'Suala la wizi wa kura kwa chaguzi za visiwani huwa si la kujadiliwa ama kuumiza vichwa sana, kwani linatambulika. Na mpaka kesho sijajua wale jamaa waliokimbia na maboksi ya kura mwaka 2000 na kwenda kubadili matokeo porini wamechukuliwa hatua gani!
Tungepata ufumbuzi wa hili suala tata nadhani tungekuwa na nafasi nzuri zaidi ya kuchambua suala hili. Mlio na taarifa za suala hili tunaziomba.'
IDIMI umenifanya nicheke saaana mkuu. Lile changa la macho tu, kuonyesha jamaa wapo makini na uchanguzi, jamaa ni wao wenyewe na walipanga nao. Watu wale wapo mitaani kama kawaida hawaijui Jela wala Rumande. (kinyume chake wanasifiwa kwa kufanikisha kazi waliyotumwa).
Maalim Seif alianzia mbali katika kupandikiza mbegu mbaya ambayo kwa sasa anaijutia. Tokea akiwa waziri wa elimu katika SMZ aliweza kubagua wananchi wa visiwa hivyo na aliendelea hata alipokuwa waziri kiongozi. Fainali ni pale alipoanza kampeni zake kabla hata ya mfumo wa vyama vingi kuingia tz.
Kauli za nchi ilipinduliwa na haiwezi kutolewa kwa makaratasi, ni maneno ya kwenye maskani na baraza za kahawa. Iwapo mwakilishi alisema hivyo katika kikao cha Baraza la Wawakilishi huo utakuwa ni utashi wake binafsi... kwani huko kuna mengi ya kushangaza, kuna mwakilishi mmoja aliitaka wizara ya Utalii kuwapaka kobe rangi, ili waweze kuvutia zaidi watalii.
Wizi wa kura visiwani upo si kwa CUf wala CCM, wote wamekuwa wakitumia njia chafu katika kupata ushindi. wanacuf wengi hupiga kula zaidi ya kituo kimoja... 2000 wakati CCM ikiwaajili wanajeshi wa SMZ kwa kuwafungulia makambi huko Pemba, CuF wao waliwapakia watu kibao toka Tanga na Mombasa kwenye majahazi kenda kupiga kura.
Maalim Seif kwa upande wa siasa za visiwani ndie mhusika mkuu wa fujo zote baada ya chaguzi, kwa madai ya kuibiwa kura(inawezekana ni kweli). Njia ambayo anatumia kufikisha ujumbe kwa wafuasi na wapenzi wa chama chake imejaa shari hivyo kuwafanya wafuasi wake wawe washari vilevile, huku yeye katulia tuli nyumbani kwake mtoni.
1995 alijitangaza kuwa ndie mshindi wa uprez, masaa 24 kabla ya matokeo rasmi kutoka, matokeo yake yakawa ni vujo mitaani. Haya tumeona vile vile mwaka jana huko Kenya.
2000, mapema alishasema kuwa hatokubaliana na matokeo ya uchaguzi, hata kabla ya yeye mwenyewe kwenda kupiga kura, kauli hii iliwajaza jazba wafuasi wake na kusababisha vujo.
Mara zote baada ya makesheshe huja na kuwatuliza wafuasi wake kwa kuwataka wavute subira na kujiandaa na chaguzi zinazokuja. Hii inaonyesha wazi jinsi anavyozikilizwa vema na wanachama wake. Hivyo basi ni yeye mwenye uwezo wa kuzuia ama kuleta vujo hapo 2010
Hakuna la kufanyika Zanzibar ni moyo wa CCM liwalo na liweko lakini upinzani kushika dola ya Zanzibar ni mwiko,hilo mkae na kulijua.
Mtu wa Pwani hayo sio maelezo mepya, Ni mambo yaliyotokea huko visiwani. Mwaka 1995, CCM ilishangazwa sana na wingi wa kura walizopata CUF na wingi wa viti katika Baraza la Wawakilishi. Hawakutegemea hayo kwani walitegemea nguvu za Marehemu Dr Omar Ali Juma angeweza kuvuta jamaa wengi wa kisiwa cha pili, hata hivyo ilikuwa ni kinyume chake. Marehemu huyo sana sana aliweza kuwaondoa Wapemba wengi hasa wale wafanyakazi SMZ toka CCM kwenda CUF, hii ilitokana na hotuba zake...kibunango hapa umetupa maelezo mepya maalim
mie sina uhakika kama kuna wanaotoka tanga na mombasa kupigia kura cuf, ila haya huenda ni sawa na siasa inayotokea huko kenya kila kundi kujenga hoja kuwa wenzao ndio wizi.
mzee kibunango una maana dr omar alikuwa akiifanyia kazi CUF?
pili unataka kunithibitishia wote CCM na CUF wanacheza rafu, ila huyu mmoja akizidiwa ndio hupiga kelele?
sasa jee nn kifanyike ili tuweze kufanya uchaguzi usio na mizengwe nakila chama kiuze sera na wananchi waamue kwa kupiga kura tu
Naam... Dr.Omar alichangia sana bila yeye kujua hilo. Kila mkutano wa kampeni aliohotubia uliondoa wapemba wengi ndani ya CCM. Mwingine aliyekuwa akichochoea ni yule ndumila kuwili Awesu Dadi.
Ni ukweli usiofichika kuwa CCM na CUF ni wacheza rafu kubwa katika chaguzi na hasa za visiwani. Wanaibiana ujuzi, mipango na mikakakati ya ushindi, kwani kila chama kina watu wake ndani ya chama kingine.
Cha kufanya sasa, kwanza ni kwa Wanzej wote kukubali kuwa wao ni wamoja,dhihaka ya upemba,unyamwezi,ungazija na mengine yawe historia. Ni kazi kubwa lakini ni lazima ifanywe.
Maalim Seif aombe sahamani kwa kuwa na sera ya utengano kwa wazenj wote.
Wenye ushawishi mkubwa na mapenzi ya wengi wawe tayali kukubali yanayofanywa na wengine katika kuleta maendeleo. Mfano Maalim Seif awe anakubali juhudi za dhati zinazofanywa na chama tawala, hali kadhalika chama tawala kipokee kwa dhati mapendekezo ya kimaendeleo toka CUF.
Wapemba wa waunguja wengi wamehusiana ni vema wakaanza kuondoa tofauti zao kisiasa ndani ya nyumba zao. Hii itasaidia kujenga taifa linaloangalia sera na sio chama.
SMZ chini ya idara ya utumishi iache tabia ya kuchunguza sana waombaji waliofuzu katika fani zao kama wamehusu kisiwa cha pili. Uwezo, ujuzi na taaluma vime ndio vigezo pekee katika kuajili na sio vinginevyo.
Aidha idara zingine zote zenye ukuritimba dhidi ya kundi au kabila fulani viache kufanya hivyo.
Zanzibar wakubali kuwa ndio Mji mkuu wa visiwa hivi. Hivyo wame tayali kupokea wahamiaji bila kuwadhihaki.
Sheria na Katiba ya nchi zifuatwe ipasavyo na sio kupindishwa kwa manufaa ya kundi fulani.
Vyama vyote vya Siasa viheshimu Mapinduzi ya mwaka 1964. Mapinduzi hayo ndio yaliyotufikisha hapa tulipo tukiwa vifua mbele kuringia Uzenj. Kwa kufanya hivyo kutaondoa misuguano ambayo ipo muda mrefu kiasi kwa sasa imekuwa kama ni silaha dhidi ya vyama vingine.
Mapinduzi hayo yamemsaidia nini kijana aliyezaliwa mwaka 1970 ambaye hana kazi, hana shamba na anaishia kuwa juha kwenye nchi yake?
Wazenji wanaotembea vifua mbele wako wangapi? Siku itafika mtakuja ondoka tu, mpende msipende. Ile ni nchi ya kila mtu na japo huko nyuma mlifanikiwa
kuiba kura, itafika siku wananchi watachukua mapanga kuwatoeni kama walivyomtoa mwarabu.