Uchaguzi Zanzibar itakuwaje 2010?

Uchaguzi Zanzibar itakuwaje 2010?

(1) Kusimamishwa kugombea kwa tiketi ya CCM inategemea na nani kati yao ni mfusi wa MTANDAO.

(2) Kuchaguliwa kuwa rais wa zanzibar itategemea serikali ya CCM inafanya nini katika kipindi cha miaka mitatu ijayo; so far hawajafanya la maana sana miaka miwili iliyopita.
 
Sidhani kama ni busara kufikiri CCM ndiyo itakayoendelea kuongoza mwaka 10 ijayo. Tunajua kabisa kunamaongezi yanayoendelea kati ya makatibu wa kuu wa CUF na CCM. Maongezi haya yanaweza kuwa na tafsi nyingi, lakini kwangu nachohisi ni kwamba CCM ishagundua nguvu ya CUF ccm, na ikiachwa bila kuratibiwa hata watumie nguvu vipi, uchaguzi wa 2010 wanaweza wakashidwa. So, what they play is politics, perhaps of manipulation or deception, for wider democracy or to safeguard the interest of the party!
 
mtumwitu.......

mie naona ipo haja ya CCM kuanza kubadilisha katiba ili angalau rais awe anakaa miaka 7 badala ya mitano,kuhusu suala la znz mie naona kuepusha majungu,mizozo na mvutano bora RAIS KARUME aendelee na kipindi cha tatu.

naomba kutoa hoja!!!!!!!!
 
Ni wakati watanzania tubadilike
maana sijui ni kigezo gani kinatumika hapa. Je hoja ni nani anaweza kuipeleka Zanzibar mbele au ni nani Mzanzibari "popular".

Naomba ninukuu msemo wa mtaalamu wetu wa mpira kuwa "some people are very popular outside the pitch but in the pitch nothing" the same kwenye uongozi lazima tujue kuwe some people are very popular but in leadership nothing.

Iwe zanzibar iwe zanzibar iwe tanzania kwa ujumla tunahitaji watu wa kutoa dira ya kwenda mbele. Tunahitaji watu ambao watakuwa na uwezo wa kufokasi mbele aone mwaka 2010, 2015, ........ na kusimamia utekelezaji wa mambo ya sasa. Sio hawa watu wa kusubiri jambo limetukia ndio wanaliona na kuanza kulishughulikia kama wanazima moto?

Mimi hii listi naona ni listi ya watu maarufu, umaarufu unaweza kutumika katika chama kuangalia nani wasimsimamishe kuwa mgombea wao kwani malengo ya chama ni tofauti na malengo ya watanzania. Malengo ya chama ni kuchukua serikali na hivyo chama kikiona kina mtu mwenye uwezo wa kuongoza nchi na kuiletea maendeleo lakini uwezekano wake wa kusimama katika kiti cha uraisi na akashinda ni mdogo watamuacha na kumsimamisha mtu ambaye anaweza kushinda uchaguzi na kukiletea chama ushindi ingawa mtu huyo haweza kuleta mabadiliko katika nchi.
Kwa watanzania malengo yetu ni maendeleo hivyo nani awe raisi si yule maarufu bali yule anayeweza kutuletea maendeleo
 
Salim sidhani kama ana hamu ya kugombea Zenji especially baada ya kitendo walichomfanya Chimwaga. Mwinyi,Bilal,Shamhuna/Khatibu mmoja wao hao atateuliwa, kuhusu Shein sijui ngoja niulize hivi cheo kipi kikubwa umakamu wa muungano ama urais wa zanzibar? lol with that in mind I dont think he will run for it.
 
MwanaSiasa,
Manano haya nayakubari moja kwamoja;

Fact or myth? You cannot predict the unpredictable; politics is an unpredictable game, don't accept CCM propaganda uncritically!

Lakini yanategemeo wewe umeyazungumza ukiwa unaangalia eangle ipi!
Unajua mimi nashangazwa kabisa na mitazamo yetu kuhusu ili swala,nilikua natemea kama watu tulio kua na siasa za mlengo tofautu na siasa za CCM,tosinge zama sana kwenye nani watamchagua kwani kama tunavyo changia kwenye mada nyingine hawa watu wote ni wamoja mradi anatoka CCM basi hakutakua na jipwa.
Kuvunjika moyo na kutowazungumzia wapinzani kabisa ni sawa na kujiweka upande wa hawa mabwana wakubwa,kauri za "Bilal au Mwinyi,ndio wanao kubarika"ni sawa na kuanza kuchochea moto uliokwisha zimika.

CCM,kama chama wanatumia system walio jingea ku-propagete mawazo kama haya (propaganda) ambayo yana inclination mawazo ya watanzania kama walivyo fanya kwenye Uchaguzi wa mwaka 2005.Wengi tunakumbuka maneno yale ya "Chaguo la Mungu,Chagua la Baba wa Taifa,Kipenzi cha watu na mengi neyo mengi amboyo kwa elimu walio kua nayo waTZ wengi tayari wanashindwa kua na maamuzi binasfi,wan amuaku-side na maneno au slogan hizo ambozi zinakua si kweli.
 
Taifa hili ni la watanzania wote hivyo ni bora tukawaangalia pia Seif .na Juma Duni pia .
 
Taifa hili ni la watanzania wote hivyo ni bora tukawaangalia pia Seif .na Juma Duni pia .

Mk

umeeleza vyema kuwa Taifa hili ni la Watanzania wote sasa nashangaa ulivyomalizia

Tanzania haikamiliki kwa kuongeza hao watu wawili uliowataja kwenye listi
bali tunaweza kuwajumuisha watanzania tukibainisha sifa za mtu anayefaa na sio kutaja majina kwani hatuwezi kuwataja watanzania wote na sio watanzania wote wanafaa kwa nafasi hiyo na inawezekana majina yanayotajwa si kwa vigezo vya sifa za nafasi bali vigezo vingene.
 
JE,
Nimekusoma hapo.
Unajua lazima tuwe mfano wakuto kubaguana katika itikadi zetu.
 
jamani nimeanza kujiuliza masuali mengi baada yaliotokea kwa ndugu zetu wa kenya.

hivi sasa kuna mazungumzo ya muafaka baina ya CUF na CCM ili kuweka hali nzuri na itayoondosha mapungufu yaliojitokeza ktk chaguzi tatu zilizopita.

mara zote baada ya uchaguzi juhudi mbali mbali zilichukuliwa ili kuondosha manun'guniko au kuweka hali ya uwazi ktk uchaguzi, ila la kushangaza hali bado haijatengamaa.

maana kila kukikaribia huzuka mapya ambayo hugharimu gharama kubwa za watu na mali.

sasa huu ni mwaka 2008 na tumebakisha miaka miwili kufikia uchaguzi, hadi sasa hata huo muafaka hujafikiwa.

maana kwanza wafikie kisha upitishwe kwenye baraza la wakilishi kisha utengezwe sheria kwa baadhi ya vipengele ya waliokubaliana.
baada ya hapo kuanze utekelezaji wa muafaka wenyewe.

wasi wasi wangu mkuu jee muda uliobaki utakidhi haja ya kurekebisha hayo watayokubaliana. na jee kama hawatofikia huo muafaka hali itakuwaje?

na kama watafikia lkn muda wa kurekebisha mapungufu ukiwa mdogo hali itakuwaje?

jee zanzibar mara hii itavuka na hali ambayo imeshazoeleka kuwa kila uchaguzi baadhi ya watu wawe kafara kwa wengine kutawala nchi?

nnapenda kuchokoza mjadala huu.

nnategemea tutaujadili kwa kuzingatia tusipojadili leo kabla ya madhara kutofika itakuwa tumeweza kusaidia kurekebisha

na tusiwe kama watu wa kusadikika hutafuta fimbo baada ya kuumwa na nyoka
 
Hakuna la kufanyika Zanzibar ni moyo wa CCM liwalo na liweko lakini upinzani kushika dola ya Zanzibar ni mwiko,hilo mkae na kulijua.
 
awali ya yote maalimu seif atashiriki?

unanifurahisha sana, nimecheka saaana.

naona maalim seif keshakuwa mtu mzima sasa sijui kama ataamua kuwa mlezi kama wazee wenziwe kina shaaban khamis mloo, mheshimiwa ali haji pandu au ndio mzee ataendelea kugombea mpaka aingie ikulu au aingie kaburini.

ila suali si muhimu nani anagombea, bali vipi tutaweza kurekebisha hio hali.

au mkuu haya yanatokea kwa kuwa maalim seif anagombea?

dua kwa hiyo tutarajie yanayotokea kenya baada ya miaka miwili yatarejea kule nyumbani au vp?
 
Maalim Seif kwa upande wa siasa za visiwani ndie mhusika mkuu wa fujo zote baada ya chaguzi, kwa madai ya kuibiwa kura(inawezekana ni kweli). Njia ambayo anatumia kufikisha ujumbe kwa wafuasi na wapenzi wa chama chake imejaa shari hivyo kuwafanya wafuasi wake wawe washari vilevile, huku yeye katulia tuli nyumbani kwake mtoni.

1995 alijitangaza kuwa ndie mshindi wa uprez, masaa 24 kabla ya matokeo rasmi kutoka, matokeo yake yakawa ni vujo mitaani. Haya tumeona vile vile mwaka jana huko Kenya.

2000, mapema alishasema kuwa hatokubaliana na matokeo ya uchaguzi, hata kabla ya yeye mwenyewe kwenda kupiga kura, kauli hii iliwajaza jazba wafuasi wake na kusababisha vujo.

Mara zote baada ya makesheshe huja na kuwatuliza wafuasi wake kwa kuwataka wavute subira na kujiandaa na chaguzi zinazokuja. Hii inaonyesha wazi jinsi anavyozikilizwa vema na wanachama wake. Hivyo basi ni yeye mwenye uwezo wa kuzuia ama kuleta vujo hapo 2010
 
kwa hio madai kuwa zake zinaibiwa hazina ukweli?

na jee kama yeye akiacha kugombea jee tume itakuwa huru na jee yeye hatoweza kuingilia ikiwa mgombea nwao atashindwa?
 
Mbegu aliyopanda Maalim, ni mbaya mno. Hata kama hatogombea malalamiko hayatoweza kwisha. Kwani jamaa wa kisiwa cha pili wanaamini kuwa wao ni wengi na wanaweza kushinda chaguzi yoyote ile hapo kisiwani.

Kwa upande mwingine, kinachoangaliwa sasa huko visiwani ni mashindano kati ya kisiwa cha pili na kisiwa cha kwanza, nani zaidi? Hakuna sera wala kampeni ambayo itaweza kubadilisha hilo kwa sasa. Hata iundwe tume huru ya aina yake haitoweza kubadili hilo.

Tume zote zilizopita zimekuwa na wajumbe toka vyama vyote vishiriki uchaguzi, hata hivyo mikwaruzo imeendelea kuwepo vilevile.
 
Maharamia wa CCM lazima wafanye wizi. Watashushwa watu kama 500,000 au hata milioni toka Tanganyika ili wakapige KULA (kura) visiwani kuihakikishia CCM ushindi wa TSUNAMI wakiwa na wasiwasi basi hata ballot box zitaibwa au kuwekewa kura bandia.

Chama twawala kazini.
 
Kutokana na yalotokea Kenya, CCM watajaribu kuwa smart zaidi, hata kama ni kwa kubadilisha mabox njiani watafanya.
 
Maharamia wa CCM lazima wafanye wizi. Watashushwa watu kama 500,000 au hata milioni toka Tanganyika ili wakapige KULA (kura) visiwani kuihakikishia CCM ushindi wa TSUNAMI wakiwa na wasiwasi basi hata ballot box zitaibwa au kuwekewa kura bandia.

Chama twawala kazini.

Duh hii kiboko, watu 500,000 si watakuwa noticed..labda wabadilishe maboksi au waweke maboksi yenye kura tayari.
 
Mbegu aliyopanda Maalim, ni mbaya mno. Hata kama hatogombea malalamiko hayatoweza kwisha. Kwani jamaa wa kisiwa cha pili wanaamini kuwa wao ni wengi na wanaweza kushinda chaguzi yoyote ile hapo kisiwani.

Kwa upande mwingine, kinachoangaliwa sasa huko visiwani ni mashindano kati ya kisiwa cha pili na kisiwa cha kwanza, nani zaidi? Hakuna sera wala kampeni ambayo itaweza kubadilisha hilo kwa sasa. Hata iundwe tume huru ya aina yake haitoweza kubadili hilo.

Tume zote zilizopita zimekuwa na wajumbe toka vyama vyote vishiriki uchaguzi, hata hivyo mikwaruzo imeendelea kuwepo vilevile.

Nimeitafuta hio mbegu mbaya ya Seif siioni hapa, lakini CCM ndio wenye mbegu mbaya wanaposema mtu wa kisiwa cha pili haongozi maisha ZANZIBAR, nakumbuka hata katika kampeni zao wakisema "kama wataka Ikulu, kajenge yako Mtambwe" akiambiwa Seif maneno hayo.
Hivi kuna mbegu mbaya zaidi ya hiyo?
Nakumbuka hata mwakilishi wa CCM (Asha Bakari Makame) ndani ya BARAZA LA WAWAKILISHI alisema: nchi haikupatikana kwa makaratasi (kura), wao walipigana, so hawatoi nchi.
Hakuna mashindano kati ya visiwa hivi, ila ni sumu ya CCM tu kugawa wananchi wanaposema 'CUF wakipata watavunja MUUNGANO then wataleta WAARABU' kwa vile tu wanataka Serikali tatu, ndio hapo watu wawili watatu wa Unguja wamepigwa changa la macho.
CUF naamini inakuja na sera muafaka na ndio maana inashinda chaguzi zote ila mizengwe tu inatumika kuwachinja. CCM just amani na utulivu then wanajisifia mambo yaliyofanywa na Serikali ya kwanza baada ya Mapinduzi, kwisha sera hapo! Ukiwauliza baada ya 1972, just wanang'aa macho tu, jibu hakuna.
Tume za Uchaguzi zoote feki, hata kuwe na hao wapinzani wawili kama wajumbe haisaidii chochote, kwani hao waliopita mbona walisema kabla ya matokeo ya kuwa taratibu muhimu za kiuchaguzi zimekiukwa, then ikawaje? haikuwa chochote na CCM mbele kwa mbele.
CCM na Serikali ya Zanzibar vyote vinaendeshwa Dodoma, from uchaguzi na uteuzi wa viongozi, hata maamuzi makubwa ya kiserikali kutoka huko pia. Tume ya Uchaguzi nayo inaendeshwa na CCM, maana wao ndio wameiweka.
Mabadiliko ya kisiasa na demokrasia ya kweli yatachukuwa nafasi yake Zanzibar siku tu CCM itapigwa mweleka Bara, ichukue nafasi ya opposition katika Bunge. Bila ya hivyo wacha tuendelee na miafaka kila baada ya miaka mitano.
Mtu wa Pwani ya 1995 ndo hayohayo ya 2010.
Time will tell
 
Back
Top Bottom