Uchambuzi Game kati Yanga

Dalton elijah

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
216
478
✍🏻Mamelodi leo walionesha kitu ambacho mara nyingi wanakionesha Brighton ( kwenye build up ) kipi hiko ?Kukuvuta uende kuwafanyia pressing ( Baiting the press ) na kwanini hivyo ?

1: Ni kwamba wanapasiana taratibu nyuma pasi fupi fupi dhamira yao uende ukawafanyie pressing ili space ifunguke nyuma yako washambulie nyuma ya kiungo chako , pasi mbili au tatu wanakusalimia

2: Wanakuwa mabeki wawili nyuma , viungo wawili mbele yao huku fullbacks wakiwa wanatanua uwanja kwenye mstari wa mmoja na viungo wawili , huku GK anakuwa kama option ya ziada wakitaka pasi ya mbele

✍🏻Lakini Yanga wao wakasema " No thank you " huo mpira kaeni nao huko kwenu hatuji kufanya pressing , Yanga walitengeneza midblock nzuri ya 4-4-2 ( walikabia katikati zaidi na wala sio chini wala juu sana ) kuwanyima space za ndani ya Mamelodi jumlisha kazi nzuri ya Maxi na Musonda kwenye ku track back kuhakikisha fullbacks wao wasiwe wazi peke yao . Game Plan 🤝

✍🏻Kwa kipindi cha kwanza tu pekee ilihitaji hivi vitu viwili goli lipatikane

1: Makosa makubwa ya kiulinzi kwa timu zote mbili
2: Ubora wa mchezaji mmoja kuamua ( individual brilliance )

✍🏻Kipindi cha pili kuna muda kama wa dakika 20 au 15 fulani hivi , timu zote mbili ziliamua kufunguka na kupishana hapo spaces zilianza kufunguka , runners wakaanza kupata spaces , pasi za mbele zilianza kuonekana , kilichokosekana :-

1: Mamelodi pasi yao ya mwisho ilikosekana
2: Yanga maamuzi sahihi , either pasi au umaliziaji

✍🏻kwenye uzuiaji timu zote zilikuwa tofauti kwenye muundo wao

: Mamelodi walichagua kukabia juu hasa pale wakipoteza mpira ( counter pressing )

: Yanga kufunga spaces wakiwa ndani : na wote ( Mamelodi na Yanga walifanikiwa kwenye mipango yao )

NOTE

1: Kwenye mechi kama hizi ukipata nafasi inabidi uwe mfanisi maana hutopata nyingi ( Mzize dakika za mwanzo na kipindi cha pili ) kwa level hii zile nafasi nzuri

2: Mudau kwenye 1v1 utakesha 😀🔥

3: Kekana mtulivu sana anacheza kwa hesabu

4: Muda na Mkude kwenye kiungo wamejituma mno hutakiwi kusinzia

5: Maxi kipindi cha kwanza , good game

6: Magolikipa wawili : Sweeper GKs , Passers : Diarra na Williams 🔥

FT: Yanga SC 0-0 Mamelodi
 
Yanga walipaswa wapate walau goli 1, ingekuwa mtaji mzuri sana kwao...

Anyway tusubiri second game...
 
wale shoe shiners wako tu overrated hamna kitu pale, ngoja tukawakande moja, wakirudisha tunakaba mpaka tunapita kwa faida ya goli la ugenini
Na wanakuzwa sana na Masandawane wa kisiwandui na hapa Kisuji Dar.
FB_IMG_1711864710612.jpg
 

Attachments

  • FB_IMG_1711864710612.jpg
    FB_IMG_1711864710612.jpg
    43.3 KB · Views: 2
Uchambuzi mzuri, japo naona Doarra hana footwork nzuri kwenye distribution.
 
Kuna mpuuzi mmoja humu baada ya mechi na azam alianza kuwaaminisha watu kua Gamondi sio kocha ni tapeli tu.
Yule jamaa laiti Yanga ingepotezea jana lazima leo angeanzisha uzi wa kukanyagia, wabongo nyoso.
Hao ni makolo wananhangaika zaidi na yanga kuliko timu Yao.
 
Back
Top Bottom