Uchambuzi wangu mfupi juu ya Lowassa kurejea CCM

Lowassa kwenda CHADEMA mnazungusha mikoni na kudeki barabarani, lakini akirudi CCM inakuwa nongwa. Halafu mnajidai mnapigania demokrasia, sasa mbona mnakwazika na uamuzi wa Lowassa?
 
Mtu aliyetukanwa kwa miaka 8 kama ni fisadi nguli, Chadema wakazunguka nchi nzima wakiongozwa na mwenyekiti kuaminisha umma wa watanzania kwamba jamaa hafai, kwamba jamaa alitakiwa awe jela na sio katika nafasi ya waziri mkuu, mtu ambaye alkuwepo kwenye list of shame ya mwembe yanga, ghafla tukaambiwa ndio mgombea urais kupitia chadema, tukaambiawa gia imebadilishiwa angani, Je zile tuhuma walisingizia? bora dkt Slaa alibaki na msimamo wake, na kitendo cha kumpoteza dkt slaa was a biggest mistake ever in political arena.
 

Utakuwa unamaanisha Chui tu (Tiger)

Hakuna kosa ambalo Chadema walifanya, Walimchukua Edo ili wapate kura nyingi na washinde uchaguzi, na walishinda....
Mwenye Kosa ni aliyeiba Kura.....

Na option ya Kumchukua Edo Ilipaswa kuwa na plan mezani ya kuwa kama wakiibiwa kura basi chaguo ni kuingia mtaani na kudai haki ambayo ingepelekea serikali ya mseto.....
Lakini hawakutaka kumwaga damu, na hapo ndipo umuhimuhi wa kumchukua Edo ulipoishia......
 
Ukisoma andiko la John. H. Barret linaitwa Individual Goal & Organizational objectives na maandiko yake mengine utafahamu sura ya maamuzi ya Mh.Lowasa kurudi CCM.

Katika maisha ya kila siku, binadamu huwa ana malengo makuu 2 ,moja ni lengo binafsi (Persons goals au individual goals) na malengo ya kitaasisi au malengo ya timu .(organizational goals,au Team goals).

Mfano ,ukiwa katika taasisi utakuwa na malengo binafsi ya kupata kitu ,kupandishwa cheo,heshima,kuwa mchapakazi mzuri na hapo hapo utakuwa na malengo ya kitasisi kusaidia taasisi kukuwa.

Viongozi wengi walio katika vyama vya Siasa wana malengo binafsi ya kuendelea kuwa wanasiasa wazuri pia wana malengo ya kitaasisi ,chama chao kuendelee kukuwa na kushika dola au kiendelee kushika dola.

2015, Mh.Lowasa alihamia Chadema hivyo kuwa mgombea urais kupitia ukawa ,kilichomfanya Mh.Lowasa kuhamia Chadema ni lengo binafsi (Individual goal) la kugombea urais ili kuwa Rais hivyo alihama kutafuta njia ya kutimiza lengo na adhma yake .

Mh.Lowasa hakuwahi kuwa na lengo la kitaasisi (Organizational goal) ambapo ina maana ya lengo la kusaidia chadema kuimarika ,hakuwahi kuwa na lengo hilo ,hii ni tofauti aliyokuwa nayo na viongozi wengine wa chadema ambao walikuwa na malengo 2 ,binafsi na ya kitaasisi.

Ukimsoma John H.Barret anasema "The organization contributes to individual goal attainment" Jumuiya au taasisi inasaidia sana mtu kutimiza lengo binafsi, hivyo alichoamini Mh.Lowasa ni kujiunga chadema (Ukawa) ili lengo lake litimie la kupata urais.

Ni jambo lisilo pingika alileta ushindani mkubwa hadi kufikia kupata kura milioni 6 dhidi ya Mh.Rais Magufuli kura milioni 8 ,kura hizi zilimpa ujasiri wa kuendelea kubaki upinzani huku akirefusha malengo yake ya kugombea urais kufikia 2020.

Kumbuka mahojiano akiwa Nairobi na kituo cha TV (Nation TV)tarehe 16/July/2017.Alisema,

"Watu wengi wananiuliza kuhusu 2020, Jibu ni Moja Tu. NITAGOMBEA"
Edward Lowassa
Nairobi Serena
16 July 2017"

Lakini lazima tufahamu kuwa Siasa hubadilika badilika ,Siasa sio static ! Siasa ni Dynamic ,ni changeable sio unchangeable.

Ukisoma kitabu cha "Political Dynamics " kilichoandikwa na Asmeritic Bier,Richard Hills,Michael Bernard na wenzao utaona walisema kubadilika badilika kwa Siasa kunategemea mahusiano na muingiliano kati ya viongozi wa kisiasa na wananchi (wapiga kura),wananchi wanaweza waza hivi leo ila kesho wakawaza vingine ukabaki unashangaa,wanasema ni vigumu kutabiri ya kesho katika Siasa.
."Political Dynamic determined by interaction between political leaders and voters,it is difficult to predict ".

Kuanzia 2015 kuelekea 2016 mwishoni upepo wa Mh.Lowasa ulikuwa mkubwa ,na yeye bado alikuwa akiamini katika kura milioni 6 alizopata kama mtaji 2020.

Wanachama wa Chadema na ukawa walitokea ghafla kuvutiwa na Mh.Tundulisu kuanzia 2017 kuelekea 2018 ,hasa katika masuala mengi aliyokuwa anayaibua na kuyashikilia ,hivyo upepo wa Mh.Lowasa ukaanza kufifi ndio maana ya Political dynamics.

Hadi changamoto alizopata Tundulisu na hata yeye kufikia waziwazi kusema akipendekezwa anaweza kubali kugombea 2020 ,pia hata wanachama wengi wa chadema wanapendekeza Tundulisu agombee 2020.

Hili ni Jambo ambalo kwa kawaidi moja kwa moja ,lilikuja kusambaratisha malengo ya Mh.Lowasa kugombea Urais 2020.

Lengo binafsi linasifa zake kwanza liwe specific, Mh.Lowasa alitaka kugombea urais (Specific) haoni tena suala hilo ,(Time bound ) alitaka iwe 2020 ,haoni tena ikiwa wengi wanampendekeza Lissu 2020, (Relevant) haoni tena relevance ya lengo lake sababu Kuna mwingine watu wameibuka nae sababu ya mabadiliko ya kisiasa hivyo haoni mbele tena ,(Attainable) ,je lengo hilo la urais angeweza kulitimiza na akapitishwa kura za maoni ,jibu aliona hapana sababu umma wanachama ulibadilika ghafla.

Hivyo hakuwa na chaguo lolote zaidi ya kurudi CCM ,ambapo anahisi atapata kuendelea kupata heshima yake kama waziri mkuu mstaafu ,na kufa akiwa katika chama chake kilichomlea hata kama akiwa mwanachama bila cheo au bila kugombea,kuliko kubaki chama ambacho alihamia tuu kwa lengo moja ambalo hakulipata .

Maamuzi yake yanatoa funzo kwa vyama pinzani kuandaa watu katika ngazi zote ,udiwani,ubunge ,hata urais .Wawe watu wenye malengo 2 ,binafsi na malengo ya kitaasisi (kukuza chama).

Shukrani.

Abdul Nondo.

Abdulnondo10@gmail.com

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante sana mzareendo mwenzetu

In God we trust
 
"Maamuzi yake yanatoa funzo kwa vyama pinzani kuandaa watu katika ngazi zote ,udiwani,ubunge ,hata urais .Wawe watu wenye malengo 2 ,binafsi na malengo ya kitaasisi (kukuza chama)".

Huu ndio ukweli unaowaboa wengi....Hata wewe kitakachokupa shida sana ni mawazo yako ya maendeleo ya kisiasa nchini na ndani ya chama chako CHADEMA ambayo sio malengo halisi ya chama chako kwa sababu kama wenzako wengi wanaokuponda hapa siasa za kipinzani ni more like crusade "unyumbu" na sio kufanya the right thing na kuwa na strategies za kukuza chama na kuiondoa CCM madarakani badala yake tunaishia kwenye kosoakosoa, pingapinga na kujibu maneno ya viongozi wa serikali... Utachoka soon.
Na ndio maana vijana wenye akili ama wanakaa kimya ama kubaki CCM kwakuwa upinzani halisi haupo..
 
Kuanzia 2015 kuelekea 2016 mwishoni upepo wa Mh.Lowasa ulikuwa mkubwa ,na yeye bado alikuwa akiamini katika kura milioni 6 alizopata kama mtaji 2020.

Kama ni mtihani, Mh Lowassa mtihani uliendelea kumshindia hapa.

Nasema uliendelea kumshindia hapo, kwa sababu kampeni alizofanya 2015 ndiko alikoanzia kushindwa. Watu walianza kuona kasoro tokea kwenye kampeni hizo.

Lakini hata baada ya kushindwa kwenye uchaguzi, mchango wake ndani ya CHADEMA haukuonekana ili watu waendelee kuwa na mategemeo naye

'Abdul Nondo'? Ni yule kijana wa Mh Waziri wa Mambo ya Ndani, Madillu, aliyesemekana "Kujiteka huku akinukia manukato"?

Mada yako ni nzuri, na inaonyesha dalili njema za kuitumia vyema elimu unayoipata. Hongera, na ninakutakia mafanikio.
 
Lowasa hana shukrani, watu wamekupa nafasi kutimiza malengo yako binafsi, hata kama hukufanikiwa ilitakiwa japo ulipe fadhira, badala yake kaja na shukrani ya punda ni mateke, na inaonyesha kama angepata hayo madaraka angewageuka chadema, naamini kosa ni kurudia kosa.

Sent using Jamii Forums mobile app
He he he nimecheka! Ulivyoongea kinyonge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom