Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,722
- 218,284
Kuna kila dalili kwamba huyu Mama ataweka rekodi mpya kwenye siasa za Tanzania , hasa kwenye Historia ya Bunge la Tanzania.
Kwa Mujibu wa macho yangu Tulia Ackson hatorudi Bungeni 2025 na zipo tetesi kwamba Hata mamlaka za Uteuzi zimemchoka kutokana na uwezo wake mdogo wa "kuisaidia serikali bungeni" , hana ushawishi Jimboni kwake wala Bungeni.
Si kwamba haisaidii ccm bungeni , bali inasemekana anatumia ubabe zaidi na mijinguvu mingi badala ya hoja kuzimwa kwa hoja.
Kwa mfano , kuahirisha mjadala wa hoja ya ripoti ya CAG kujadiliwa bungeni kwenye kikao hiki cha Bajeti kulikotangazwa na Spika , ulikuwa mpango wa serikali yenyewe ili kukwepa aibu na kuwasahaulisha Wananchi wa Tanzania ambao mara nyingi huonekana kama Wajinga mbele ya viongozi , lakini Approach iliyotumiwa na Spika kulielezea jambo hilo lilistua kila mtu, jambo ambalo limeifanya serikali kufedheheka na kuamua kufanya U-Turn na kurejesha mjadala huo kwenye kikao hiki hiki , Spika alishindwa kutumia lugha laini ambayo ingewapumbaza wadau ili angalau waone serikali ina nia njema .
Taarifa zinaeleza kwamba serikali ya sasa inahitaji viongozi wenye ushawishi kwa jamii kutokana na lugha na matendo yao , hasa huko tuendako ambako Katiba Mpya naTume huru ya Uchaguzi vinakuja , haihitaji mtu mzigo anayetaka kubebwa na serikali au rushwa, hii ni kwa vile hayo mambo huko mbele hayatakuwa na nafasi tena .
Usiondoke JF kwa sasa , kwa vile kuna uhondo mwingi unakuja.