Uchaguzi wa Serikali za Mitaa umeharibiwa na Rais Magufuli mwenyewe

Ikulumaliyawananch

JF-Expert Member
Mar 14, 2018
339
533
watanzania ni wagumu kupambanunuwa mambo kwelikweli. Nimekuwa nikisikia watanzania wengi wakiwemo wanasiasa wakilaumu wasimamizi wa uchaguzi kwa kuharibu uchaguzi.

Na wengine wakitaka raisi Magufuli atowe tamko la kukemea uchafuzi huo na kuchukuwa hatua dhidi ya walio husika na uhalibifu wa uchaguzi.

Kitu ambacho kinanifanya nijiulize uwezo wetu wa kufikiri uko sawa au ni asiri ya unafiki wa kuogopa kusema ukweli unao tusumbuwa? Inawezakanaje katika miaka minne ya Magufuli hawakuweza kuona mipango yake ya kuharibu na kupora nguvu ya uma kuchaguwa viongozi ?

Yaani mtu apange kwa miaka minne tena hadharani mipango yake na kila mtu akiona halafu mipango imekamirika kama ilivyo pagwa halafu unaenda kwake kumwambia kuwa aharibu alicho kikamilisha kwa sababu sio kizuri kwako?

Kwa uwazi bila unafiki ni kwamba hiki kilicho tokea kwenye mchakato wa uchaguzi wa Serikali za mitaa hakikutokea kwa bahati mbaya wala hao watendaji wa kata na vitogoji walio amuwa kufunga office wakati wa kurejesha form hawakujiamlia kufanya hivyo wala hawakuwekwa kwenye nafasi zao kwa bahati mbaya.

Hawa watendajii walipewa instructions na wamefuwata maelekezo kwa ufasaha mkubwa sana. sasa kulaumu mtu aliye fuwata maelekezo kwa umakini unakuwa unamuonea. Au kumwambia mtu aliye andaa maelekezo kuwa maelekezo yake yameeleweka vizuri na walio pewa maelekezo wameyafanyia kazi vizuri.

Wapizanii na watanzania watakuwa ni kituko kama watakubali suluhisho litakalo pendekezwa na aliye panga kwa miaka minne kupora wananchi mamraka yao ya kuchaguwa viogozi wanaowataka na kujipa mwenyewe uwezo wa kuteuwa viongozi wote anao wataka yeye na si vingenevyo. hapa suluhisho ni katiba mpya na tume huru.

Jinsi ya kupata vitu hivi viwili sio kwa kumbembeleza Magufuli na serikali yake, bali ni kuvidayi kwa gharama yoyote bila hofu wala woga.

Na hapa ndio tutakapo wakumbusha watawala kuwa Tanzania ni mali ya watanzania na sio ya watawala. haiwezekani mtawala anafikia hatuwa ya kudharau wananchi kiasi hiki halafu tukaendelea kucheka naye.

Anatumia kodi zetu kutuchagulia nani aongoze maisha yetu kama vile maisha yetu ni kama magari yake anaweka dreva anaye mtaka yeye. Tukiendelea kucheka na watawala wa aina hii ipo siku tutapangiwa mda wa kulala na mda wa kuongea.
 
Ungeacha Aya ingependeza. Na ingefanya wenye akili waisome yote.

Kwa upande wangu nimeishia kichwa cha habari
 
Hiyo Tume unayoitaja humu haihusiki na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Acha kuwapotosha wananchi.
 
Hivi mtendaji wa ngazi ya chini akifanya vizuri katika kutimiza majukumu yake praise team sifa hupeleka kwanani vile? Na ikitokea mtendaji huyohuyo wa chini kafanya vibaya kwenye majukumu yake lawama huenda kwanani vile ?
Majibu tunayo ila Watanzania tumejaa unafiki over
 
Hiyo Tume unayoitaja humu haihusiki na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Acha kuwapotosha wananchi.
Tume yenyewe tayari inmeshachakachuliwa kwa maandalizi ya 2020. Kuviunganisha hivi vitu viwili ni Sawa kabisa.
 
Mkuu pumzika, vuta pumzi alafu itoe tararibu maana si kwa hamaki uliyonayo na hasira katika uwasilishaji wa hoja yako yenye kweli tupu. Ujumbe umefika na you have hit the right target.

Watanzania tunazaraulika sana kwa ujinga wetu wenyewe. Tumekuwa wepesi wa kusahau mambo mapema sana, tumerithishwa uoga ambao hauna manufaa kwa wananchi na Tanzania yetu, uoga unawafanya watawala wafanye watakacho kama vile nchi haina kanuni na taratibu za jinsi ya kuiongoza.

Kilichobaki ni kudai KATIBA MPYA NA TUME HURU YA UCHAGUZI, mengine yatafuata baada ya hayo kurekebishwa
 
Let us not move around the bush, Magufuli ndo mhusika mkuu, aliwaita watendaji ikulu akawapa maelekezo wametimiza walichoelekezwa. Nina rafiki yangu mmoja ndugu yake ni mmoja wa watendaji walioitwa, aliporudi alimwambia huyo rafiki yangu kwamba kwa maelekezo tuliyopewa kitakachotokea mtakiona! Na kweli tumekiona. Jafo is simply a victim of circumstance but the master mind is Magufuli whose irrational and eccentric behavior leads him to do what he does.
 
Huyu kimeo kesha tuharibia nchi mbona kitambo tu nishangaa sana Hawa ccm wana buluzwa kama makondoo vile alafu yako comfortable as is doing the right things kumbe kesha habari Kila kitu
Ccm wanahitaji maombi mazito mnooooooooooooooo
 
Back
Top Bottom