Interested Observer
Platinum Member
- Mar 27, 2006
- 4,998
- 7,927
Mtu wa Pwani,
Binafsi sina ushabiki upande wowote na kwakuwa Zitto alikuwa na namba yangu kama mwanachama wa JF basi akaniuliza kama niko mtandaoni na naweza kuwafahamisha kinachojiri. Nikafanya kuwafahamisha kadiri alivyokuwa anani-update.
Kwa sasa nimepata ujumbe toka kwake ambapo anawashukuru wana JF kwa ushirikiano. Ujumbe unasema hivi:
"Tupo kituo cha polisi Kiteto, RPC amesafiri toka Babati kuja kufuatilia suala hili. Wamekamatwa makomandoo wawili ambao wamekiri ni toka CCM na wametokea Dar trained JKT Militias. Majina yao ni Hamis Kilindo na Keneth Mbilinyi. Keneth anayejiita mlinzi wa Pius Msekwa alikabidhiwa machine gun na mkuu wa kituo". Mwisho wa kumnukuu.
Mjumbe hauwawi sio?
UnbelievablE!!!!
Hivi mapigano haya yamesababishwa na nini?
Pius Msekwea analindwa na hao makomandoo wa mtaani ?CCM jimbo moja ndilo linataka kuua watu namna hii ?Nimesoma kwamba kuna jumla yao 30.Sasa panakalika kweli hapo Jimboni ?Polisi anawapa hao silaha ? Kwa imani ipi na makubaliano yapi ?
Kweli JK una ukaribu na wapinzani nasi tunaona .
Eti Msekwa yuko involved na haya?
AMANI na UTULIVU... Amen!
AMANI na UTULIVU... Amen!
Najua watu wa vyombo vya habari nyumbani bado havijamaliza kuchapa magazeti ya kesho.. tafadhali kombeni hizo picha zitoke Kesho kuonesha jinsi gani serikali yetu inajali haki za binadamu na utawala wa sheria!
Hivi ni kitu gani kinawafanya
Hivi sasa kuna habari nyingine nafuatilia kutoka Dar ambayo ina impact kubwa zaidi na JF... Mkiona imezimika kimbilieni KLH News...
Hivi ni kitu gani kinawafanya Polisi waamini kuwa kwa kutumia nguvu wanaweza kubadili mawazo ya watu? Huyo OCD lazima atimuliwe kazi na mkuu wao wa kituo vile vile na tunataka kina Makamba na Msekwa watoke hadharani na kulaani vitendo hivyi vya kinazi, kinyama, na ambavyo hakuna maneno yoyote yanayoweza kuvihalalisha.
Hivi sasa kuna habari nyingine nafuatilia kutoka Dar ambayo ina impact kubwa zaidi na JF... Mkiona imezimika kimbilieni KLH News...
Hiyo ya Dar.. I hope itaisha kimya kimya maana ikilipuka JF mmekwisha... inaonekana mnapata nyeti nyingi kutoka serikalini hata mambo yasiyoandikwa au waandishi hawajui. eg Kwamba Kikwete alienda Ujerumani kunywa chai na kurudi kumuwahi Bush.
Ninaisubiri kwa hamu hiyo taarifa ya DAR maana kuna kila dalili itakuwa breking newz kali