Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,547
- 41,059
TLS imefanya kazi kubwa ya kupitia kipengere kimoja kimoja cha Mkataba kati ya Tanzania na kampuni ya DP World ya Dubai. Taarifa hiyo imeaimisha kinagaubaga maeneo yote ya hovyo, ikaelezea madhara yanayoweza kutokea mkataba usipobadilishwa, na pia imetoa mapendekezo ya nini kifanyike.
Jambo moja kubwa na la msingi, ni kwamba imethibitika wazi kuwa watu wenye uwezo wa kuchambua mambo, watu wenye weledi, wenye upeo na akili kubwa, watu wenye uzalendo na walio wakweli wapo nje ya Serikali na nje ya Bunge.
Hoja zote ambazo watu mbalimbali walizionesha kama ni kasoro kubwa kwenye mkataba huu, zimeonekana pia ndani ya report ya uchambuzi ya hawa wataalam wasomi wa sheria.
TLS ndiyo chombo kikubwa kuliko vyote nchini mwetu kuhusiana na mambo yanayogusa sheria. Kwa sababu kinawakilisha wanataaluma wote wa masuala ya sheria. Wanasheria wote, pamoja na mwanasheria mkuu, ni wanachama wa TLS. Hivyo kauli rasmi ya TLS, inafuta kauli zote za wanasheria wote, pamoja na mwanasheria mkuu, zilizo tofauti na report hii.
Report hii inathibitisha kuwa sisi tuliopaza sauti, tena siyo wanasheria, tulikuwa sahihi. Na watetezi wote wa ule mkataba, ama wamekosa uelewa, au wamepofushwa na rushwa, au wamekosa uzalendo, au wamekula njama na DP ili kuiangamiza nchi.
Tunaomba TLS watoe nakala ya report hii itakayokuwa kwa lugha ya Kiswahili. Na kisha zitolewe nakala nyingi, ambazo mtu yeyote ataweza kuzinunua. Tununue nakala hizo na kuwapelekea wananchi wetu, tuzisambaze kwa wingi, hasa kwa wale ambao hawana uwezo wa kuzifikia. Lengo ni kuhakikisha wananchi wanatambua tuna watu wa namna gani huko Bungeni, na ndani ya Serikali.
Wananchi wawasute wabunge, waeleze kwa nini waliidhinisha mkataba wa hovyo na wa kuliangamiza Taifa wa kiwango hiki.
Kwa hiki kilichotokea, hakuna imani kabisa juu ya mikataba mingine iliyosainiwa huko Uarabuni. Tunaambiwa ilisainiwa mikataba 30. Je, tuna uhakika gani na hiyo mingine siyo ya hovyo kama huu au hata kuwa mibaya zaidi ya huu?
Habari zaidi, soma: