Uchaguzi ujao ni wa muhimu sana! Pengine kupita chaguzi zote toka Uhuru!

Sidhani! Historia inaonyesha uchaguzi wa wakati ambao mgombea wa CCM anamaliza muda wake ndiyo huwa na kashkash! Uchaguzi wa 2020 utakuwa mrahisi kwa CCM kuliko wa 2015. Sioni mtu yoyote anayeweza kuwa tishio kuliko Lowassa alivyokuwa uchaguzi uliopita. Labda 2025! Mtu ukiwa unafuatilia siasa za Tanzania kupitia kwenye mtandao unaweza kudhani CCM haina hata wiki bila kuondolewa. Lakini unapofanya ziara mwenyewe huko mikoani na kuongea na watu unaona kabisa hakuna tishio lolote kwa CCM. Hata ziara anazofanya Rais Magufuli mikoani hazina dalili yoyote ya rais aliyechokwa na wananchi!

Umekusea mkuu,sins uhakika kama kweli ulikuwa wafwatilia ziara za mkulu mkoani kwa ukaribu...

NB
Uliona alivyokua akilalamikia na kunung`unikia wakazi wa mbalali jinsi walivyo kimya,na kuwa busy na mambo yao akiwa anahutubia?
 
Everything speaks for itself! Need I say more?
Mara nyingi huwa namsikiliza Rais Magufuli akihutubia, lakini hotuba zake zimejaa masimulizi zaidi ya mipango mikakati ya Maendeleo ya nchi Kisiasa, kiuchumi, Kijamii, n.k.

Wananchi tuhahitaji kusikia mikakati na hatua madhubuti za kukuza demokrasia, kuongeza kipato na kutoa huduma za jamii.

Masimulizi ya mambo madogo madogo yaliyotokea hatuyahitaji kuyasikia toka kwa mkuu wa nchi.

Mfano stori ya ndege, sijui walitaka kupiga, mara sijui huyu ni TISS mara hivi mara vile, hayo ni mambo ya utendaji wa ndani ambayo sisi wananchi hatuhitaji kusimuliwa
 
Uchaguzi ujao naona kwa karibu ukiwa landslide victory kukaribia ile kikwete anaingia madarakani!
Utakuwa tight humu jf na kwenye mitandao ya kijamii ila kiuhalisia, JPM atashinda kwa kishindo!
Hivi mnaposema kutakuwa na upinzani, upinzani mwingine mnauongelea au huu wa kina Mbowe na genge lake?
Kwahiyo watu humu JF siyo hao walioko mitaani?
 
Well said.
 
It's true

Uchaguzi huo ni muhimu sana, lakini ni lazima kwanza ihakikishwe kuwa uchaguzi unakuwa free and fair, kwa maana ni lazima Tume ya uchaguzi itende kazi yake kwa uadilifu wa hali ya juu
Bado una msimamo wa tume huru kama tindo?
 
Katika vitu nimemuomba Lissu kupitia email niliyomuandikia atakapokuja kwenye kampeni, ahakikishe anaondoa hata imani ndogo ya tume ya uchaguzi iliyopo. Ahakikishe anaivua nguo kiasi ambacho itabidi ibadilishwe taka wasitake. Hakuna namna tume hii itaweza kubadilishwa bila shinikizo, na namna pekee ni kuweka udhaifu wake hadharani. Naisubiri kampeni kwa nguvu zangu zote, ila sio kama mpiga kura chini ya tume hii mbovu, bali kama mdau wa kuhakikisha tume ya uchaguzi haiwi mali ya mwenyekiti wa ccm. Nawashauri wadau wote tuendelee kurudia hili suala la tume huru ya uchaguzi, ili vyama vyetu vijue tunataka nini.
 
Kwa Tume ya Uchaguzi hii hii....ambayo Rais ana mamlaka ya kureshufle wakurugenzi wake (IT etc) miezi michache kabla ya uchaguzi? Yaliyotokea Zanzibar ambapo Mwenyekiti wa Tume "alitekwa" mchana kweupe na kwenda kutengua matokeo chini ya mtutu wa Shaba ni ishara tosha kwamba 2020 hakuna jipya. Mark my words
Wakifanya hivo dhambi hiyo iwe juu ya vichwa vyao.
 
Uchaguzi ujao naona kwa karibu ukiwa landslide victory kukaribia ile kikwete anaingia madarakani!
Utakuwa tight humu jf na kwenye mitandao ya kijamii ila kiuhalisia, JPM atashinda kwa kishindo!
Hivi mnaposema kutakuwa na upinzani, upinzani mwingine mnauongelea au huu wa kina Mbowe na genge lake?

Ni sawa na Yanga ifanye mazoezi huku goli moja likiwa wazi, wafungaji wake wawe wanafunga sana, kisha iseme itashinda sana kwakuwa washindani wake hawakubaliwi kufanya mazoezi kama inavyopaswa. Kuna kitu inaitwa surprise, na hapo ndio panic mode itakapotokea kwa jiwe, na kuanza kutumia vyombo vya dola na kundi la watu wasiojulikana, kwani vitengo hivi ni muhimu kwa huo ushindi bandia unaosakwa.
 
Surprise ilikua 2015 sio sasa! Labda msubiri hiyo surprise 2035 wakati jpm anatoka maana sasa hivi waTz tushasema atake asitake 2025 anaunga mpaka 2035.
 
Sio watz wote, sema wanaccm, tume ya uchaguzi na vyombo vya dola. Msilazimishe kuchanganya watz wote kwenye matamanio yenu. Na kama hujamalizia nyumba yako, jiandae kisaikolojia.
 
Surprise ilikua 2015 sio sasa! Labda msubiri hiyo surprise 2035 wakati jpm anatoka maana sasa hivi waTz tushasema atake asitake 2025 anaunga mpaka 2035.
Umetumia tahmini gani? Au unazungumzia MATAGA?
 
It's true

Uchaguzi huo ni muhimu sana, lakini ni lazima kwanza ihakikishwe kuwa uchaguzi unakuwa free and fair, kwa maana ni lazima Tume ya uchaguzi itende kazi yake kwa uadilifu wa hali ya juu
Hivi limefikia wapi?
 
It's true

Uchaguzi huo ni muhimu sana, lakini ni lazima kwanza ihakikishwe kuwa uchaguzi unakuwa free and fair, kwa maana ni lazima Tume ya uchaguzi itende kazi yake kwa uadilifu wa hali ya juu
Everything speaks for itself! Need I say more?

Uchaguzi huu ccm ni LAZIMA ianguke, suala ni kama watakubali kuachia madaraka kwa amani!

Ni uchaguzi ambao utatupatia UHURU mpya.
Wakitenda haki wametusaidia wasipotenda haki wametusaidia, Waache wafanye watakalo
 
Back
Top Bottom