Uchaguzi wa Marekani: Trump awaambia wapiga kura wa North Carolina wapige kura mara mbili

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,876
Trump amesema wapigaji kura wanapaswa kupiga mara mbili


Rais wa Marekani Donald Trump amewaambia watu katika jimbo la North Carolina wapige kura mara mbili katika uchaguzi wa mwezi Novemba, licha ya kwamba kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Bwana Trump alisema wapigakura watume kura kwa njia ya posta, halafu wapige kura binafsi ili kuujaribu mfumo wa upigaji kura.

Rais huyo mara kwa mara amekuwa akitoa madai ya uongo kwamba kura zinazopigwa kwa njia ya posta zinauwezekano wa kuibiwa.

" Wacha watume kura na waache waende kupiga kura ," aliliambia shirika la habari la North Carolina WECT-TV Jumatano.

"Na kama mfumo ni mzuri kama wanavyosema basi bila shaka hawataweza kupiga kura yao binafsi ."

Mkuu wa North Carolina Josh Stein ali tweet kwamba "nimeshitushwa sana na kuwashashawishi " watu katika jimbo "kuvunja sheria ili kumsaidia kupandikiza ghasia katika uchaguzi wetu ".

Voters in Wilmington, North Carolina


"Hakikisha unapiga kura, lakini usipige kura mara mbili !" Bwana Stein aliongeza "Nitafanya chochote ninachoweza kufanya kulingana na mamlaka yangu ya kisheriakuhakikisha utashi wa watu unaidhinishwa katika mwezi wa Novemba.

Wademocrats pia wamemshutumu Rais Trump na chama cha Republican kwa kujaribu kuwazuwia watu kupiga kura ili kuusaidia upande wao wa siasa katika uchaguzi.

Rais Trump alikuwa Wilmington, North Carolina, kuiidhinisha rasmi miji hiyo kama miji ya kumbukumbu ya urithi ya Vita vya Dunia.

Nini kitatokea kama watu watapiga kura mara mbili?
Mchakato wa upigaji kura unaendeshwa na majimbo.

Msemaji wa bodi ya Uchaguzi ya jimbo la North Carolina ameliambia gazeti la New York Times kwamba katika jimbo hilo haitawezekana kwasababu ni kura ya kwanza pekee itakayorekodiwa.

Mtu ambaye tayari amepiga kura kwa njia ya posta atafahamishwa katika kituo cha kupigia kura kwamba hawezi kupiga kura ya binafsi, alisema.

Kupiga kura mara mbili makusudi ni uhalifu, aliongeza.

Ni kwanini upigaji kura kwa njia ya posta unazungumziwa zaidi katika uchaguzi huu?
Majimbo kadhaa ya Marekani yamekuwa yakiruhusu na kuwashawishi watu kupiga kura kwa njia ya posta kwa miaka kadhaa.
Lakini idadi ya watu wanaopiga kura kwa njia ya posta inatarajiwa kuongezeka sana mwaka 2020 kutokana na hofu ya mikusanyiko ya watu katika vituo vya kupigia kura wakati huu wa janga la corona.

Matokeo yake, makumi kadhaa ya majimbo ya Marekani yamepanua huduma ya upigaji kura kwa njia ya posta.
Kuna hofu kuwa idadi kubwa ya kura zinazopigwa kwa njia ya posta ina maanisha kuwa hesabu ya kura itachukua siku kadhaa au wiki kadhaa , baada ya siku ya uchaguzi.

Ni yapi madai ya Trump juu ya wizi - na je kuna ukweli kuyahusu?
Si mara ya kwanza Rais Trump kutoa kauli tata juu ya upigaji kura kwa njia ya posta.
Akizungumza katika kongamano la kitaifa la chama cha Republican (RNC) mwezi uliopita, alidai kuwa "kuna wizi mkubwa uliohusika " na upigaji kura ya njia ya postana hilo "tunapaswa kuwa makini sana makini sana nalo ".

lakini madai haya yamekuwa yakikipingwa mara kwa mara na wataaalamu.
Ellen Weintraub, kamishina wa kamati ya shirikisho ya uchaguzi, alijibu wakati huo kwamba "hakuna kabisa msingi wa dhana ya njama kwamba kupiga kura kwa njia ya barua pepe kunasababisha wizi ".

Katika upafiti kadhaa wa kitaifa na katika ngazi ya majimbo kwa miaka mingi haujafichua ushahidi wa kuenea kwa wizi mkubwa.
Katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2016 , karibu theruthi moja ya wapigakura walipiga kura yao kwa njia ya posta na idadi inatarajiwa kuongezeka kutokana na hofu ya virusi vya corona.

Majimbo binafsi yanadhibiti sheria zao za kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa kitaifa -na wengi wanaangalia jinsi ya kuongeza upigaji kura wa njia ya posta ili kuzuwia mikusanyiko ya watu katika vituo vya kupigia kura siku ya uchaguzi. Majimbo kadhaa yanapanga kuendesha uchaguzi wa "wote kwa baruapepe" mwezi ujao wa Novemba.

Kiwango cha wizi wa kura kwa ujumla nchini Marekani ni kati ya 0.00004% na 0.0009%, kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2017 uliofanywa na kituo cha Brennan Center for Justice.
 
Mh. Rais Trump yuko sahihi mno katika hili. Uwezekano wa Marekani kupiga kura kwa njia ya posta bila kutokea matatizo ya wizi wa kura haupo. Wanatakiwa wamuongezee muda halafu uchaguzi ufanyike Corona ikiisha.

Wanataka kuleta tena mambo kama ya mwaka 2000 ya Frolida County recount, wakati wa Bush. Mwezi mzima kila uki-switch CNN unakutana na Frolida County recount. Waache hizo kwa sababu wao ndiyo wanaotufundisha Demokrasia sisi, lazima watuonyeshe mfano mzuri. Mimi nashauri Rais Trump wamwongezee muda, wasipige kura kwa njia ya Posta kunaweza kukuwa na wizi kura wa wa ajabu sana. Kwani kuna tatizo gani Trump wakimwongezea hata mwaka mmoja, halafu Corona ikiisha wanapiga kura zao?
 
Kiwango cha wizi wa kura kwa ujumla nchini Marekani ni kati ya 0.00004% na 0.0009%, kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2017 uliofanywa na kituo cha Brennan Center for Justice.
Hiki ni kiwango cha wizi katika hali ambayo ni ya kawaida, ambapo system ya upigaji kura inakuwa ni ile ya kawaida, yaani ile ya siku zote. Kwa system ambayo ni mpya, na katika hali ambayo Control Mechanisms zinatawaliwa na uwepo wa ugonjwa wa Corona, kiwango cha wizi bado hakijulikani, isipokuwa kitajuikana tu baada ya kuwa wameshapiga kura, kama kweli watafanya hivyo. Under the current influence of Corona, that percentage can be anything, kitu ambacho si kizuri sana.

Mimi nawaomba sana Marekani waendelee kutuonyesha Demokrasia makini, kama ambavyo wamekuwa wakifanya tangu kipindi kirefu nyuma. Waahirishe uchaguzi Corona ipite kwanza. Marekani ipo siku zote na muda pia nao upo siku zote. Kama ni hivyo wanakimbizana na nini? Mwishowe waje wasababishe tena upotevu wa maisha ya watu ambao haukutarajiwa kwa sababu ya kupiga kura kipindi cha Corona, haitapendeza kabisa ikitokea hivyo
 
Back
Top Bottom