Uchambuzi huru: Jakaya Kikwete anafuata nyayo za Rais Vladimir Putin?

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Rais wa sasa wa Urusi ndugu Vladimir Putin alihakikisha anatimiza ndoto yake ya kudumu ndani ya ikulu ya Moscow kwani aliamini kuwa bila yeye Urusi itayumba!

Ili kutokuvunja katiba ya Urusi, kijanjajanja alimpachika mtu wake Dmitry Medvedev kuwa rais kwa kipindi kimoja ili atakapogombea tena asiambiwe kuwa amevunja katiba ya Urusi kwa kugombea awamu tatu mfululizo! Ili kuzuia hilo, alijipa uwaziri mkuu kisha akamuweka mtu awe rais wa Urusi ambaye alikuwa huyo Dmitry Medvedev. Hata hivyo, kipindi cha utawala wa Dimitry, Vladimir Putin ndiye aliyekuwa akiiwakilisha ikulu ya Moscow kwenye vikao mbalimbali na hasa ndiye alikuwa msemaji mkuu wa dola la Urusi kimataifa! Baada ya utawala wa Dmitry Medvedev, bwana Putin alirejea katika usukani wake wa kuitawala tena ikulu ya Moscow kwa awamu nyingine mbili kama rais! Hakuulizwa kwani alikidhi vigezo vyote vya kugombea achilia mbali kuwahi kuitawala Urusi kwa miaka kumi hapo kitambo kidogo!

Tanzania tunaye rais mstaafu wa awamu ya nne ndugu Jakaya Kikwete! Mbali na kuwa na rais wa nchi John Magufuli, Kikwete ndiye amekuwa kioo cha nchi kimataifa!

Kikwete ameshafanya vikao vitatu ndani ya nchi kuisemea Tanzania kimataifa, vivyo hivyo
vikao vitatu nje ya nchi ambapo viwili barani Afrika na kimoja ulaya!

Mbali na ukweli kuwa Kikwete hatarajii tena kurejea katika ikulu ya Dar es Salaam kama Putin wa Russia, lakini anatoa tafsiri ya walakini kwa rais Magufuli. Kiukweli inaonekana kuwa rais Magufuli ama ameonyesha wazi kuwa na uwezo mdogo kuiwakilisha Tanzania kimataifa au ana matatizo ya kusafiri umbali mrefu kama inavyosemwasemwa! Ila kwa kiongozi mkuu wa nchi, hii inatoa tafsiri ambayo siyo nzuri na inafifisha nguvu ya utawala wa Magufuli!
 
Aah wapi JK IQ yake iko chini mno huwezi kulinganisha na mtu smart kama Puttin. Puttin anajenga hoja, anatetea hoja hata kama ni kosa. Kwenye tatizo Puttin ana show up na kutumia kama opportunity kujijenga. JK hana substance ni mipasho tu. Kukitokea tatizo anaingia mitini, akibanwa sana analaumu washauri wake.Labda kama ni Puttin wanna be zaidi ya hapo atabaki kuwa mzee wa starehe na mipasho.
 
Jakaya Mrisho Kikwete,ni nikiongozi shupavu mwenye maono,uwezo wake namlinganisha na J.K.Nyerere.
 
Rais wa sasa wa Urusi ndugu Vladimir Putin alihakikisha anatimiza ndoto yake ya kudumu ndani ya ikulu ya Moscow kwani aliamini kuwa bila yeye Urusi itayumba!

Ili kutokuvunja katiba ya Urusi, kijanjajanja alimpachika mtu wake Dmitry Medvedev kuwa rais kwa kipindi kimoja ili atakapogombea tena asiambiwe kuwa amevunja katiba ya Urusi kwa kugombea awamu tatu mfululizo! Ili kuzuia hilo, alijipa uwaziri mkuu kisha akamuweka mtu awe rais wa Urusi ambaye alikuwa huyo Dmitry Medvedev. Hata hivyo, kipindi cha utawala wa Dimitry, Vladimir Putin ndiye aliyekuwa akiiwakilisha ikulu ya Moscow kwenye vikao mbalimbali na hasa ndiye alikuwa msemaji mkuu wa dola la Urusi kimataifa! Baada ya utawala wa Dmitry Medvedev, bwana Putin alirejea katika usukani wake wa kuitawala tena ikulu ya Moscow kwa awamu nyingine mbili kama rais! Hakuulizwa kwani alikidhi vigezo vyote vya kugombea achilia mbali kuwahi kuitawala Urusi kwa miaka kumi hapo kitambo kidogo!

Tanzania tunaye rais mstaafu wa awamu ya nne ndugu Jakaya Kikwete! Mbali na kuwa na rais wa nchi John Magufuli, Kikwete ndiye amekuwa kioo cha nchi kimataifa!

Kikwete ameshafanya vikao vitatu ndani ya nchi kuisemea Tanzania kimataifa, vivyo hivyo
vikao vitatu nje ya nchi ambapo viwili barani Afrika na kimoja ulaya!

Mbali na ukweli kuwa Kikwete hatarajii tena kurejea katika ikulu ya Dar es Salaam kama Putin wa Russia, lakini anatoa tafsiri ya walakini kwa rais Magufuli. Kiukweli inaonekana kuwa rais Magufuli ama ameonyesha wazi kuwa na uwezo mdogo kuiwakilisha Tanzania kimataifa au ana matatizo ya kusafiri umbali mrefu kama inavyosemwasemwa! Ila kwa kiongozi mkuu wa nchi, hii inatoa tafsiri ambayo siyo nzuri na inafifisha nguvu ya utawala wa Magufuli!

Huu ni upuuzi.
 
Magufuli anajenga nchi kwanza, hata wewe una haki ya kuisemea nchi kimataifa popote upatapo fursa.
 
Acha tu aende maana hakuna namna nyingine

Kama mkuu hawezi kwenda na aende tuu
 
Back
Top Bottom