Uchaguzi 2020 Uchaguzi tarehe 28; CHADEMA inapoteza kila kitu

kajekudya

JF-Expert Member
Sep 24, 2015
2,469
4,904
Kuna watu humu wanajipa moyo eti CHADEMA hii ya Lissu, Mbowe, Mnyika, Heche, Halima, Bulaya Matiko na Wenzake wanaweza kuishinda CCM ya Magufuli, Bashiru Ali, Mangula, na mfumo mzima wa Chama Cha Mapinduzi.

Kama Kuna mtu anawaza hivo na anamanisha na ana amini Mawazo yake hayo yanaweza kuwa uhalisia, basi huyo ana tatizo kubwa sana kifikira.

Uchaguzi huu CDM iliyopalaganyika ikiwa inamtegemea mtu mmoja inakwenda kupambana na:
1. Rais Magufuli
2.Chama Cha Mapinduzi.
3.Watanzania

1.Rais Magufuli
Rais Magufuli tangu aingie Madarakani amekuwa akifanya baadhi ya Mambo ambayo yanakuwa reflected Kama ya kwake.Hali hii imemfanya pengine awe maarufu kuliko hata Chama chake. Magufuli amejijengea ufalme wake ndani ya mioyo ya Watanzania, siyo lazima akubalike na wote na hakuna anayetegemea iwe hivo, lakini ukweli umaarufu wake unamfanya yeye Kama yeye apate kura ambazo atapigiwa yeye Kama Magufuli, na nyingi ni zile za wasio na Chama.

Hizi kelele za mitandaoni dhidi ya JPM ukizifatilia ni za wale wale, hata thread humu ukiangalia wale wale ndio wanakoment, lakini waulize je Mama zao, Dada zao, wajomba zao, shangazi zao, Babu zao na Bibi zao wanaijua Facebook, wanaijua JF, wanaijua tweeter au Instagram. Jibu wanalo, je hoja ya Uhuru na maendeleo ya vitu inaeleweka kwa Hawa watu. Mtu ambaye hakuwahi kuona umeme( sizungumzii Maria Sarungi Wala Fatuma Katume, na Hawa hawafiki hata 5000) leo kauona umeme unaweza kumueleza asimchague Magufuli eti kwakuwa amemnyima Uhuru wakati anaenda kanisani, anapiga simu, anaenda sokoni anaenda shambani Bila wasiwasi akakuelewa?.

2. Chama Cha Mapinduzi
Dubwasha linalotisha, Dude hatari Barani Africa, dude ambalo Lina historia ya kuwaweka viongozi kadhaa wa Afrika Madarakani. Hili dude Lina vichwa, Lina Consultants, lina rasilimali watu na fedha za kutosha, Lina uzoefu wa kutosha katika anga hii ya siasa. Halafu Kuna mtu anawaza linaweza kushindwa na mtu anaitwa Tundu Lissu.

Hebu angalia muundo was CCM kuanzia hapo kwenye mtaa unaoishi, angalia kwa sasa kwenye eneo lako la nyumbani kumi muundo wa CCM, angalia WanaCCM hao katika muundo huo katika eneo Hilo la nyumba kumi walivyojipanga na wanavyoendelea kuzisanya kura kwa ajiri ya CCM. Sasa unaona, Kuna kura za Magufuli ambazo atazipata yeye na kura ambazo Chama Cha Mapinduzi kitazipata. Hali hii iliwahi kutokea mwaka 2005 ambapo Jakaya Mrisho Kikwete yeye Kama yeye alipigiwa kura na CCM nayo ikapata kura zilivyounganishwa mkwere akapiga 80%. Lakini 2010 watu wakawa hawana hamu naye, lakini Chama Cha Mapinduzi kikamtafutia kura. Akapiga 61% Kama sikosei, hizi zilikuwa za Chama.

Najua wengi mmejaa kwenye Social Media, hamupo field, hamuoni huo muundo ulivyo hatari. CDM is no where, katika level hizi, CDM ipo mgongoni kwa Lissu. Upande mwingine Kuna CCM Kuna Magufuli na Kuna CCM.

Sasa ukiangalia hali ilivo Sasa unaona kabisa atapigiwa parefu, lakini bahati mbaya hata upande wa Wabunge Mambo ni magumu mno. Majimbo ambayo siku za nyuma yalikuwa ni hoja isiyobishaniwa Sasa mwaka huu ni hoja nzito, Pale Mbeya Sugu amekamatwa Ke....nde, na Dr. Tulia, Lema ameshikwa Pu....bu, na Gambo, hapo Arusha, Mbowe jasho linatirtika hadi kwenye meno, Mzee wa Kondoo wa bwana anapumulia Kisogo Cha Halima. CDM ni Kama wapo kwenye furushi ambalo tarehe 28 linadondoka.

3. Watanzania
Sisi tunayo Kariba ambayo tumejengewa na Mzee Baba mwenyewe, Mchonga, Baba wa Taifa, Julius Kambarage Nyerere. Ni Kariba ambayo unaweza iita utakavyo kulinga a na muono wako, Njema sana, Mbaya, woga, au uungwana.

Watanzania tunapenda Amani Bila kujali gharama yake, Watanzania ni wavumilivu bila kujali gharama, Watanzania tunapenda uungwana sana, hatupendi Shari, lakini mbaya zaidi tunayo Imani Kali kuwa Mabeberu ni watu hatari, na watu wabaya sana. Lakini sisi ni wanafiki, Watanzania ukiwa na sisi tutakueleza hivi, ukitoka tunafanya tofauti, Tunakutanguliza halafu tunasikilizia, upepo ukibadilika tunaingia mitini!

Watanzania ukishaonyesha dalili za ushari, dalili za kuleta uvunjifu wa Amani au ukajinasibisha na Mababeru, au ukasingiziwa Mambo hayo, basi sisi Watanzania tunachofanya, tunakukwepa.

Tarehe 28 Watanzania bila kujali gharama, bila kujari Lissu anaahidi nini Watamkwepa, watajiepusha naye.
Msisahau hapa sijazungumzia swala la CCM kuwa Chama Dora!!

Nimevaa ngao🤣🤣🤣
 
Hatutaki Rais dikteta ,sauti za wananchi kuzizima, bunge letu kuwa kibogoyo, Radio zote kutangaza habari za ccm,magazeti yote kutangaza habari za ccm,watu kupigwa risasi ovyo na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa ,kulagai wakulima kuwa nitanunua mazao lakini ndio kwanza mazao yamekufa, korosho hola, alizeti hola, mpunga hola, kahawa hola biashara nyingi zimefungwa sasa serikali ya namna hii ni ya nini huyu ni Idd Amini wa Tanzania hafai hata kwa kulumagia
 
Kuna watu humu wanajipa moyo eti CDM hii ya Lissu, Mbowe, Mnyika, Heche, Halima, Bulaya Matiko na Wenzake wanaweza kuishinda CCM ya Magufuli, Bashiru Ali, Mangula, na mfumo mzima wa Chama Cha Mapinduzi...
Watanzania wa wapi unawasemea? au watanzania wako binafsi hapo ulipo? Tambua kuwa huu ni mwaka 2020 tayari watanzania wametaabika kwa mateso manyanyaso makubwa wana machungu hasira kubwa hawataki kusikia history za huko nyuma wanakuja kivingine kabsa kusaka Haki na uhuru toka kwa Mkoloni kaburu mweusi
 
Hatutaki Rais dikteta ,sauti za wananchi kuzizima, bunge letu kuwa kibogoyo, Radio zote kutangaza habari za ccm,magazeti yote kutangaza habari za ccm,watu kupigwa risasi ovyo na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa ,kulagai wakulima kuwa nitanunua mazao lakini ndio kwanza mazao yamekufa ,korosho hola,alizeti hola,mpunga hola,kahawa hola biashara nyingi zimefungwa sasa serikali ya namna hii ni ya nini huyu ni Idd Amini wa Tanzania hafai hata kwa kulumagia
Tarehe 28 Tanzania inaenda kupata uhuru upya baada ya manyanyaso mateso makubwa kwa mda wa miaka mitano
 
1603541193490.png
 
Watanzania wa wapi unawasemea? au watanzania wako binafsi hapo ulipo? Tambua kuwa huu ni mwaka 2020 tayari watanzania wametaabika kwa mateso manyanyaso makubwa wana machungu hasira kubwa hawataki kusikia history za huko nyuma wanakuja kivingine kabsa kusaka Haki na uhuru toka kwa Mkoloni kaburu mweusi
Tukutane baada ya Tar. 28 Buda
 
Bora sema wewe, tukisema sisi, tutanyooshewa vidole vya Makada!.
P
Aseme nini? Hakuna cha maana kasema pale zaidi ya porojo tu, Tambua kuwa hakuna mabaya yasiyo na mwisho na sasa CCM inafika mwisho wake Nchi inaenda kupata uhuru upya tokea chato kwa Mkoloni kaburu mweusi na ndipo utawala wa haki utaingia ikulu kuleta usawa maridhiano ya kitaifa
 
Magufuli anaendelea kuwa Rais kwa muhula wa pili, wapiga kelele wa jamiiforums wengi hawapo hata kwenye daftari la mpiga kura + wanatumia multiple IDs ili kuonesha kuwa Lissu yuko juu!

Rais Magufuli ntampigia kura yangu aendelee kuongoza taifa letu, amefanya mazuri mengi ndani ya mda mfupi. Hawa wafuasi wa Lissu wamejitia upofu na kuungana na Lissu wakijinasibu kumuondoa Rais Magufuli

Hawawezi! Ushindi mapemaaaaaa
 
Back
Top Bottom