Uchaguzi wa magari

Shagiguku

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
407
133
wadau wa jf, kumekuwa na aina mbalimbali za magari kwa mfano, used na brand new, automatic na manual, ya mjapani, mchina, mfaransa, mmarekani, mjerumani na yale ya kibongo (nyumbu), na kwa kuangalia haya magari yanatofautiana mambo mengi kama vile speed, uimara, uchemshaji wa injini, kuchoka haraka nk, nk ,nk...!!

sasa wewe mdau wa jf, je, unaweza kutuambia ni gari aina gani ungependa umiliki au una miliki gari lipi kati ya hayo yaliyotajwa...?? kwa nini unamiliki au unataka umiliki gari ulilolitaja...??? na kama unalimiliki unalionaje je, ungependa kuendelea nalo ama ungependa kuliTema...??
 
mi napanda taxi tu maana nitabadili kila aina ya gari, na siku mojamoja navizia lift za watu
 
Du!
Actually huwezi kupata gari iliyo bora sana kupita zingine!...Hata mpya itakupa presha fulani ambazo huwezi kuzipata ukiwa na used!

Nilisoma nikiwa darasa la pili kuwa hapo zamani za kale Katika nchi fulani kulifanyika uchaguzi ambapo alitakiwa kupatikana kiongozi ambaye atawashinda wote kwa mali, kwa akili, kwa uzuri, kwa urefu , kwa nguvu, kwa watoto, kwa unene, kwa mavazi, na kila kitu!
Lakini kwa bahati mbaya uchaguzi wao haukufanikiwa, maana walimkosa mtu wa aina hiyo!
 
Mimi napenda ya kibongo kwa sababu yametengenezwa kwa kuzingatia mazingira ya Kibongo.
Yanahimili mikiki mikiki na bara bara zetu mbovu kuliko mengine..
Hata ikitokea ukaligongesha kwenye gari nyingine haliharibiki sana kiasi cha kukuacha kwenye mataa.
Ya Ulaya hayako stable sana hasa kwa tabia yetu ya uendeshaji, yanachemsha haraka.
Ukiyagongesha na mengine hesabu umeumia, hayana uvumilivu kabisa, very delecate.
Ya Kijapani hali kadhlika, kwanza ni malaini kuliko hata ya Ulaya, na hayana kabisa uvumilivu wa mazingira yetu..
Hayana uwezo wa kubeba mizigo mikubwa, vinginevyo utaliua kabla ya siku zake..

Naungana na mkuu Kiduku kuwa kama huna uwezo wa kumiliki gari bora kuendelea na Taksi, ikiwezekana kuomba lift kwa wengine.
Ingawa lift za mara kwa mara siyo nzuri sana, kama una haraka bora ukamate Taksi na lift iwe option ya pili kama ikijitokeza bila wewe kulazimisha.
Ingawa Taksi siku hizi zinonekana kuwa hatari kwa usalama, hivyo tuzipande at awa ouni riski...
 
Mimi napenda hiace na coaster!
Huitaji kuweka mafuta, kununua spare wala kufanya service. We unapanda unatoa jiti tatu au nne, then unafika unapotaka kwenda!
 
Mimi napenda ya kibongo kwa sababu yametengenezwa kwa kuzingatia mazingira ya Kibongo.
Yanahimili mikiki mikiki na bara bara zetu mbovu kuliko mengine..
Hata ikitokea ukaligongesha kwenye gari nyingine haliharibiki sana kiasi cha kukuacha kwenye mataa.
Ya Ulaya hayako stable sana hasa kwa tabia yetu ya uendeshaji, yanachemsha haraka.
Ukiyagongesha na mengine hesabu umeumia, hayana uvumilivu kabisa, very delecate.
Ya Kijapani hali kadhlika, kwanza ni malaini kuliko hata ya Ulaya, na hayana kabisa uvumilivu wa mazingira yetu..
Hayana uwezo wa kubeba mizigo mikubwa, vinginevyo utaliua kabla ya siku zake..

Naungana na mkuu Kiduku kuwa kama huna uwezo wa kumiliki gari bora kuendelea na Taksi, ikiwezekana kuomba lift kwa wengine.
Ingawa lift za mara kwa mara siyo nzuri sana, kama una haraka bora ukamate Taksi na lift iwe option ya pili kama ikijitokeza bila wewe kulazimisha.
Ingawa Taksi siku hizi zinonekana kuwa hatari kwa usalama, hivyo tuzipande at awa ouni riski...
duh elimu ni kuona kile kisichoonekanika....kweli ndinga za kibongo ziko strong na 99% ni dabo d-Fu!!
 
Back
Top Bottom