Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,355
- 1,991
mpaka kieleweke, hayo ya kununua shahada haitoshi kusema, pandeni watu watakaojifanya wanauza warekodini muwaumbie hadi hivi sasa hakuna ushahidi wowote wa CCM kununua maana ungekuwepo ungetolewa.
Kuna ugumu gani wa kupanda wauza shahada feki ili muwakamate wanaonunua?
Ndio maana mimi siamini kuna watu wamenunuliwa ndani ya miaka zaidi ya 15 hakuna hata mtu mmoja aliyejitokeza na ushahidi wa wazi. Yote ni mazingira tu, yaani hakuna uwezo wa watu kufikiria jinsi ya kufanya hivyo?
Taarifa nilizonazo mimi ni kuwa Dume la Mbegu Aka Tinga Tinga sasa limepaki bungeni Dodoma, likijazwa mafuta na punde litapelekwa Kiteto- na huko vitambulisho vya mpiga kura vitanunuliwa na uharamia wote utafanyike. Na mwisho Ole Kimesera ataambulia asilimia kumi kama nilivyotabiri. Wapinzani mlie tu. Hivyo vitisho vya Erasto Tumbo aliyeshindwa Kisesa kwamba fedha za ufisadi zitazuiwa zisigawanywe kwa nguvu ya umma vitawatokea puani. Na mkileta ungangari mtapata za Kikenya Kenya aka Ngunguri style!
PM
PM
Mshaanza kulia lia ku justify kushindwa kwenu....
Taarifa nilizonazo mimi ni kuwa Dume la Mbegu Aka Tinga Tinga sasa limepaki bungeni Dodoma, likijazwa mafuta na punde litapelekwa Kiteto- na huko vitambulisho vya mpiga kura vitanunuliwa na uharamia wote utafanyike.
Taarifa za hivi punde ni kuwa CCM wakiongozwa na mzee Malecela wameanza kale ka mchezo ka Tunduru ka kununua shshada za wapiga kura na wameanzia eneo linaloitwa Matui na hapo yupo mzee Malecela mwenyewe akiongoza hujuma hiyo dhidi ya vyama vya upinzani.
wanunuzi wa kadi si Tingatinga personally bali ni wajumbe wa nyumba kumi na wenyeviti wa Vijiji.
ndiyo hivyo.. maana tuliambiwa kulikuwa na ushahidi wa kutosha kule Kigoma lakini ikawa kimya.. sasa haya ya Kiteto kama ni kushinda, wapinzani watashinda bila kulia lia.. ama sivyo wanaweza kujikuta wanafunguliwa tovuti yao wenyewe..
Kasheshe
Ndiyo maana akaitwa tingatinga kwa ushujaa wa wizi wa kura . Amekuwa anakisaidia chama kwa uovu wa aina hii . Nani asiyejua ? baridi walipiga hata watu kwa Amri yake kule kwa Cheo umesha sahau ? Jina Tingatinga means hodari wa kazi hii ya wizi na fujo kenye kampeni .
Yaani unamwagia sifa Malecela kwa uharamia anao endesha ama mimi sijaelewa ? Hivi huyu watamtumia hadi lini ?Kama CCM ni safi na inafanya wayatakayo wananchi kwa nini kununua kadi zao za kupigia na kufanya uharamamia kama ulivyo sema hapo juu ?Kukubalika kwa CCM ni kupi sasa kwa wananchi kwa tabia hizi ?