Mr mutuu
JF-Expert Member
- Jan 27, 2023
- 2,000
- 9,940
Wasaalam,
Kila siku tumekua tukisema hakuna kitu kibaya kama kufanya mikataba ya kisirisiri, tatizo Hili kubwa halipo kwenye mpira tu Bali hata kwenye mikataba ya kiserikali, wananchi ndio tuna dhamana na nchi yetu na ndio walipa Kodi lakini watu wachache wanaingia mikataba au mikopo kisirisiri bila kuwapo na uwazi hata kidogo, utaskia tumeingia mkataba na nchi flani wenye dhamani ya trillion kadhaa, au tumechukua mabilioni kadhaa ya mkopo kutoka nchi flani huku sisi walipaji wa Hio mikopo hatujui vipengele Wala masharti ya mkopo huo
Tukirudi kwenye swala la Yanga, Mimi napenda kua neutral kwenye swala Hili, sielewi nani hasa ndio mwenye makosa kati ya club au Sportpesa!
Siri ambayo wengi hawaijui ni kua kwenye mashindano ya CAF yoyote, iwe CAF champions league au CAF confederation cup Simba SC au Yanga SC hawawezi kuitumia logo ya mdhamini wao mkuu Sportpesa!
Hii inatokana na kua muandaaji wa mashindano hayo 'CAF' tayari ana mkataba na kampuni ya kubet kutoka Russia 1xbet kama mmoja wa official sponsors wa michuano yoyote ya CAF! Kwa io huyu 1xbet ni part wa main sponsors kama walivyo Total energies!
Mkataba ambao 1xbet waliingia na CAF ni kua hakuna timu inayodhaminiwa na kampuni yoyote ya betting itatumia logo ya kampuni hizo kwenye michuano ya CAF ndio maana tunaona Simba SC alikua anatumia 'Visit Tanzania' kwenye michuano ya CAF..
Sportpesa sio wageni kwenye migogoro hii maana mwaka 2019 utata ulianza pale club ya Gor mahia walipozuiliwa kuitumia logo ya Sportpesa aliyekua mdhamini wao kipindi hicho, hii ilitokana na malalamiko kutoka 1xbet kua hataki Kuona wapinzani wake(kampuni za kubet) wakijibrand kupitia michuano anayoidhamini.. kitu kilochopelekea Gor mahia kucheza mechi ya marudio na zamalek na shirt zisizokua na logo mechi iliyofanyika Kenya na Gor mahia kushinda goli 4-2
Gor mahia alitafuta wadhamini wengine bila mafanikio ikabidi wawe wanacheza mechi zao bila kutumia logo yoyote!
Wachezaji wa Gor mahia kwenye michuano ya ndani
Wachezaji wa Gor mahia kwenye michuano ya CAF
Swali ninalojiuliza.. kama Sportpesa walikua wameshawahi kupitia mgogoro huu 2019, mpaka Leo kwenye mkataba wao na Yanga au Simba Hilo swala watakua hawakuliweka sawa ili kuzuia Hili liliotokea sasa ivi? Au Kuna loopholes waliziacha Yanga wakaliona Hili wakaamua kupitia hapohapo
Kuna mtu atauliza mbona mechi za mtoano kama Yanga aliocheza na Al hilal mbona walitumia logo ya Sportpesa, jibu ni kua hizo mechi CAF Hana mamlala nazo na ndio maana hata haki za matangazo ya kurusha mechi alikua anamiliki timu ya nyumbani,
Kuna nchi kama Austria ambao wanaruhusu sponsor mbalimbali kwa timu Moja ila wakienda kucheza UEFA basi inawabidi wawe na sponsor mmoja tu kwa jersey
hao ni wachezaji wa timu Moja 'wien' ya Austria wakiwa wamevaa shirt zenye sponsor tofauti
Nimeleta hii ili mjue kua swala la sponsor kwenye shirt Kila nchi Ina makubaliano yake, ila ukienda kwenye michuano flani basi lazima ufuate Sheria za huko! Mfano kama england wao wanatumia sponsor mmoja tu kwenye mashindano yote! Mwaka 2010 Kuna timu iliomba kua na sponsor tofauti, yaani epl wamtumie huyu na fa wamtumie mwingine ila wakakataliwa maana Sheria Kule zipo wapi sponsor mmoja kwa mashindano yote
Ukakasi unakuja Yanga hawezi kuvaa logo ya Sportpesa kwenye CAF, Yanga nao hawataki kuvaa visit Tanzania kama ambavyo Sportpesa walidhani, sijajua kwanini ila nahisi Itakua mambo ya ki maslahi tu maana sidhani kama Simba alivaa Bure pia, kama hawakusema walipewa chochote basi Kuna watu walipiga pesa hapa, maana Kuna kitengo Cha kutangaza utalii kina bajeti zake kubwa tu, rejea Rwanda wanalipa mabilioni kwa arsenal na psg wakivaa 'visit Rwanda'
Sababu kubwa ya epl kukataa timu kuvaa logo tofauti hata kwenye michuano ya kimataifa ni kua italeta ukakasi sana! Na Hili ndo litakuja kujitokeza kwa Yanga! Mfano Yanga wanavyofanya promotion zao au wakihudhuria shughuli nyingine za kijamii watatumia shirt zenye logo ipi? Tumeshaona jersey zenye logo nyingine zishaanza kuuzwa Hili nalo halijakaa sawa kwa Sportpesa kibiashara!!
Rushwa kwa wachezaji itajipenyeza kwa Kasi maana Kila kampuni sasa kati ya Sportpesa au haier italazimika kuwahonga either wachezaji au watu wenye influence kuzivaa jezi zenye logo zao wakiwa hawapo uwanjani au kuzipost kwenye social media ili wajitangaze zaidi
CAF wao hawawezi kumpangia Yanga logo atayovaa kama Haingilii maslahi Yao na kama hajavunja masharti na mdhamini wao Sportpesa! Sasa na jukumu la Yanga na Sportpesa kuacha usiri na kutuambia 'live' je mkataba baina Yao unasemaje? Kama Sportpesa walijua Yanga hawezi kuvaa logo yao kimataifa je walimbana asije akavaa nyingine?au wali assume atavaa visit Tanzania kama Simba so hawakuligusia Hili?kama walijisahu basi Hio ni loophole Yanga atakua kapita nayo
Ifike muda waweke usiri pembeni waletee mikataba mezani tujue kipi ni kipi, maana wananchi washaanza kununua jersey ili Hali Kuna Hali ya sintofahamu