Uchaguzi wa nyumba ya Kupanga

DISPLEI

Member
Oct 17, 2012
70
46
Najiuliza naomba tushirikishane uzoefu kuhusu nyumba za kupanga. Nia ni iwapo mtu anataka kujenga nyumba zaidi ya moja kwenye kiwanja kimoja, wapangaji wenye vipato vya kati na kuendelea wanapendelea nini! Namaanisha nyumba za kodi ya TZS300,000 au zaidi kwa mwezi. Tuseme nyumba yenye vyumba viwili vya kulala katika kiwanja kimoja na fensi moja.

Mfano.

1. Gorofa moja kwa familia mbili au zaidi

2. Nyumba za chini za familia 2 au zaidi

3. Nyumba zinazojitegemea za chini kwa familia moja moja.

Tuseme usalama na maegesho ya magari yawe hayana shida, mfano kila nyumba iwe hata na uwezo wa kupaki gari 2

naombeni ushauri kwa wapangaji na hata ujenzi kwa upande wa gharama na matarajio ya mapato kutoka kwenye uwekezaji huo.
 
Wapangaji tunapendelea nyumba inayojitegemea, vyumba at least 2 na bei isiwe juu kama hivyo (laki 3),angalau laki 2. hata hivyo inategemea na eneo/sehemu unapoijenga hiyo nyumba.
 
Back
Top Bottom