Uchaguzi una kushinda na kushindwa...

Uchaguzi una kushinda na kushindwa...

Kuna watu wameulizza sana juu ya matokeo ya uchaguzi Arusha, but jibu la harakaharaka katika kila uchaguzi kuna kushinda na kushindwa, na mshindani wa kweli lazima ajiandae kwa yote maana asiyekubali kushindwa si mshindani.(kama mabo yote yamekwenda sawa).

Nape huwa sina shida na wewe....kwa sababu wewe hufanya siasa....na wala hutumii uovu kufanya siasa!
Big up mwana jimbo la ubungo mwenzangu but different political colors.
 
Hivi tuliposhindwa Arumeru tulikataa kumbe?
Chaguzi za Arusha mkishindwa mnakuwa wepesi kukubali matokeo tofauti na sehemu nyingine! What's up?

Kama sijakosea Nyerere alisema"Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM"
 
Nape umesahau ulivyosema CDM wamesabisha mlipuko Arusha-Soweto kwa sababu wangelishindwa uchaguzi. Bila huruma za waliokufa na kujeruhiwa! CCM mkaendelea na bunge...I will never forget this labda mtubu hiyo dhambi...
 
Hivi tuliposhindwa Arumeru tulikataa kumbe?

Cha muhimu mjipime...wapi mmekosea....CCM kama chama mna majembe ya kutosha sema hamjayapa nafasi,nyie mnakomaa na kina Shonza ambao hutoa kauli za kuudhi then hao hao ndio wanakuwa frontline!
Nakuhahakishia ungepiga kampeni wewe peke yako tu....mngepata hata kata moja....!
 
Kushindwa ni sehemu ya mchezo ccm jipangeni zaidi kwa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.
 
Huyu Nape angekuwa muungwana angeipongeza Chadema.

Amekiri kushindwa lakini ameshindwa kwenda mbele zaidi.
 
Kuna watu wameulizza sana juu ya matokeo ya uchaguzi Arusha, but jibu la harakaharaka katika kila uchaguzi kuna kushinda na kushindwa, na mshindani wa kweli lazima ajiandae kwa yote maana asiyekubali kushindwa si mshindani.(kama mabo yote yamekwenda sawa).

swali kwa kaka nape: sasa hawa watu mnaomiliki wanaosababisha chama chenu na serikali yenu kutukanwa kila kona inamaana ccm anakosekana mtu wa kuwa replace?? Maana hao ndo chanzo cha anguko lenu 2015
 
Siku hizi huyu jamaa haonekani kabisaaa sijui kwa nini, bora umekubali matokeo maana na wewe Nape unaongoza kwa siasa chafu hapa nchini...
 
Nape hongera sana kwa post yako, unaanza kukomaa kisiasa na kujua kwamba tupo kwenye siasa za kiushindani. Usiwe kama Mwigulu aliyekunywa maji ya bendera ya kijani. Shame on him!
 
ndivyo ilivyo, sasa hamishia nguvu kwa bwana mwigulu maana bluetooth imenasa mkanda mpya.
 
Shikamoo chadema
Kinachofurahisha ni kwamba makatibu wakuu wa ccm kila anayeingia anapata kichapo.Makamba alipokea kichapo Tarime, MUKAMA alipokea kichapo ARUMERU, leo mzee wa meno ya tembo kapokea kichapo palepale mtaani kwake AR.wHAT A SHANGWE
 
Bora yako Nape Nnauye umekubali kushindwa, kuna wengine saa hii wangekuwa wanasema wameibiwa kura, ila sasa wapo kimya kuhusu hilo.
 
Last edited by a moderator:
Busara kama hii Mwigilu hana, yeye anajua ni ushindi tu kwa gharama yoyote ile! na hicho ndicho kinachowagharimu nyie ccm.

Nape wewe tunajua ni Chadema .ila auna jinsi ilimradi mkono uende kinywani .you just hang over there .as chadema undercover for 2015 victory
 
Kwa hili mmeshikwa pabaya mtakoma 2015 hiyo ni rasha rasha tu subiri makubwa 2015
 
kuna watu wameulizza sana juu ya matokeo ya uchaguzi arusha, but jibu la harakaharaka katika kila uchaguzi kuna kushinda na kushindwa, na mshindani wa kweli lazima ajiandae kwa yote maana asiyekubali kushindwa si mshindani.(kama mabo yote yamekwenda sawa).
poleni saaana! Japo hamkuwa na jinsi!
 
kwa namna moja au nyingine viongozi wawe makini na propaganda zao kwani, Nape alisema kuwa waliolipua mabomu Arusha ni CHADEMA, kwa vile wamekosa mvuto ARUSHA, na hivyo wamelipua mabomu kujiangamiza wapate kura za huruma.

haya majibu ya wanaARUSHA, katika uchaguzi wa leo, inaweza kuonesha kuonesha ni nani anapoteza mvuto na hivyo ni nani alilipua bomu. WANASIASA KUWA MAKINI NA KAULI ZENU ONA SASA KAULI ZAKO MWENYEWE INAKUHUKUMU
 
Back
Top Bottom