Uchambuzi wa Habari: Gazeti Uhuru linapofichua njama za kufunika 'madudu' ya Ekelege wa TBS! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchambuzi wa Habari: Gazeti Uhuru linapofichua njama za kufunika 'madudu' ya Ekelege wa TBS!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Feb 26, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Feb 26, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  Mhariri wa gazeti la Uhuru anaitwa Jaqueline Liana. Hakika anastahili pongezi kwa kazi yake njema kwa taifa. Niweke wazi, katika magazeti yote niliyoyapitia siku ya jana Jumamosi, gazeti la Uhuru ndilo kwangu lilitia fora.

  Kati ya habari kadhaa zenye kumfumbua macho msomaji, gazeti Uhuru lilibeba habari tatu zenye umuhimu mkubwa kwa nchi yetu; habari kuu ilikuwa na kichwa cha habari; " Ripoti uozo TBS yavaiva- Njama za kuizima zaandaliwa". Nyingine ni; " Majengo ya UDA kuhifadhi makontena". Na mwisho ni wito; "Tumieni mitandao ya kijamii kuhabarisha". Habari hizo mbili za mwisho nitazichambua katika siku za usoni kutokana na ufinyu wa muda kwa sasa.

  Nianze basi na habari kuu iliyotokana na uchunguzi wa gazeti Uhuru; Mwandishi anabainisha, kuwa taarifa ya uozo wa ndani ya Shirika la Viwango Tanzania ( TBS) imekamilika na imewasilishwa kwa Spika wa Bunge kwa hatua zaidi.

  Kwamba wakati ripoti hiyo ikiwa tayari na huku Watanzania wakisubiri hatua gani zitachukuliwa, gazeti Uhuru limebaini uwepo wa mipango kabambe inayosukwa ili kuzima na kuwalinda vigogo wa shirika hilo la umma wanaotuhumiwa kufanya mambo kinyume na taratibu.

  Uhuru linabainisha, kuwa Kamati ya Bunge ya Mahesabu ya Mashirika ya Umma ( POAC) imebaini matatizo mengi ndani ya TBS yakiwemo ukaguzi wa bidhaa usiokidhi viwango na mazingira ya rushwa miongoni mwa maofisa waandamizi. Na kutokana na kubainika kwa madudu hayo, Kamati hiyo imependekeza baadhi ya maofisa waandamizi wa TBS, akiwemo Mkurugenzi Mkuu, Charles Ekelege, wasimamishwe kazi kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.

  Na licha ya Kamati ya Bunge kukamilisha ripoti yake hiyo, uchunguzi uliofanywa na gazeti la Uhuru unaonyesha kuwa kuna mipango inasukwa kwa kuwahusisha baadhi ya wabunge, ofisi ya bunge na wizara ya Viwanda na Biashara kuhakikisha suala hilo halifikishwi katika mkutano ujao wa bunge na kuchukuliwa hatua.

  Uchunguzi wa gazeti Uhuru unazidi kuonyesha , kuwa wahusika wa mpango huo ni baadhi ya wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ( PAC) na maofisa wa bunge kwa kushirikiana na maofisa waandamizi wa wizara.

  Kwa mujibu wa gazeti Uhuru, mmoja wa wajumbe wa POAC alithibitisha kuwepo mipango hiyo na kuongeza kuwa, baadhi ya wabunge wanatumiwa katika suala hilo.

  Mjumbe mwingine wa kamati hiyo alisema, kwa uozo ndani ya TBS uko wazi kwa sababu hata wafanyakazi wa chini wamekuwa wakilalamika kuwa wanakwamishwa kufanya kazi ipasavyo na viongozi wao.

  " Wafanyakazi walitueleza kuwa wanapogundua kuna bidhaa mbovu na kuzizuia, wafanyabiashara wanazungumza moja kwa moja na viongozi wa juu wa shirika na matokeo yake bidhaa zile ambazo ni mbovu zinaruhusiwa kutumika.

  " Kama watu walioaminiwa na kupewa nafasi kuongoza shirika kubwa kama hili wanakiuka utaratibu, kuna imani gani tena? Hii inaonyesha watu hawa hawana nia njema na maisha yetu na wako tayari kuwaangamiza Watanzania kwa sababu ya maslahi yao". Alisema mjumbe huyo.

  Kwa mujibu wa gazeti Uhuru, Makamu wa Mwenyekiti wa kamati hiyo ya bunge , Mbunge wa Ludewa , Deo Filikunjombe, ameweka bayana msimamo wa kamati yake, kuwa hawatakubali suala hilo kuzimwa au kumalizwa kinyemela kwa sababu kufanya hivyo ni kukubali Watanzania waendelee kuangamia kwa kutumia bidhaa mbovu.

  Filikunjombe anasema;

  " Upo ushahidi kwamba zipo bidhaa zisizo na viwango kama kondomu, mafuta ya kupikia, matairi, vyakula na blue band ambazo zina nembo ya TBS na zinatumika. Huu ni uoza mkubwa, ni lazima tufike mahali tuseme basi. Ni lazima TBS isafishwe na wahusika wa mchezo huu mchafu lazima waondolewe haraka". ( Deo Filikunjombe, Uhuru Februari 25, 2012)

  Naam, kila Mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi yake hana budi kuwaunga mkono wahariri wa mfano wa Jacqueiline Liana na wabunge wa mfano wa Deo Filikunjombe. Ni Watanzania wenzetu walioonyesha utayari wa kujitoa muhanga kuipigania nchi yao dhidi ya vitendo vya kifisadi kama hiki cha TBS chenye hatari ya kuliangamiza taifa.
   
 2. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  moja ya mambo ya kipuuzi na ya kijinga kutoka kwa mjengwa ni hili la leo.

  Unampongeza mwanahabari kwa yeye kukumbuka weledi wa kazi yake?

  Anapoandika maslai ya walaji wakuu mbona huwa hauumpi pongezi?kama jana kama leo,mwandishi anatakiwa aandike kwa manufaa ya taifa.Ni wazi umetambua ya kuwa huwa haandiki au gazeti la uhuru haliandiki kwa faida ya umma.

  Nakupa pole kwa kujua kuwa huwa hawaandiki kwa manufaa ya waliwaji bali kwa manufaa ya walaji wakuu.
   
 3. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Waweza kuwa uchambuzi yakinifu lakini kama wahusika hawafanyii kazi matatizo ya mashirika yetu,itakuwa ni sawa na kuendeleza wimbo wetu"yaliyopita si ndwele tugange yajayo" na kila kitu kikaishia hapo.
   
 4. Mtanzania haswa

  Mtanzania haswa JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 665
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Majid asante kwa kutumegea kipande hicho kutoka gazeti kongwe uhuru mimi mala ya mwisho kulisoma gazeti hilo ni kipindi mzee wangu analinunua na mimi kulikuta nyumbani miaka ya 90
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Ekerege atalindwa kwa nguvu zote maana waliomuweka wanajua anafanya nini pale ingawa huwa wanajisahau na kutojua wajibu wao...kumtoa ngumu kama mama ndalichako!!
   
 6. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,601
  Likes Received: 2,458
  Trophy Points: 280
  Inawezekena hii ikawa ni moja ya habari ya mwaka kutolewa na uhuru. Itoshe kusema kuwa nchi hii imekosa viongozi waadilifu, wenye upendo, wazalendo, wenye kuweka mbele maslahi ya watz na taifa kwa ujumla. Endapo inafikia hatua ya kuingiza sokoni bidhaa zisizo na viwango na kwa vyovyote vile hii ni sumu, je tunakwenda wapi tz? Endapo inathibitika kuwa kuna watumishi waliohusika na mpango huu je hawa si ni wauwaji kabisa. Naumia sana
   
 7. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #7
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Good Avatar

  [​IMG]


  kwenye marketing techniques Uhuru wabadili jina la gazeti na style......mwandishi katika hili nampa heko!!
   
 8. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,782
  Likes Received: 36,777
  Trophy Points: 280
  Kwa siku moja hili gazeti linauzwa nakala sii zaidi ya 100 tz nzima.
  Wasomaji wa gazeti hili ni watanzania wachache waliojivua ufahamu.
   
 9. only83

  only83 JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Sijaelewa na nimeona uvivu kusoma yote hii habari...nimehisi haina tija,ni kama ya kuipa promo ligazeti la uhuru...
   
 10. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #10
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280

  if they were astray is it wrong for them to come on in the correct path??
   
 11. m

  mchukiaufisadi JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 538
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Ekerege atalindwa kama Erio William Mkapa wa PPF anavyolindwa na Serikali. Erio kafisadi kumzidi hata aliyemtangulia David Mattaka, lakini haguswi lakini Mattaka yupo matatani.


   
 12. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #12
  Feb 26, 2012
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Majid nakupongeza kwa kuliona hili na kutoa pongezi kwa waandishi husika-tukijenga tabia hii ya kusifia pale mtu anapofanya tendo la kishujaa na tukaponda pale anapokosea tutakuwa tunaplay our part.Wengi wetu tuna tabia ya kuchambua hoja kwa kumuangalia mtoaji na sio mantiki ya hoja yenyewe hili nadhani si sahihi.
   
 13. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #13
  Feb 26, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,032
  Likes Received: 7,434
  Trophy Points: 280
  Imekuwa ni jambo la kusikitisha sana kwa muda mrefu kwa gazeti kongwe la uhuru, ambalo ukilikuta linauzwa barabarani au vibandani heading zake huwa zimegeuzwa chini juu, ishara ya kuwa wauzaji wanatambua kuwa halina soko na wamekubali kuingia nalo sokoni kwa malipo maalum toka kwa wamiliki.

  Itakuwa ni proud ya kipekee kama limeamua kujivua hadhi ya kuwa chombo cha ki propaganda cha chama tawala, na kuanza kufanya kazi kwa maslah ya taifa.
   
 14. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #14
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Mimi sijawahi kununua au kusoma gazeti la uhuru tangu mfumo wa vyama vingi uanze kwa sababu ya propaganda za kijinga gazeti hili linazobeba. Ila kama wamejirekebisha na kuanza kuandika mambo ya maslahi kwa umma na si kwa chama cha magamba, watanipata na nitasoma habari zao. Tofauti yangu na watu wengine pamoja na kuishi kijijini huwa sinunui gazeti bali nanunua habari
   
 15. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #15
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Wana JF kuna mipango inasukwa kwa kuwahusisha baadhi ya wabunge, ofisi ya bunge na wizara ya Viwanda na Biashara kuhakikisha suala TBS halifikishwi katika mkutano ujao wa bunge na kuchukuliwa hatua.

  wahusika wa mpango huo ni baadhi ya wabunge ambao ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ( PAC) na maofisa wa bunge kwa kushirikiana na maofisa waandamizi wa wizara.

  Mbunge wa Ludewa , Deo Filikunjombe, ameweka bayana msimamo wa kamati yake,kuhusu sakata la TBS kuwa hawatakubali suala hilo kuzimwa au kumalizwa kinyemela kwa sababu kufanya hivyo ni kukubali Watanzania waendelee kuangamia kwa kutumia bidhaa mbovu.

  Filikunjombe anasema;
  ” Upo ushahidi kwamba zipo bidhaa zisizo na viwango kama kondomu, mafuta ya kupikia, matairi, vyakula na blue band ambazo zina nembo ya TBS na zinatumika. Huu ni uoza mkubwa, ni lazima tufike mahali tuseme basi. Ni lazima TBS isafishwe na wahusika wa mchezo huu mchafu lazima waondolewe haraka”.


  Uhuru Februari 25, 2012
   
 16. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #16
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Smartness ya uhuru newspaper inapimwa kwa makala ya Jaqueline Liana?
  Mjengwa kapotea njia.
   
 17. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #17
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Mkuu hata genius hupongezwa anapofanya vizuri ingawa tayari watu huwa tunajua yeye ni genius, khaaaaaaaaaa! Una chuki wewe!
   
 18. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #18
  Feb 26, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,032
  Likes Received: 7,434
  Trophy Points: 280
  Kwani hapo tatizo liko wapi? Je kama makala za gazeti husika ilikuwa ni sehemu ya indicators zake katika kupima ubora?
  Vp kama indicator hiyo imefanya vizuri na kulipa credibilties uhuru? Ulitaka afiche matokeo?
   
 19. M

  Martinez JF-Expert Member

  #19
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 518
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  Its such a good move !
  But mostly its an implication. An implication that the hyenas are eating themselves!
   
 20. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #20
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Ni vizuri kuwataja wabunge hao ili tuwajue,tofauti na hapo ni majungu
   
Loading...