Uchambuzi wangu mfupi juu ya Lowassa kurejea CCM

Kilichomfanya Lowasa kurudi ccm hujaandika hata kimoja , kwanza ni mbinyo mkali sana kwenye biashara zake na miradi yake ,pili ni kumuokoa mkwewe sioi sumari ,zingine zote ni porojo tu .
 
Kijana wangu Nondo,

Umefanya vema sana kuchambua jambo hili kitaaluma ukitumia nadharia za kutaasisi na kimifumo (Institutional and Organisational Theories) na sio kisiasa (political biasness) kama ilivyozoeleka humu jukwaani. Kwa kufanya hivi umeitendea haki JF kama maskani ya tafakuri tunduizi na wewe mwenyewe kama mtaalamu (mtarajiwa!!) wa sayansi ya siasa.

Hata hivyo ninaona kasoro moja kubwa ambayo inaonekana mara nyingi kwetu sisi watanzania tunapofanya marejeo ya nadharia, vitabu, au makala za kitaaluma katika uwasilishaji wetu: kwamba tunaendeshwa au kutukuza sana fikra na tafakuri za kisomi za wataalamu na waandishi wa nje na haturejei kabisa wataalamu wa ndani hata katika fani kama yako ambayo ina uhusiano mkubwa sana na mazingira na matukio ya kila siku ya kijamii. Utanisahihisha kama siko sahihi, ila dhana hii imejenga fikra kwa watanzania wengi kwamba mtu anapomnukuu msomi/mwandishi/kiongozi mtu fulani wa Ulaya, Amerika, au Mashariki ya mbali, basi mtu huyo huonekana msomi/mjuaji zaidi na anachokiongea kina tija zaidi na hili huonekana sana katika muktadha wa kisasa (ambayo imetawala sana maisha yetu) na wasomi au wanazuoni kama wewe. Nini msingi wa hoja yangu?

Utakubaliana nami kwamba ukisoma nadharia za kitaasisi, mifumo, na oganaizesheni (institutional, systems, and organisational theories), pamoja na mambo mengine, utaona msisitizo wa umuhim wa kuzingatia mazingira halisi au muktadha (context) katika kuchambua, kutafiti, kutafuta maana, na kuchokonoa tafakuri tunduizi zitokanazo na matukio na michakato ya kitaasisi na mifumo: hasa unapotumia dhana za kinadharia (concepts or constructs emerging from theoretical perspectives). Hivyo kwa uchambuzi kama huu ambao umetumia nadharia za kitaasisi, mifumo, na sayansi ya siasa kwa jambo lililotokea katika mazingira yetu, nilitegemea kuona nukuu na rejea za wabobezi wa taalama hizo toka Afrika, Tanzania au chuo chako: na mahususi idara unayosoma. Nadhani idara yako ni moja ya idara zenye wanazuoni bingwa (maprofesa) wa utawala, mifumo, na siasa kuliko nyingine nyingi katika CKD (walifariki,, waliostaafu, walioko kwenye tafiti, na "waliokwenda mjini"). Kwa nini hakuna fikra zao katika uchambuzi kama huu? Ni kwa sababu hatuziamini? Ni kwa sababu hawaandiki vitabu/majarida? Au ni kwa sababu wanachoandika hakina uzito/mashiko?

Nimalize kwa kusema kuwa, pamoja na kwamba hoja yangu imekulenga moja kwa moja katika ulichoandika, haimaniishi nakukosoa wewe binafsi au kukushanbulia, Nimekusudia tu kuleta changamoto na kuibua tafakuri na maswali juu ya nafasi ya wazalisha maarifa katika jamii na mazingira yetu na namna sisi wengine tunavyoheshimu, kuthamini, na kutumia maarifa hayo katika chambuzi zetu, kuibua mijadala na tafakuri tunduizi. Hivyo usisome nilichandika kwa mtizamo binafsi (individual perspective) wenye lengo binafsi (in serving individual goal) bali katika mtizamo wa kimfumo (system perspective) kwa manufaa ya jukwaa (serving a system goal).

Again, hongera kwa kuitendea haki elimu yako. If mentored/ guided, you can make a good researcher /academic.

Mwalimu MM

Ukisoma andiko la John. H. Barret linaitwa Individual Goal & Organizational objectives na maandiko yake mengine utafahamu sura ya maamuzi ya Mh.Lowasa kurudi CCM.

Katika maisha ya kila siku, binadamu huwa ana malengo makuu 2 ,moja ni lengo binafsi (Persons goals au individual goals) na malengo ya kitaasisi au malengo ya timu .(organizational goals,au Team goals).

Mfano ,ukiwa katika taasisi utakuwa na malengo binafsi ya kupata kitu ,kupandishwa cheo,heshima,kuwa mchapakazi mzuri na hapo hapo utakuwa na malengo ya kitasisi kusaidia taasisi kukuwa.

Viongozi wengi walio katika vyama vya Siasa wana malengo binafsi ya kuendelea kuwa wanasiasa wazuri pia wana malengo ya kitaasisi ,chama chao kuendelee kukuwa na kushika dola au kiendelee kushika dola.

2015, Mh.Lowasa alihamia Chadema hivyo kuwa mgombea urais kupitia ukawa ,kilichomfanya Mh.Lowasa kuhamia Chadema ni lengo binafsi (Individual goal) la kugombea urais ili kuwa Rais hivyo alihama kutafuta njia ya kutimiza lengo na adhma yake .

Mh.Lowasa hakuwahi kuwa na lengo la kitaasisi (Organizational goal) ambapo ina maana ya lengo la kusaidia chadema kuimarika ,hakuwahi kuwa na lengo hilo ,hii ni tofauti aliyokuwa nayo na viongozi wengine wa chadema ambao walikuwa na malengo 2 ,binafsi na ya kitaasisi.

Ukimsoma John H.Barret anasema "The organization contributes to individual goal attainment" Jumuiya au taasisi inasaidia sana mtu kutimiza lengo binafsi, hivyo alichoamini Mh.Lowasa ni kujiunga chadema (Ukawa) ili lengo lake litimie la kupata urais.

Ni jambo lisilo pingika alileta ushindani mkubwa hadi kufikia kupata kura milioni 6 dhidi ya Mh.Rais Magufuli kura milioni 8 ,kura hizi zilimpa ujasiri wa kuendelea kubaki upinzani huku akirefusha malengo yake ya kugombea urais kufikia 2020.

Kumbuka mahojiano akiwa Nairobi na kituo cha TV (Nation TV)tarehe 16/July/2017.Alisema,

"Watu wengi wananiuliza kuhusu 2020, Jibu ni Moja Tu. NITAGOMBEA"
Edward Lowassa
Nairobi Serena
16 July 2017"

Lakini lazima tufahamu kuwa Siasa hubadilika badilika ,Siasa sio static ! Siasa ni Dynamic ,ni changeable sio unchangeable.

Ukisoma kitabu cha "Political Dynamics " kilichoandikwa na Asmeritic Bier,Richard Hills,Michael Bernard na wenzao utaona walisema kubadilika badilika kwa Siasa kunategemea mahusiano na muingiliano kati ya viongozi wa kisiasa na wananchi (wapiga kura),wananchi wanaweza waza hivi leo ila kesho wakawaza vingine ukabaki unashangaa,wanasema ni vigumu kutabiri ya kesho katika Siasa.
."Political Dynamic determined by interaction between political leaders and voters,it is difficult to predict ".

Kuanzia 2015 kuelekea 2016 mwishoni upepo wa Mh.Lowasa ulikuwa mkubwa ,na yeye bado alikuwa akiamini katika kura milioni 6 alizopata kama mtaji 2020.

Wanachama wa Chadema na ukawa walitokea ghafla kuvutiwa na Mh.Tundulisu kuanzia 2017 kuelekea 2018 ,hasa katika masuala mengi aliyokuwa anayaibua na kuyashikilia ,hivyo upepo wa Mh.Lowasa ukaanza kufifi ndio maana ya Political dynamics.

Hadi changamoto alizopata Tundulisu na hata yeye kufikia waziwazi kusema akipendekezwa anaweza kubali kugombea 2020 ,pia hata wanachama wengi wa chadema wanapendekeza Tundulisu agombee 2020.

Hili ni Jambo ambalo kwa kawaidi moja kwa moja ,lilikuja kusambaratisha malengo ya Mh.Lowasa kugombea Urais 2020.

Lengo binafsi linasifa zake kwanza liwe specific, Mh.Lowasa alitaka kugombea urais (Specific) haoni tena suala hilo ,(Time bound ) alitaka iwe 2020 ,haoni tena ikiwa wengi wanampendekeza Lissu 2020, (Relevant) haoni tena relevance ya lengo lake sababu Kuna mwingine watu wameibuka nae sababu ya mabadiliko ya kisiasa hivyo haoni mbele tena ,(Attainable) ,je lengo hilo la urais angeweza kulitimiza na akapitishwa kura za maoni ,jibu aliona hapana sababu umma wanachama ulibadilika ghafla.

Hivyo hakuwa na chaguo lolote zaidi ya kurudi CCM ,ambapo anahisi atapata kuendelea kupata heshima yake kama waziri mkuu mstaafu ,na kufa akiwa katika chama chake kilichomlea hata kama akiwa mwanachama bila cheo au bila kugombea,kuliko kubaki chama ambacho alihamia tuu kwa lengo moja ambalo hakulipata .

Maamuzi yake yanatoa funzo kwa vyama pinzani kuandaa watu katika ngazi zote ,udiwani,ubunge ,hata urais .Wawe watu wenye malengo 2 ,binafsi na malengo ya kitaasisi (kukuza chama).

Shukrani.

Abdul Nondo.

Abdulnondo10@gmail.com

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nazidi kuelewa kwanini kuna watu huwa wananasibishwa na kutokuwa raia wa nchi ya Tanganyika. Nadhani wanatumia uwezo wa akili wa mtu. Wakikuona akili zako ni "exceptional" hapo wanakudhania si raia. Raia halisi ni kama akina msiba, slowslow, DAB nk.

Kijana una uwezo mzuri sana wa kujenga hoja na kuchambua mambo.
 
Write your reply...katika jambo ambalo chadema walifanya makosa in kumpokea Lowasa.Hii imewaweka wazi kuwa ni watafuta madaraka na si wapigania haki za wananchi.Chadema walijijenga vyema hasa katika kuwatetea wanyonge,ghafla watu waliowataabisha wananchi wakapokelewa chadema.kimsingi kuna haja yakuwa na chama mbadala cha upinzani kitakacho kuwa na uwezo wa kusimamia maslahi ya Taiga.

Ni kweli hilo la kumpokea Lowassa cdm walichemka. Hebu anzisha chama chako cha upinzani tukione, au unangoja mpaka cdm ige kama wengine wanavyosema? Huwa kuna watu wanasema inabidi vyama vya upinzani vilivyopo vife, kisha kianzishwe chama cha upinzani chenye nguvu, je ni lazima vife ndio hicho chenye nguvu kianze?
 
Lowassa kwenda CHADEMA mnazungusha mikoni na kudeki barabarani, lakini akirudi CCM inakuwa nongwa. Halafu mnajidai mnapigania demokrasia, sasa mbona mnakwazika na uamuzi wa Lowassa?

Cdm wamempiga risasi kwa kurudi ccm? Hapa kinachofanyika ni uchambuzi wa kisiasa kuhusu kuwepo na kuondoka cdm, kila mtu anachangia kwa nafasi yake.
 
"Maamuzi yake yanatoa funzo kwa vyama pinzani kuandaa watu katika ngazi zote ,udiwani,ubunge ,hata urais .Wawe watu wenye malengo 2 ,binafsi na malengo ya kitaasisi (kukuza chama)".

Huu ndio ukweli unaowaboa wengi....Hata wewe kitakachokupa shida sana ni mawazo yako ya maendeleo ya kisiasa nchini na ndani ya chama chako CHADEMA ambayo sio malengo halisi ya chama chako kwa sababu kama wenzako wengi wanaokuponda hapa siasa za kipinzani ni more like crusade "unyumbu" na sio kufanya the right thing na kuwa na strategies za kukuza chama na kuiondoa CCM madarakani badala yake tunaishia kwenye kosoakosoa, pingapinga na kujibu maneno ya viongozi wa serikali... Utachoka soon.
Na ndio maana vijana wenye akili ama wanakaa kimya ama kubaki CCM kwakuwa upinzani halisi haupo..

Bila kupinga maoni yako kwenye post yako, nimecheka sana hiyo paragraph yako ya mwisho. Kwamba kuna vijana wenye akili huamua kukaa kimya au kubaki ccm kwakuwa upinzani halisi haupo. Huenda hujui usemalo au umesema ukionngozwa na itikadi mfu. Mtu ana akili au anaamua kubaki ccm, ila anangoja wenzake waanzishe upinzani halisi ndio ajiunge! Kwanini asitumie hiyo akili yake kuanzisha upinzani halisi? Huko ccm ndio kuna vijana wanachungulia dirishani waone upinzani halisi kisha wahamie. Hilo jukumu la kuanzisha upinzani halisi wamemuachis nani kisha wao waende kujiunga? Huenda una point ila una uwezo mdogo wa kuziwasilisha. Rudi ukazipange upya.

Unasema huyo mleta uzi ana mawazo mazuri lakini atakwamishwa na chama chake kwani hicho chama kwa mujibu wa maelezo yako ni pinga pinga, na kukosoa kauli za viongozi. Huenda una hoja kwenye hili. Lakini Inaonekana unatoa maoni yako kwa kufuata mkumbo kwamba wapinzani wanapinga kila kitu, bila kuonyesha wanaopinga nini na kwanini. Tuko sisi wapinzani huwa tunapinga/ kukosoa na kuonyesha mbadala wa tunachoona ni sawa. Kukosoa kauli za viongozi ni ubinadamu, hukujaanza leo wala jana na hakutakaa kuishe.
 
Laiti EL angejua tulivyopata heka heka kwenye ndoa zetu esp kwa wamama asingefanya haya..watu ilikua ntinti balaa..kwakwel huyu babu sitakuja msamehe..!mie nilijulikana kweli kweli as Ngoyai Daughter😂😂😂waliokuwa kwenye groups za cdm wananijua..nyooooko sana huyu panzi!
 
Bila kupinga maoni yako kwenye post yako, nimecheka sana hiyo paragraph yako ya mwisho. Kwamba kuna vijana wenye akili huamua kukaa kimya au kubaki ccm kwakuwa upinzani halisi haupo. Huenda hujui usemalo au umesema ukionngozwa na itikadi mfu. Mtu ana akili au anaamua kubaki ccm, ila anangoja wenzake waanzishe upinzani halisi ndio ajiunge! Kwanini asitumie hiyo akili yake kuanzisha upinzani halisi? Huko ccm ndio kuna vijana wanachungulia dirishani waone upinzani halisi kisha wahamie. Hilo jukumu la kuanzisha upinzani halisi wamemuachis nani kisha wao waende kujiunga? Huenda una point ila una uwezo mdogo wa kuziwasilisha. Rudi ukazipange upya.

Unasema huyo mleta uzi ana mawazo mazuri lakini atakwamishwa na chama chake kwani hicho chama kwa mujibu wa maelezo yako ni pinga pinga, na kukosoa kauli za viongozi. Huenda una hoja kwenye hili. Lakini Inaonekana unatoa maoni yako kwa kufuata mkumbo kwamba wapinzani wanapinga kila kitu, bila kuonyesha wanaopinga nini na kwanini. Tuko sisi wapinzani huwa tunapinga/ kukosoa na kuonyesha mbadala wa tunachoona ni sawa. Kukosoa kauli za viongozi ni ubinadamu, hukujaanza leo wala jana na hakutakaa kuishe.
Bro naheshimu maelezo yako mazuri ila unajua kuwa upinzani uliobaki ni kuwapoyoka tu... Hii inatunyima trust vijana.. huko kuna demokrasia ya kweli? huko hakuna upigaji wa ruzuku? what abt ukanda kwenye vyeo na teuzi? Hata Lowassa ambaye ni powerful alipofika huko aliona hausiki ama uhusika wake unapwaya...
Yes mnaonesha mbadala..but hiyo sio national strategy ya upinzani kwani muhimu ni kuitoa CCM madarakani na kukuza chama
Rudi kwenye hoja zake za msingi...Maaandalizi ya mgombea, kuhimarisha chama etc
 
Upinzani uliobaki ni wa kuropoka kwa tafsiri ya ccm. Unasema unawanyima trust vijana. Nyie vijana mko kwenye kichaka gani mnasubiri trust kwa wengine? Kwanini vijana msijitokeze mtengeneze upinzani wenu utakaojenga trust? Unasema huko kuna demokrasia ya kweli, demokrasia ipo, kama ni ya kweli au la inategemea utashi wako, haikufai unaweza kuondoka maana chama sio nchi. Upigaji wa ruzuku uko chama chochote na kama ni kipimo basi ccm ni zaidi, huo upigaji ni tatizo letu kama taifa, iwe serekalini, kwenye taasisi za dini, michezo nk.

Unasema hata Lowassa ni powerful, Lowassa hakuwa powerful wala hatakaa awe powerful bali alikuwa anahonga watu kumsifia, hongo hizo alizitoa kwa wapambe wa kisiasa, nyumba za ibada nk. Sijawahi kumuona Lowassa ukiacha alivyokuwa waziri mkuu, akiongea zaidi ya dkt 15 akitoa falsafa zake na kushawishi kwa hoja. Watu wenye uelewa finyu ndio walichezeshwa propaganda za kwamba Lowassa ni powerful kupitia wapambe wake, vyombo vya habari na viongozi wa dini waliokula hela zake. Juu ya hayo hakuna mabadiliko yanaletwa na mtu/mzee aliye above 60yrs hasa mtu huyo awe yuko au ametoka ccm.

Unasema national strategy ya upinzani ni kuitoa ccm kwa hili uko sahihi, kumbuka kuitoa ccm ni ushindani na siku zote kwenye ushindani kuna mshindi na mshindwa. Pia ccm kwa sasa sio chama cha siasa kinachoshindina kisiasa bali ni chama chenye mafungamano na vyombo vya dola, hivyo kukitoa inabidi nguvu ya zaidi ya ushawishi wa kisiasa na box la kura. Hii ni nchi yetu na tunaona kinachoendelea kwenye box la kura jinsi gani taasisi za kimamlaka na vyombo vya dola vinavyoibeba ccm. Maandalizi ya mgombea urais yako vizuri na chama kiko hai hata kama kinafanyiwa hujuma za wazi na rais aliye madarakani. Ukija kujadiliana na mimi hakikisha hubebi hoja za kufuata mkumbo na kuokoteza okoteza maana utapata tabu sana.
 
Upinzani wa kuropoka sio tafsiri ya CCM na Wana CCM pekee bali ni hali halisi ya upinzani wa nchi yetu ukiondoa mahaba yetu ya kutetea vyama vyetu na kutopenda kuzungumziwa tusiyoyapenda...
Upinzani uliojikita kwenye nini kitazungumzwa na serikali au chama tawala ndipo basis ya hoja itokee kwao...hakuna hoja halisi kwa sasa Bali inategemeana na upepo wa siku toka serikalini.
Kwa wauimini wa siasa wasiofungamanishwa na upande katika kujadili hoja zao wanauona ukweli halisi ambao waumini kindakindaki hawawezi ona yasiyowafurahisha daima huona wanayoyataka Tu.
Maoni na hoja mbadala yanahitajika katika kila hoja pingani kutoka upande usiokubaliana....
Wizi wa ruzuku kuwa ni changamoto ya kitaifa haiupi uhalali upinzani unaotarajia kuleta serikali mbadala kuona ni jambo la kuzoeleka...mbadala wa DHAMBI haupaswi kuwa dhambi Bali epuko la dhambi Kwa vitendo....
Kumtangaza mtu miaka zaidi ya nane kuwa ni fisadi papa na nyangumi, Kwa kutumia rasilimali za wazalendo wenye kuona umuhimu wa mabadiliko kimfumo, kisha kumbatiza mtu huyo huyo ndani ya dakika thelathini kuwa hakuna hoja ya msingi yenye kuthibitisha tuhuma dhidi yake wakati mleta hoja hizo ndio wewe unaemsafisha kirahisi, hiki ni kitendo cha dharau kubwa sana Kwa waliokiamini chama kuwa kipo kwenye mkakati wa kweli dhidi ya adui mkubwa wa taifa UBADHILIFU/ WIZI/ UFISADI/ RUSHWA.....
HOJA HII YA UFISADI .Bila unafiki wazalendo waliosutwa na nafsi zao waliuona udhaifu wa chama kiasi kikubwa na ndipo wanapokuja na hoja ya kusema kuwa chama ni roporopo kilichokosa ajenda maalumu isipokuwa kupata madaraka tu bila kujali Aina ya siasa ya kumchafua mtu hata Kwa uwongo Tu.....inahitaji limbwata la hali ya juu Sana kuendelea kuamini waropokaji wa chama wanapoleta uropokaji wao dhidi ya mwanasiasa mwezao...Dr. Slaa aliamua kutokuwa mnafiki sambamba na Mzee lipumba...kumbuka wapo waumini wengi Sana waliojiondoa kimya kimya nyakati hizo...
Usimwamini mwanasisa, daima atakuchezesha ngoma Kwa midundo yake atimize adhma yake.
Tanzania bila unafiki haiwezekani hasa Kwa waumini waaminifu wa vyama vyao...mfano mkubwa mmoja Tu unatuonyesha sura zetu halisi ingawa twajificha kwenye kivuli cha siasa ni dynamic....
Sisi tuliompinga mamvi na siasa zake akiwa CCM, tukamuita majina yote na list of shame tukamuweka kinara ndio Sisi tiliodeki barabara na kuzungusha mikono tukidai mabadiliko ni yeye...ajabu sana.... Na ndio Sisi leo tunaemsema amerudi alikotoka, nyakati zote hizi hatuhitaji kutia Uhuru wa fikra zetu Bali mahaba ya itikadi zetu kisiasa.....

Unasema hata Lowassa ni powerful, Lowassa hakuwa powerful wala hatakaa awe powerful
Hapa ndio mwisho wangu wa kusoma.... Kama unabisha hili tunajadili nini sasa?
Kalala CCM kaamkia chadema na ugombea uraisi.. na kakimbiza nchi nzima ukamwite sio powerful?? Am lost bro
Leo hii ukiandika list ya watu powerful Tanzania no matter yuko chama gani usipomuweka Lowassa katika top 5 unatatizo
 
Upinzani wa kuropoka sio tafsiri ya CCM na Wana CCM pekee bali ni hali halisi ya upinzani wa nchi yetu ukiondoa mahaba yetu ya kutetea vyama vyetu na kutopenda kuzungumziwa tusiyoyapenda...
Upinzani uliojikita kwenye nini kitazungumzwa na serikali au chama tawala ndipo basis ya hoja itokee kwao...hakuna hoja halisi kwa sasa Bali inategemeana na upepo wa siku toka serikalini.
Kwa wauimini wa siasa wasiofungamanishwa na upande katika kujadili hoja zao wanauona ukweli halisi ambao waumini kindakindaki hawawezi ona yasiyowafurahisha daima huona wanayoyataka Tu.
Maoni na hoja mbadala yanahitajika katika kila hoja pingani kutoka upande usiokubaliana....
Wizi wa ruzuku kuwa ni changamoto ya kitaifa haiupi uhalali upinzani unaotarajia kuleta serikali mbadala kuona ni jambo la kuzoeleka...mbadala wa DHAMBI haupaswi kuwa dhambi Bali epuko la dhambi Kwa vitendo....
Kumtangaza mtu miaka zaidi ya nane kuwa ni fisadi papa na nyangumi, Kwa kutumia rasilimali za wazalendo wenye kuona umuhimu wa mabadiliko kimfumo, kisha kumbatiza mtu huyo huyo ndani ya dakika thelathini kuwa hakuna hoja ya msingi yenye kuthibitisha tuhuma dhidi yake wakati mleta hoja hizo ndio wewe unaemsafisha kirahisi, hiki ni kitendo cha dharau kubwa sana Kwa waliokiamini chama kuwa kipo kwenye mkakati wa kweli dhidi ya adui mkubwa wa taifa UBADHILIFU/ WIZI/ UFISADI/ RUSHWA.....
HOJA HII YA UFISADI .Bila unafiki wazalendo waliosutwa na nafsi zao waliuona udhaifu wa chama kiasi kikubwa na ndipo wanapokuja na hoja ya kusema kuwa chama ni roporopo kilichokosa ajenda maalumu isipokuwa kupata madaraka tu bila kujali Aina ya siasa ya kumchafua mtu hata Kwa uwongo Tu.....inahitaji limbwata la hali ya juu Sana kuendelea kuamini waropokaji wa chama wanapoleta uropokaji wao dhidi ya mwanasiasa mwezao...Dr. Slaa aliamua kutokuwa mnafiki sambamba na Mzee lipumba...kumbuka wapo waumini wengi Sana waliojiondoa kimya kimya nyakati hizo...
Usimwamini mwanasisa, daima atakuchezesha ngoma Kwa midundo yake atimize adhma yake.
Tanzania bila unafiki haiwezekani hasa Kwa waumini waaminifu wa vyama vyao...mfano mkubwa mmoja Tu unatuonyesha sura zetu halisi ingawa twajificha kwenye kivuli cha siasa ni dynamic....
Sisi tuliompinga mamvi na siasa zake akiwa CCM, tukamuita majina yote na list of shame tukamuweka kinara ndio Sisi tiliodeki barabara na kuzungusha mikono tukidai mabadiliko ni yeye...ajabu sana.... Na ndio Sisi leo tunaemsema amerudi alikotoka, nyakati zote hizi hatuhitaji kutia Uhuru wa fikra zetu Bali mahaba ya itikadi zetu kisiasa.....

Sent using Jamii Forums mobile app
yani umemaliza maelezo boss.... mwenye mahaba ya kisiasa hawezi kuona hili
 
Ukisoma andiko la John. H. Barret linaitwa Individual Goal & Organizational objectives na maandiko yake mengine utafahamu sura ya maamuzi ya Mh.Lowasa kurudi CCM.

Katika maisha ya kila siku, binadamu huwa ana malengo makuu 2 ,moja ni lengo binafsi (Persons goals au individual goals) na malengo ya kitaasisi au malengo ya timu .(organizational goals,au Team goals).

Mfano ,ukiwa katika taasisi utakuwa na malengo binafsi ya kupata kitu ,kupandishwa cheo,heshima,kuwa mchapakazi mzuri na hapo hapo utakuwa na malengo ya kitasisi kusaidia taasisi kukuwa.

Viongozi wengi walio katika vyama vya Siasa wana malengo binafsi ya kuendelea kuwa wanasiasa wazuri pia wana malengo ya kitaasisi ,chama chao kuendelee kukuwa na kushika dola au kiendelee kushika dola.

2015, Mh.Lowasa alihamia Chadema hivyo kuwa mgombea urais kupitia ukawa ,kilichomfanya Mh.Lowasa kuhamia Chadema ni lengo binafsi (Individual goal) la kugombea urais ili kuwa Rais hivyo alihama kutafuta njia ya kutimiza lengo na adhma yake .

Mh.Lowasa hakuwahi kuwa na lengo la kitaasisi (Organizational goal) ambapo ina maana ya lengo la kusaidia chadema kuimarika ,hakuwahi kuwa na lengo hilo ,hii ni tofauti aliyokuwa nayo na viongozi wengine wa chadema ambao walikuwa na malengo 2 ,binafsi na ya kitaasisi.

Ukimsoma John H.Barret anasema "The organization contributes to individual goal attainment" Jumuiya au taasisi inasaidia sana mtu kutimiza lengo binafsi, hivyo alichoamini Mh.Lowasa ni kujiunga chadema (Ukawa) ili lengo lake litimie la kupata urais.

Ni jambo lisilo pingika alileta ushindani mkubwa hadi kufikia kupata kura milioni 6 dhidi ya Mh.Rais Magufuli kura milioni 8 ,kura hizi zilimpa ujasiri wa kuendelea kubaki upinzani huku akirefusha malengo yake ya kugombea urais kufikia 2020.

Kumbuka mahojiano akiwa Nairobi na kituo cha TV (Nation TV)tarehe 16/July/2017.Alisema,

"Watu wengi wananiuliza kuhusu 2020, Jibu ni Moja Tu. NITAGOMBEA"
Edward Lowassa
Nairobi Serena
16 July 2017"

Lakini lazima tufahamu kuwa Siasa hubadilika badilika ,Siasa sio static ! Siasa ni Dynamic ,ni changeable sio unchangeable.

Ukisoma kitabu cha "Political Dynamics " kilichoandikwa na Asmeritic Bier,Richard Hills,Michael Bernard na wenzao utaona walisema kubadilika badilika kwa Siasa kunategemea mahusiano na muingiliano kati ya viongozi wa kisiasa na wananchi (wapiga kura),wananchi wanaweza waza hivi leo ila kesho wakawaza vingine ukabaki unashangaa,wanasema ni vigumu kutabiri ya kesho katika Siasa.
."Political Dynamic determined by interaction between political leaders and voters,it is difficult to predict ".

Kuanzia 2015 kuelekea 2016 mwishoni upepo wa Mh.Lowasa ulikuwa mkubwa ,na yeye bado alikuwa akiamini katika kura milioni 6 alizopata kama mtaji 2020.

Wanachama wa Chadema na ukawa walitokea ghafla kuvutiwa na Mh.Tundulisu kuanzia 2017 kuelekea 2018 ,hasa katika masuala mengi aliyokuwa anayaibua na kuyashikilia ,hivyo upepo wa Mh.Lowasa ukaanza kufifi ndio maana ya Political dynamics.

Hadi changamoto alizopata Tundulisu na hata yeye kufikia waziwazi kusema akipendekezwa anaweza kubali kugombea 2020 ,pia hata wanachama wengi wa chadema wanapendekeza Tundulisu agombee 2020.

Hili ni Jambo ambalo kwa kawaidi moja kwa moja ,lilikuja kusambaratisha malengo ya Mh.Lowasa kugombea Urais 2020.

Lengo binafsi linasifa zake kwanza liwe specific, Mh.Lowasa alitaka kugombea urais (Specific) haoni tena suala hilo ,(Time bound ) alitaka iwe 2020 ,haoni tena ikiwa wengi wanampendekeza Lissu 2020, (Relevant) haoni tena relevance ya lengo lake sababu Kuna mwingine watu wameibuka nae sababu ya mabadiliko ya kisiasa hivyo haoni mbele tena ,(Attainable) ,je lengo hilo la urais angeweza kulitimiza na akapitishwa kura za maoni ,jibu aliona hapana sababu umma wanachama ulibadilika ghafla.

Hivyo hakuwa na chaguo lolote zaidi ya kurudi CCM ,ambapo anahisi atapata kuendelea kupata heshima yake kama waziri mkuu mstaafu ,na kufa akiwa katika chama chake kilichomlea hata kama akiwa mwanachama bila cheo au bila kugombea,kuliko kubaki chama ambacho alihamia tuu kwa lengo moja ambalo hakulipata .

Maamuzi yake yanatoa funzo kwa vyama pinzani kuandaa watu katika ngazi zote ,udiwani,ubunge ,hata urais .Wawe watu wenye malengo 2 ,binafsi na malengo ya kitaasisi (kukuza chama).

Shukrani.

Abdul Nondo.

Abdulnondo10@gmail.com

Sent using Jamii Forums mobile app
Lissu aliwahi kutuambia kuwa Chadema ilifanya utafiti wake kwa kuwatumia wazungu na waliogopa kuwatumia watanzania wasije wakawadanganya na wale watafiti waliwajibu Chadema ili malengo ya Chadema yatimie ya kushika Dola lazima wampate Mh Lowasa.

Hivyo japo Lowasa aliamini lazima awe Rais wa Tanzania pia haindoi ukweli kuwa Chadema nao waliona 2015 lazima waishike nchi..! Tena imani hii kwao kwa 2015 ilikuwa kubwa kwa Mh Lowasa kuliko imani waliyokuwanayo 2020.

Lowasa hakuiwezesha Chadema kushika Dola lakini tusijidanganye leo hii kuwa ata viti vya ubunge walivyopata Chadema ni baada ya upepo kubadilika kwa ujio wa Lowasa Chadema.

Ujio wa Lowasa ndani ya Chadema lilikuwa lengo la Taasisi na Lengo lake Lowasa binafsi.
 
Upinzani wa kuropoka sio tafsiri ya CCM na Wana CCM pekee bali ni hali halisi ya upinzani wa nchi yetu ukiondoa mahaba yetu ya kutetea vyama vyetu na kutopenda kuzungumziwa tusiyoyapenda...
Upinzani uliojikita kwenye nini kitazungumzwa na serikali au chama tawala ndipo basis ya hoja itokee kwao...hakuna hoja halisi kwa sasa Bali inategemeana na upepo wa siku toka serikalini.
Kwa wauimini wa siasa wasiofungamanishwa na upande katika kujadili hoja zao wanauona ukweli halisi ambao waumini kindakindaki hawawezi ona yasiyowafurahisha daima huona wanayoyataka Tu.
Maoni na hoja mbadala yanahitajika katika kila hoja pingani kutoka upande usiokubaliana....
Wizi wa ruzuku kuwa ni changamoto ya kitaifa haiupi uhalali upinzani unaotarajia kuleta serikali mbadala kuona ni jambo la kuzoeleka...mbadala wa DHAMBI haupaswi kuwa dhambi Bali epuko la dhambi Kwa vitendo....
Kumtangaza mtu miaka zaidi ya nane kuwa ni fisadi papa na nyangumi, Kwa kutumia rasilimali za wazalendo wenye kuona umuhimu wa mabadiliko kimfumo, kisha kumbatiza mtu huyo huyo ndani ya dakika thelathini kuwa hakuna hoja ya msingi yenye kuthibitisha tuhuma dhidi yake wakati mleta hoja hizo ndio wewe unaemsafisha kirahisi, hiki ni kitendo cha dharau kubwa sana Kwa waliokiamini chama kuwa kipo kwenye mkakati wa kweli dhidi ya adui mkubwa wa taifa UBADHILIFU/ WIZI/ UFISADI/ RUSHWA.....
HOJA HII YA UFISADI .Bila unafiki wazalendo waliosutwa na nafsi zao waliuona udhaifu wa chama kiasi kikubwa na ndipo wanapokuja na hoja ya kusema kuwa chama ni roporopo kilichokosa ajenda maalumu isipokuwa kupata madaraka tu bila kujali Aina ya siasa ya kumchafua mtu hata Kwa uwongo Tu.....inahitaji limbwata la hali ya juu Sana kuendelea kuamini waropokaji wa chama wanapoleta uropokaji wao dhidi ya mwanasiasa mwezao...Dr. Slaa aliamua kutokuwa mnafiki sambamba na Mzee lipumba...kumbuka wapo waumini wengi Sana waliojiondoa kimya kimya nyakati hizo...
Usimwamini mwanasisa, daima atakuchezesha ngoma Kwa midundo yake atimize adhma yake.
Tanzania bila unafiki haiwezekani hasa Kwa waumini waaminifu wa vyama vyao...mfano mkubwa mmoja Tu unatuonyesha sura zetu halisi ingawa twajificha kwenye kivuli cha siasa ni dynamic....
Sisi tuliompinga mamvi na siasa zake akiwa CCM, tukamuita majina yote na list of shame tukamuweka kinara ndio Sisi tiliodeki barabara na kuzungusha mikono tukidai mabadiliko ni yeye...ajabu sana.... Na ndio Sisi leo tunaemsema amerudi alikotoka, nyakati zote hizi hatuhitaji kutia Uhuru wa fikra zetu Bali mahaba ya itikadi zetu kisiasa.....

Sent using Jamii Forums mobile app

Dr. Slaa hakutoka cdm kwa utashi wake. Sote tunajua mazingira yalivyokuwa na mengine siyo busara hata kujadili hadharani. Yameshapita hayo tugange yajayo. Ya Lipumba ndiyo kabisa hatuhitaji hata kujadili kwani kila mtu anaona kwa macho yake kazi aliyopewa. Kifupi, Nyerere's country is gone to the dogs, period!
 
Back
Top Bottom