mh.Lowasa ulikuwa mkubwa ,na yeye bado alikuwa akiamini katika kura milioni 6 alizopata kama mtaji 2020.

Wanachama wa Chadema na ukawa walitokea ghafla kuvutiwa na Mh.Tundulisu kuanzia 2017 kuelekea 2018 ,hasa katika masuala mengi aliyokuwa anayaibua na kuyashikilia ,hivyo upepo wa Mh.Lowasa ukaanza kufifi ndio maana ya Political dynamics.

Hadi changamoto alizopata Tundulisu na hata yeye kufikia waziwazi kusema akipendekezwa anaweza kubali kugombea 2020 ,pia hata wanachama wengi wa chadema wanapendekeza Tundulisu agombee 2020.

Hili ni Jambo ambalo kwa kawaidi moja kwa moja ,lilikuja kusambaratisha malengo ya Mh.Lowasa kugombea Urais 2020.

Lengo binafsi linasifa zake kwanza liwe specific, Mh.Lowasa alitaka kugombea urais (Specific) haoni tena suala hilo ,(Time bound ) alitaka iwe 2020 ,haoni tena ikiwa wengi wanampendekeza Lissu 2020, (Relevant) haoni tena relevance ya lengo lake sababu Kuna mwingine watu wameibuka nae sababu ya mabadiliko ya kisiasa hivyo haoni mbele tena ,(Attainable) ,je lengo hilo la urais angeweza kulitimiza na akapitishwa kura za maoni ,jibu aliona hapana sababu umma wanachama ulibadilika ghafla.

Hivyo hakuwa na chaguo lolote zaidi ya kurudi CCM ,ambapo anahisi atapata kuendelea kupata heshima yake kama waziri mkuu mstaafu ,na kufa akiwa katika chama chake kilichomlea hata kama akiwa mwanachama bila cheo au bila kugombea,kuliko kubaki chama ambacho alihamia tuu kwa lengo moja ambalo hakulipata .

Maamuzi yake yanatoa funzo kwa vyama pinzani kuandaa watu katika ngazi zote ,udiwani,ubunge ,hata urais .Wawe watu wenye malengo 2 ,binafsi na malengo ya kitaasisi (kukuza chama).

Shukrani.

Abdul Nondo.

Abdulnondo10@gmail.com

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante kwa uchambuzi, ila Mimi Naona ameenda ili amkwamue mkwewe aliyekuwa lockup aachiwe huru. So Kuondoka kulikuwa motivated na family matters than political issues. On top of that mi naona pia uwepo wao upinzani uliwafanya watawala kuongeza mbinyo wa kuwadhibiti upinzani kwa kuwa walijua wakiwaacha huru ni threat kwa sisiem maana masisiem wengine wangeweza kumufuata. bora ameondoka tu
 
Akaona bora areje alikoibia nchi akishirikiana na mabeberu. Chama cha waoga wanaogopa hata akina mama de chadema na ACT kutumia mibaba yenye bunduki.
sasa mkwe wake atafutiwa kesi na mali zake alizopora watanzania zirakuwa salama zitasaidia kujenga ccm

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upinzani wa kuropoka sio tafsiri ya CCM na Wana CCM pekee bali ni hali halisi ya upinzani wa nchi yetu ukiondoa mahaba yetu ya kutetea vyama vyetu na kutopenda kuzungumziwa tusiyoyapenda...
Upinzani uliojikita kwenye nini kitazungumzwa na serikali au chama tawala ndipo basis ya hoja itokee kwao...hakuna hoja halisi kwa sasa Bali inategemeana na upepo wa siku toka serikalini.
Kwa wauimini wa siasa wasiofungamanishwa na upande katika kujadili hoja zao wanauona ukweli halisi ambao waumini kindakindaki hawawezi ona yasiyowafurahisha daima huona wanayoyataka Tu.
Maoni na hoja mbadala yanahitajika katika kila hoja pingani kutoka upande usiokubaliana....
Wizi wa ruzuku kuwa ni changamoto ya kitaifa haiupi uhalali upinzani unaotarajia kuleta serikali mbadala kuona ni jambo la kuzoeleka...mbadala wa DHAMBI haupaswi kuwa dhambi Bali epuko la dhambi Kwa vitendo....
Kumtangaza mtu miaka zaidi ya nane kuwa ni fisadi papa na nyangumi, Kwa kutumia rasilimali za wazalendo wenye kuona umuhimu wa mabadiliko kimfumo, kisha kumbatiza mtu huyo huyo ndani ya dakika thelathini kuwa hakuna hoja ya msingi yenye kuthibitisha tuhuma dhidi yake wakati mleta hoja hizo ndio wewe unaemsafisha kirahisi, hiki ni kitendo cha dharau kubwa sana Kwa waliokiamini chama kuwa kipo kwenye mkakati wa kweli dhidi ya adui mkubwa wa taifa UBADHILIFU/ WIZI/ UFISADI/ RUSHWA.....
HOJA HII YA UFISADI .Bila unafiki wazalendo waliosutwa na nafsi zao waliuona udhaifu wa chama kiasi kikubwa na ndipo wanapokuja na hoja ya kusema kuwa chama ni roporopo kilichokosa ajenda maalumu isipokuwa kupata madaraka tu bila kujali Aina ya siasa ya kumchafua mtu hata Kwa uwongo Tu.....inahitaji limbwata la hali ya juu Sana kuendelea kuamini waropokaji wa chama wanapoleta uropokaji wao dhidi ya mwanasiasa mwezao...Dr. Slaa aliamua kutokuwa mnafiki sambamba na Mzee lipumba...kumbuka wapo waumini wengi Sana waliojiondoa kimya kimya nyakati hizo...
Usimwamini mwanasisa, daima atakuchezesha ngoma Kwa midundo yake atimize adhma yake.
Tanzania bila unafiki haiwezekani hasa Kwa waumini waaminifu wa vyama vyao...mfano mkubwa mmoja Tu unatuonyesha sura zetu halisi ingawa twajificha kwenye kivuli cha siasa ni dynamic....
Sisi tuliompinga mamvi na siasa zake akiwa CCM, tukamuita majina yote na list of shame tukamuweka kinara ndio Sisi tiliodeki barabara na kuzungusha mikono tukidai mabadiliko ni yeye...ajabu sana.... Na ndio Sisi leo tunaemsema amerudi alikotoka, nyakati zote hizi hatuhitaji kutia Uhuru wa fikra zetu Bali mahaba ya itikadi zetu kisiasa.....

Sent using Jamii Forums mobile app

Ninashukuru nimekutia hasira ww na themagufulianzi mpaka mmeamua kuja kwa hamaki. Sasa kwa sababu mmejaa vyema kwenye 18 zangu wacha niwajibu wote kwa pamoja kila mtu atabeba kinachomuhusu. Narudia tena kwamba hoja ya kwamba wapinzani ni watu wa kuropoka ni kwa mujibu wa ccm pindi wanapojitetea kwani huwa wanabanwa na hoja hizo. Kama kuna mwananchi anayemini wapinzani ni watu wa kuropoka hiyo ni haki yake na kwasababu anazoziamini yeye, ni kama ilivyo kwa wapinzani na wananchi wanaomini ccm ni chama cha mafisadi.

Unasema wizi wa ruzuku kuwa tatizo la kitaifa hakuipi cdm haki na yenyewe kuwa wala ruzuku. Cdm pia inaongozwa na binadamu wazuri na wabaya sio chama cha malaika hivyo mapungufu tunayoyaona kwenye taasisi nyingine haishangazi kuona cdm pia yapo. Pia tambua wananchi hawachagui chama cha malaika bali chama kinachowaridhisha. Kama ruzuku inaliwa hatua zichukuliwe na vyombo husika kwa chama chochote bila kuleta mizengwe.

Kuhusu Lowassa kuchafuliwa miaka 8 na hao hao waliomchafua kisha kumsafisha, ukiwa na nafasi pitia post zangu za toka nilipojiunga ndani ya jf nitag popote nilipowahi kumsafisha Lowassa ukipaona naomba nipigwe ban ya maisha. Kosa la viongozi wa cdm kumpokea Lowassa, kumsafisha na kumpa nafasi ya kugombea urais sikuwahi kuunga mkono na wala sintokaa niiunge mkono. Kwamba yeye ni mchafu hilo lilithibitishwa na bunge wakati wa sakata la Richmond lililogharimu uwaziri wake mkuu. Kuna huyo mwenzako anayesema eti watu watano wenye nguvu Lowassa yupo. Ni kweli anaweza kuwa na nguvu ila sio za kisiasa bali za fedha. Kama ni za kisiasa tungemuona akiijenga ccm kama walivyofanya kina Kinana, Nape nk. Au tungeona kuleta mabadiliko ndani ya cdm kwa kuongeza viti vya ubunge, udiwani au hata kufungua matawi mapya ya cdm. Muache kuabudu sanamu.

Watu kujitoa ndani ya taasisi yoyote sio jambo la ajabu, watu huhama dini, vyama, timu za soka nk, la ajabu ni lipi mtu akitoka upinzani? Kama mtu hapo alipo hapati anachokitaka au kaona pengine pazuri au penye fursa kwake utamzuia? Ila ni wendawazimu kanisa la Romani kuonekana halifai na watu kuhama eti kisa kuna mapadre wanalawiti watoto.

Kumuamini mwanasiasa au kutokumuamini huo ni utashi wako wala hakuna anayekuzuia, ila ukweli ulio wazi ni kwamba tunaoongozwa na wanasiasa. Unawaamini au huwaamini hilo utajua ww.

Cc:Themagufulianzi
 
Hivi sisiemu kuna vijana wanaeza kujieleza hivi(kuchambua mada hivi)
Ukiendelea kusoma utawaona humu badala ya kujibu hoja kwa uchambuzi wataishia kumsimanga na kumkandia. Wenye akili watachambua kisomi wajinga wataishia kumzodoa kwakuwa hawana uwezo kitaaluma. Dawa nzuri unapoona huna hoja ni kunyamaza lakini utawaona wakijitutumua kujiaibisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninashukuru nimekutia hasira ww na themagufulianzi mpaka mmeamua kuja kwa hamaki. Sasa kwa sababu mmejaa vyema kwenye 18 zangu wacha niwajibu wote kwa pamoja kila mtu atabeba kinachomuhusu. Narudia tena kwamba hoja ya kwamba wapinzani ni watu wa kuropoka ni kwa mujibu wa ccm pindi wanapojitetea kwani huwa wanabanwa na hoja hizo. Kama kuna mwananchi anayemini wapinzani ni watu wa kuropoka hiyo ni haki yake na kwasababu anazoziamini yeye, ni kama ilivyo kwa wapinzani na wananchi wanaomini ccm ni chama cha mafisadi.

Unasema wizi wa ruzuku kuwa tatizo la kitaifa hakuipi cdm haki na yenyewe kuwa wala ruzuku. Cdm pia inaongozwa na binadamu wazuri na wabaya sio chama cha malaika hivyo mapungufu tunayoyaona kwenye taasisi nyingine haishangazi kuona cdm pia yapo. Pia tambua wananchi hawachagui chama cha malaika bali chama kinachowaridhisha. Kama ruzuku inaliwa hatua zichukuliwe na vyombo husika kwa chama chochote bila kuleta mizengwe.

Kuhusu Lowassa kuchafuliwa miaka 8 na hao hao waliomchafua kisha kumsafisha, ukiwa na nafasi pitia post zangu za toka nilipojiunga ndani ya jf nitag popote nilipowahi kumsafisha Lowassa ukipaona naomba nipigwe ban ya maisha. Kosa la viongozi wa cdm kumpokea Lowassa, kumsafisha na kumpa nafasi ya kugombea urais sikuwahi kuunga mkono na wala sintokaa niiunge mkono. Kwamba yeye ni mchafu hilo lilithibitishwa na bunge wakati wa sakata la Richmond lililogharimu uwaziri wake mkuu. Kuna huyo mwenzako anayesema eti watu watano wenye nguvu Lowassa yupo. Ni kweli anaweza kuwa na nguvu ila sio za kisiasa bali za fedha. Kama ni za kisiasa tungemuona akiijenga ccm kama walivyofanya kina Kinana, Nape nk. Au tungeona kuleta mabadiliko ndani ya cdm kwa kuongeza viti vya ubunge, udiwani au hata kufungua matawi mapya ya cdm. Muache kuabudu sanamu.

Watu kujitoa ndani ya taasisi yoyote sio jambo la ajabu, watu huhama dini, vyama, timu za soka nk, la ajabu ni lipi mtu akitoka upinzani? Kama mtu hapo alipo hapati anachokitaka au kaona pengine pazuri au penye fursa kwake utamzuia? Ila ni wendawazimu kanisa la Romani kuonekana halifai na watu kuhama eti kisa kuna mapadre wanalawiti watoto.

Kumuamini mwanasiasa au kutokumuamini huo ni utashi wako wala hakuna anayekuzuia, ila ukweli ulio wazi ni kwamba tunaoongozwa na wanasiasa. Unawaamini au huwaamini hilo utajua ww.

Cc:Themagufulianzi
Usichokijua ni kwamba unazungumza na mtu ambae kumtia hasira Kwa hizi porojo zako unahitaji uje na idadi kubwa ya waharibu ubongo wenye mantiki, hivyo sio rahisi kama uhisivyo kunitia hasira Kwa hizi porojo unless unajitekenya na kujichekesha kama iilivyo Ada yenu wanasiasa na kujifariji mkidhani mnakamata bongo za kila mja.
Paragraph ya Kwanza Tu Bado unadhihirisha mihemko yako na uropokaji wako uliotukuka,
Nitake radhi Kwa kuniita magufulis, mie sio sehemu ya waabudu wanasiasa na kamwe sitakaa niwe, ni mtu huru ninaeongozwa na utashi wangu binafsi kadri ya mambo yanayodhihirika....usiniunganishe kwenye matimu timu sapoti watu na interest zao sifit huko asilani.
Usisingizie propaganda za CCM ilhali Hakuhitahijiki microscope wala macroscope kuona uroporopo wa wanasiasa wa upinzani ambao hawafahamiki hasa wanataka kipi kifanywe, ndipo mdau kakueleza kuwa mbio zao na wenzao wa CCM ni kutawala Tu ila technique Yao kubwa ni katika kuhubiri uovu ambao ukija upande wao unapakwa rangi rangi na kusifiwa kisiasa unless unajifanya huoni kwakuwa uko upande fulani...
Jifunzeni kutoa maboriti kabla hamjaondoa vibanzi vya wenzenu....Haki yapaswa kudaiwa na wenye mikono Safi..
Issue ya udhaifu kama ni pande zote sasa yanini kuwapigia kelele upande wa pili ikiwa to err is human?
Let them embrace their administration if that being a case, mtanzania asimchague yoyote tuendelee na business as usual coz wote wanakosea kama sehemu ya ubinadamu wao......
Mawazo mbadala, hoja mbadala ya kimfumo utakaobadilisha mfumo tuliouzowea ambao hauonekani kuleta mabadiliko ndicho kinahitajika....pambaneni kuwaboreshea maslahi raia wenu acheni ubinafsi nyie wanasiasa matumbo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kipindi kile cha 2015 .. Ukawa walikuwa kwenye wakati mgumu katika kuchagua jina LA mgombea

hada kati ya Dk na profesa .. Na hata baadhi ya mashabiki na wanachama pia waligawanyika.. Hapo ndipo Mbowe na Maalimu wakafanya maamuzi magumu.. Niliwapongeza sana bila hivyo ukawa ingekufa kabla ya uchaguzi
 
Usichokijua ni kwamba unazungumza na mtu ambae kumtia hasira Kwa hizi porojo zako unahitaji uje na idadi kubwa ya waharibu ubongo wenye mantiki, hivyo sio rahisi kama uhisivyo kunitia hasira Kwa hizi porojo unless unajitekenya na kujichekesha kama iilivyo Ada yenu wanasiasa na kujifariji mkidhani mnakamata bongo za kila mja.
Paragraph ya Kwanza Tu Bado unadhihirisha mihemko yako na uropokaji wako uliotukuka,
Nitake radhi Kwa kuniita magufulis, mie sio sehemu ya waabudu wanasiasa na kamwe sitakaa niwe, ni mtu huru ninaeongozwa na utashi wangu binafsi kadri ya mambo yanayodhihirika....usiniunganishe kwenye matimu timu sapoti watu na interest zao sifit huko asilani.
Usisingizie propaganda za CCM ilhali Hakuhitahijiki microscope wala macroscope kuona uroporopo wa wanasiasa wa upinzani ambao hawafahamiki hasa wanataka kipi kifanywe, ndipo mdau kakueleza kuwa mbio zao na wenzao wa CCM ni kutawala Tu ila technique Yao kubwa ni katika kuhubiri uovu ambao ukija upande wao unapakwa rangi rangi na kusifiwa kisiasa unless unajifanya huoni kwakuwa uko upande fulani...
Jifunzeni kutoa maboriti kabla hamjaondoa vibanzi vya wenzenu....Haki yapaswa kudaiwa na wenye mikono Safi..
Issue ya udhaifu kama ni pande zote sasa yanini kuwapigia kelele upande wa pili ikiwa to err is human?
Let them embrace their administration if that being a case, mtanzania asimchague yoyote tuendelee na business as usual coz wote wanakosea kama sehemu ya ubinadamu wao......
Mawazo mbadala, hoja mbadala ya kimfumo utakaobadilisha mfumo tuliouzowea ambao hauonekani kuleta mabadiliko ndicho kinahitajika....pambaneni kuwaboreshea maslahi raia wenu acheni ubinafsi nyie wanasiasa matumbo.

Sent using Jamii Forums mobile app

Unajua kusoma lakini huelewi, rudia kusoma kama nimekuita themagufulianzi kwenye hiyo paragraph ya mwanzo. Huna ujualo zaidi ya kuleta hadithi mfu. Kama mifumo haiko sawa ibadilishe, sio umekaa pembeni unaagiza kama uko hotellini wali kuku, wali ng'ombe. Maelezo marefu lakini ni ya kufuata mkumbo. Huna lolote unaloongea zaidi ya mahaba yako kuguswa.
 
Trust me, Dr Bashiru or Prof Kabudi wouldn't have done much better analysis than this.
Cream of the crop wa UDSM? A 5th grade elementary school student in America would have done a much better analysis job.

Loyalty To country Alyways,To government When it deserves
 
Unajua kusoma lakini huelewi, rudia kusoma kama nimekuita themagufulianzi kwenye hiyo paragraph ya mwanzo. Huna ujualo zaidi ya kuleta hadithi mfu. Kama mifumo haiko sawa ibadilishe, sio umekaa pembeni unaagiza kama uko hotellini wali kuku, wali ng'ombe. Maelezo marefu lakini ni ya kufuata mkumbo. Huna lolote unaloongea zaidi ya mahaba yako kuguswa.
Aiseeee!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom