Elections 2010 Uchaguzi wa Spika wa bunge la 10 la Tanzania

Mh. Sita asiwe na wasiwasi wakati mwingine mlango unapofungwa Mungu hufunguwa mlango mwingine wenye heri.

I like this quote from Eistain "Any intelligent fool can make things bigger, more complex, and more violent. It takes a touch of genius -- and a lot of courage -- to move in the opposite direction."

Kwa hiyo mimi naamini muda ni dawa ya kila kitu ktk maisha.
 
Mungu washushie roho wakomm hao wabunge wa ccm,kura watakazopiga kwa maslahi yao ziende kwa marando,Amen!
 
Mnisamehe nashindwa kuleta update toka humu mjengoni, nimekaa angle mbaya ila tv zote ziko live.
Shukrani mkuu, ila ukifanikiwa tufahamishe japo kwa uchache yale ambayo utagundua hayatarushwa ktk Televisheni
 
Tayari huyu mama anayechangia TBC analizungumzia na kuendelea kuonyesha mashaka yake kwa Makinda, nadhani anamfahamu sana.
 
upigaji wa kura rahisi tu.
unaweka vema kwa yule umtakaye awe spika.
Naona ndo wanakusanya sasa zile karatasi
 
Salamu wana JF,

Ule mchakato wa kumpata spika mpya ndo umeanza asubuhi hii, kwa wana JF walioko on ground na wale wanaofatilia kwenye TV tunaweza kuitumia thread hii ili kuhabarishana live news.

Jamani mbona mabere amechakachuliwa mic wakati wakujieleza, hii ni haki kweli? haya bwana ccm wameamua kujimaliza wenyewe na kwakufanya hivyo wanatusaidia kusafisha njia maana watanzania wanaona kinachofanyika.Nimemuona samweli sitta amekaa kwa unyonge sana.kweli ccm wakubuhu kwa uonevu.Mtu anaye pendwa na wengi kwa utendaji kazi wake na anaye simamia haki ccm hawampendi.sijajua sababu ya kumpiga chini sitta,kama hivyo ndivyo mbona kikwete hawakumpiga chini wakati wa kura za maoni za kuomba nafasi ya kugombea uraisi,kwani kikwete alikuwa nafaa hukumu hii,lakini kwasababu anamanufaa kwa watu flani wachache hawakuweza kufanya hivyo na badala yake wanamtosa samweli sitta na kumwacha sitta.
 
baba tendaaaaa muujizaaaaaa.........

usiache mwaka huu upite bila marando kuwa spika....

tendaa muujizaaa

baba tendaaaa..........
 
Marando kaahidi kutumia taaluma yake ya sheria kufuata katiba ya nchi na kuwatndea haki watanzania
 
Back
Top Bottom